< Esajas 42 >

1 Se min Tjener, ved hvem jeg holder fast, min udvalgte, hvem jeg har kær! Paa ham har jeg lagt min Aand, han skal udbrede Ret til Folkene.
Tazama, mtumishi wangu, niliyekushika; niliyekuchagua, kwake ninapata furaha. Nimeiweka roho yangu juu yake; ataleta haki kwa mataifa.
2 Han raaber og skriger ikke, løfter ej Røsten paa Gaden,
Hatalia wala kupiga kelele, wala sauti yake haitasikika mitaani.
3 bryder ej knækket Rør og slukker ej rygende Tande. Han udbreder Ret med Troskab,
Mwanzi ulioangamizwa hatauvunja, na wala utambi unaowaka na kutoa mwanga hautaungua: atatekeleza haki kwa uaminifu.
4 vansmægter, udmattes ikke, før han faar sat Ret paa Jorden; og fjerne Strande bier paa hans Lov.
wala hatazimia wala kukata tamaa mpaka atakapoanzisha haki katika nchi; na pwani inasubiria sheria yake.
5 Saa siger Gud HERREN, som skabte og udspændte Himlen, udbredte Jorden med dens Grøde, gav Folkene paa den Aandedræt og dem, som vandrer der, Aande.
Mungu Yahwe asema hivi—yeye aliyeziumba mbingu na yeye zinyoosha nje, yeye aliyeiumba nchi na vitu vyote izalishavyo, yeye aliyewapa punzi watu na wale waishio juu:
6 Jeg, HERREN, har kaldet dig i Retfærd og grebet dig fast om Haand; jeg vogter dig, og jeg gør dig til Folkepagt, til Hedningelys
Mimi Yahwe nimekuita kwa haki yangu na nitakushika kwa mkono wangu. Nitakutunza wewe, na nitakuweka wewe kama agano kwa watu wangu, kama mwanga wa wayunani
7 for at aabne de blinde Øjne og føre de fangne fra Fængslet, fra Fangehullet Mørkets Gæster.
Kuyafungua macho ya vipofu, kuwatoa waliofungwa gerezani, kuwatoa wale walio gizani kutoka kwenye nyumba iliyofungiwa.
8 Jeg er HERREN, saa lyder mit Navn. Jeg giver ej andre min Ære, ej Gudebilleder min Pris.
Mimi ni Yahwe, Hilo ndilo jina langu; na utukufu wangu sitashiriana na mtu mwingine wala sifa zangu sitashirkiana na sanamu ya kuchonga.
9 Hvad jeg forudsagde, se, det er sket, jeg forkynder nu nye Ting, kundgør dem, før de spirer frem.
Tazama, mambo ya nyuma yamekuja na kupita, sasa ninakaribia kutangaza mambo mapya. Kabla hayajaanza kutokea nitawambia kuhusu wao.''
10 Syng HERREN en ny Sang, hans Pris over Jorden vide; Havet og dets Fylde skal juble, fjerne Strande og de, som bebor dem;
Mwimbieni Yahwe wimbo mpya, na sifa zake kutoka mwisho wa nchi; wewe ushukae chini kwenye bahari, na vyote vilivyomo ndani yake, waishio pwani na wale wanaoishi huko.
11 Ørkenen og dens Byer stemmer i, de Lejre, hvor Kedar bor; Klippeboerne jubler, raaber fra Bjergenes Tinder;
Wacha jangwa na miji ilie, vijiji anavyoishi na Kaderi, lia kwa furaha! waache wenyeji wa Sela waimbe; waache wapige kelele juu ya kilele cha mlima.
12 HERREN giver de Ære, forkynder hans Pris paa fjerne Strande.
waache wamtukuze Yahwe na kutangaza sifa zake katika aridhi ya pwani.
13 HERREN drager ud som en Helt, han vækker som en Stridsmand sin Kamplyst, han udstøder Krigsskrig, han brøler, æsker sine Fjender til Strid.
Yahwe atatoka nje kama shujaa; kama mtu wa vita ataichochea bidii yake. Atapiga kelele, ndio, atalia kw kishindo katika vita yake; atawaonyesha adui zake nguvu zake.
14 En Evighed lang har jeg tiet, været tavs og lagt Baand paa mig selv; nu skriger jeg som Kvinde i Barnsnød, stønner og snapper efter Luft.
Nimenyamaza kimyi kwa mda mrefu; bado nimendelea kujizuia mimi mwenyewe; Nitalia kama mwanamke anayetaka kuzaa; nitatweta na kuugua.
15 Jeg gør Bjerge og Høje tørre, afsvider alt deres Grønt, gør Strømme til udtørret Land, og Sumpe lægger jeg tørre.
Nitaiharibu milima na vilima na kukausha uoto wake wa asili; nitajeuza mito kuwa visiwa na nitakausha matindiga.
16 Jeg fører blinde ad ukendt Vej, leder dem ad ukendte Stier, gør Mørket foran dem til Lys og Bakkelandet til Slette. Det er de Ting, jeg gør, og dem gaar jeg ikke fra.
Nitawaleta vipofu kwa njia wasioijua; katika njia wasiyoijua Nitawapitisha wao. Nitaligeuza giza kuwa mwanga mbele yao, na kupanyoosha mahali palipopotoka. Mambo yote haya nitayafanya, na sitaachana na wao.
17 Vige og dybt beskæmmes skal de, som stoler paa Billeder, som siger til støbte Billeder: »I er vore Guder!«
Watageuka nyuma, wataabishwa sana, wale wote wanaoiamini sanamu ya kuchonga, wanaosema na kuziambia sanamu za chuma, ''Nyinyi ni miungu wetu.''
18 I, som er døve, hør, løft Blikket, I blinde, og se!
Sikilizeni ewe kiziwi; tazama, ewe kipofu, ili uweze kuona.
19 Hvo er blind, om ikke min Tjener, og døv som Budet, jeg sendte? Hvo er blind som min haandgangne Mand, blind som HERRENS Tjener?
aliye kipofu ila mtumishi wangu? au kiziwi ni kama mjumbe niliyemtuma? Ni nani aliye kipofu kama mpenzi wangu wa agano, au kipofu kama mtumishi wa Yahwe?
20 Meget saa han, men ænsed det ikke, trods aabne Ører hørte han ej.
Mmeona mambo mengi, lakini hamuelewi; masikio yamefunguka, lakini hakuna anayesikia.
21 For sin Retfærds Skyld vilde HERREN løfte Loven til Højhed og Ære.
Itampendeza Yahwe kuisifu haki yake na kuitukuza sheria yake.
22 Men Folket er plyndret og hærget; de er alle bundet i Huler, skjult i Fangers Huse, til Ran blev de, ingen redder, til Plyndring, ingen siger: »Slip dem!«
Lakini watu hawa ni wale waliokamtw na kutekwa; wote wamenaswa kwenye mashimo; wafungwa wote wamewekwa gerezani; wamekuwa mateka na hakuna hata mmoja wa kuwaokoa wao, hakuna asemaye, warudisheni.''
23 Hvem af jer vil lytte til dette, mærke sig og fremtidig høre det:
Ni nani miongoni mwenu atalisikiliza hili? nani atayasikia na ni nani atasikia wakati ujao?
24 Hvo hengav Jakob til Plyndring, gav Israel hen til Ransmænd? Mon ikke HERREN, mod hvem vi synded, hvis Veje de ej vilde vandre, hvis Lov de ikke hørte?
Ni nani aliyemtoa Yakobo kwa majambazi, na Israeli kwa wanyang'anyi? Je hakuwa Yahwe, dhidi ya wale waliotenda dhambi, waliokataa kutembea katika njia zako na wale waliokataa kusheshimu sheria yako.
25 Han udgød over det Harme, sin Vrede og Krigens Vælde; den luede om det, det ænsed det ej, den sved det, det tog sig det ikke til Hjerte.
Hivyo basi humwaga asira yake kali nje dhidi yao, kwa uharibifu wa vita. Iliwaka kuwazunguka wao, hata hawakujua hilo, lakini hawakuyachukulia hayo moyoni mwao.

< Esajas 42 >