< Prædikeren 10 >

1 Døde Fluer gør Salveblanderens Olie stinkende, lidt Daarskab ødelægger Visdommens Værd.
Kama nzi walio kufa husababisha manukato kutoa harufu ya uozo, hivyo hivyo upumbavu kidogo hushinda hekima na heshima.
2 Den vise har sin Forstand til højre, Taaben har sin til venstre,
Moyo wa mtu mwenye hekima huelekea kulia, lakini moyo wa mpumbavu huelekea kushoto.
3 Hvor Daaren end færdes, svigter hans Forstand, og han røber for alle, at han er en Daare.
Wakati mpumbavu anapotembea barabarani, fikira zake zina upungufu, ikithibitisha kwa kila mtu kwamba ni mpumbavu.
4 Naar en Herskers Vrede rejser sig mod dig, forlad ikke derfor din Plads; thi Sagtmodighed hindrer store Synder.
Kama jaziba za mtawala zikiinuka kinyume na wewe, usiache kazi yako. Utulivu unaweza kutuliza ukatili mkubwa.
5 Der er et Onde, jeg saa under Solen; det ser ud som et Misgreb af ham, som har Magten:
Kuna uovu niliouona chini ya jua, aina ya kosa ambalo huja kutoka kwa mtawala:
6 Daarskab sættes i Højsædet, nederst sidder de rige.
Wapumbavu wanapewa nafasi za uongozi, wakati watu walio faulu wanapewa nafasi za chini.
7 Trælle saa jeg højt til Hest og Høvdinger til Fods som Trælle.
Nimewaona watumwa wakipanda farasi, na watu walio faulu wakitembea kama watumwa juu ya ardhi.
8 Den, som graver en Grav, falder selv deri; den, som nedbryder en Mur, ham bider en Slange;
Yeyote anayechimba shimo anaweza kutumbukia yake, na popote mtu anayevunja ukuja, nyoka anaweza kumuuma.
9 den, som bryder Sten, kan saare sig paa dem; den, som kløver Træ, er i Fare.
Yeyote achongaye mwawe, anaweza kuumizwa nayo. Na mtu achongaye mbao, anaweza kujihatarisha kwa hiyo.
10 Naar Øksen er sløv og dens Æg ej hvæsses, maa Kraft lægges i; men den dygtiges Fortrin er Visdom.
Kama chuma bapa kisicho na makali, na mtu hainoi, kisha ni lazima atumie nguvu nyingi, lakini hekima hutoa faida kwa ufaulu.
11 Bider en Slange, før den besværges, har Besværgeren ingen Gavn af sin Kunst.
Kama nyoka akiuma kabla hajafurahi, hivyo hakuna faida kwa mfurahishaji.
12 Ord fra Vismands Mund vinder Yndest, en Daares Læber bringer ham Vaade;
Maneno ya kinywa cha mtu mwenye hekima yana huruma. Lakini midomo ya mpumbavu humumeza mwenyewe.
13 hans Tale begynder med Daarskab og ender med den værste Galskab.
Kama maneno yanavyo anza kutiririka mdomoni mwa mpumbavu, ujinga hutoka, na mwisho mdomo wake hutiririka wazimu mbaya.
14 Taaben bruger mange Ord. Ej ved Mennesket, hvad der skal ske; hvad der efter hans Død skal ske, hvo siger ham det?
Mpumbavu huongeza maneno, lakini hakuna ajuaye kinachokuja. Ni nani ajuaye baada yake?
15 Daarens Flid gør ham træt, thi end ikke til Bys ved han Vej.
Jasho la wapumbavu huwavaa wao, hivyo hawajui hata barabara ya kwenda mjini.
16 Ve dig, du Land, hvis Konge er en Dreng og hvis Fyrster holder Gilde ved Gry.
Ole wako ardhi kama mfalme wako ni kijana mdogo, na kama viongozi wako huanza karamu ahsubuhi!
17 Held dig; du Land, hvis Konge er ædelbaaren, hvis Fyrster holder Gilde til sømmelig Tid som Mænd og ikke som Drankere.
Lakini umebarikiwa ardhi kama mfalme wako ni mwana wa waungwana, na kama vingozi wako hula wakati muafaka, kwa nguvu, na sio kwa ulevi.
18 Ved Ladhed synker Bjælkelaget; naar Hænderne slappes, drypper det i Huset.
Kwa sababu ya uvivu paa huanguka. Na kwa sababu isiyo fanya kazi nyumba hupata ufa.
19 Til Morskab holder man Gæstebud, og Vin gør de levende glade; men Penge skaffer alt til Veje.
Watu huandaa chakula kwa kicheko, divai huleta furaha maishani, na fedha hutimiza hitaji kwa kila kitu.
20 End ikke i din Tanke maa du bande en Konge, end ikke i dit Sovekammer en, som er rig; thi Himlens Fugle kan udsprede Ordet, de vingede røbe, hvad du siger.
Usimlaani mfalme, hata katika akili, na usiwalaani wenye mali katika chumba chako cha kulala. Kwa kuwa ndege wa angani inaweza kuchukua maneno yako. Chochote kilicho na mabawa kinaweza kusambaza jambo.

< Prædikeren 10 >