< Židům 3 >
1 Proto se, bratři Bohem povolaní a Bohu oddaní, snažte poznávat Ježíše, který byl Božím vyslancem na zemi a nyní je naším zástupcem u Boha.
Kwa hiyo, ndugu watakatifu, washiriki wa wito wa mbinguni, mumfikiri Yesu, Mtume na Kuhani Mkuu wa ukiri wetu.
2 Nezpronevěřil se Bohu, který jej ustanovil. Byl věrný jako Mojžíš, který se staral o Boží lid.
Alikuwa mwaminifu kwa Mungu aliyemteua, kama Musa alivyokuwa mwaminifu pia katika nyumba yote ya Mungu.
3 Ale Ježíš převyšuje Mojžíše, jako tvůrce převyšuje své dílo. Vždyť on jako Bůh stvořil vše.
Kwa kuwa Yesu amehesabiwa kuwa na heshima kubwa kuliko aliyokuwa nayo Musa, kwa sababu yule anayejenga nyumba anahesabiwa kuwa na heshima kubwa kuliko nyumba yenyewe.
Kwa kuwa kila nyumba hujengwa na mtu fulani, lakini yule anayejenga kila kitu ni Mungu.
5 Mojžíš byl pouze svědek toho, co pověděl Bůh. Byl věrný služebník Božího lidu.
Hakika Musa alikuwa mwaminifu kama mtumishi katika nyumba yote ya Mungu, akitoa ushuhuda kuhusu mambo yatakayosemwa wakati ujao.
6 Kristus však jako Boží Syn je naším Pánem a zůstane jím, jestliže si až do konce zachováme pevnou jistotu a radostnou naději.
Lakini Kristo ni Mwana katika usimamizi wa nyumba ya Mungu. Sisi ni nyumba yake kama tutashikilia haraka katika kujiamini na fahari ya kujiamini.
7 Proto nás Duch svatý napomíná: „Když dnes zaslechnete jeho hlas,
Kwa hiyo, ni kama Roho Mtakatifu asemavyo, “Leo, kama utasikia sauti yake,
8 nezatvrzujte se ve vzdoru proti němu jako Izraelci při zkoušce na poušti,
Usiufanye moyo wako kuwa mgumu kama Waisraeli walivyofanya katika uasi, katika wakati wa kujaribiwa nyikani.
9 kde si vaši otcové žádali důkazy a tak mne pokoušeli.
Huu ulikuwa wakati ambao baba zenu waliniasi kwa kunijaribu, na wakati, kwa miaka arobaini, waliona matendo yangu.
10 To pokolení se mi zošklivilo a řekl jsem: ‚Nerozumí sami sobě, ani nechápou mé cesty.
Kwa hiyo sikufurahishwa na kizazi hicho. Nilisema, 'Wanapotea kila mara katika mioyo yao, na hawajui njia zangu.
11 Proto jsem v hněvu přísahal, že nedosáhnou odpočinku, který jsem jim připravil.‘“
Ni kama vile nilivyoapa katika hasira yangu: hawataiingia raha yangu.”
12 Dejte si tedy pozor, bratři, aby se ve vás neuhnízdilo zlo a nevěra, které by vás odváděly od živého Boha.
Muwe waangalifu, ndugu, ili kwamba usije ukawepo moyo mwovu wa kutokuamini kwa mmoja wenu, moyo ambao utakwenda mbali na Mungu aliye hai.
13 Zkoumejte se každý den, dokud je k tomu příhodná chvíle, aby se někdo z vás nezatvrdil zaslepující a mámivou svůdností hříchu.
Badala yake, mhamasishane kila siku kila mmoja na mwenzie, ili kila iitwapo leo mtamani, ili kwamba mmoja kati yenu asifanywe kuwa mgumu kwa udanganyifu wa dhambi.
14 Máme podíl na všem, co náleží Kristu, když setrváme do konce v počáteční důvěře. Ale vraťme se ke slovům:
Kwa maana tumekuwa washiriki wa Kristo ikiwa tutashikamana na uthabiti wetu kwa nguvu katika yeye kutoka mwanzo hadi mwisho.
15 „Když dnes zaslechnete Boží hlas, nezatvrzujte se vzpurně proti němu.“
Kuhusu hili imekwisha kusemwa, “Leo kama mtaisikiliza sauti yake, msiifanye mioyo yenu kuwa migumu, kama Waisraeli walivyofanya wakati wa uasi.”
16 Kdo se to vlastně vzbouřil, když zaslechl Boží hlas? Ti, které Mojžíš vyvedl z Egypta.
Ni akina nani hao waliomsikia Mungu na kuasi? Hawakuwa wale wote ambao Musa alikuwa amewaongoza kutoka Misri?
17 A koho měl Bůh v ošklivosti po čtyřicet let? Ty neposlušné, kteří pak zahynuli na poušti.
Na kina nani ambao Mungu aliwakasirikia kwa miaka arobaini? Siyo pamoja na wale waliotenda dhambi, ambao miili yao iliyokufa ililala jangwani?
18 Přísahal jim, že nedosáhnou odpočinku, který jim připravil. Nemohli ho dosáhnout pro nevěru.
Ni akina nani aliowaapia Mungu kwamba hawataingia katika raha yake, kama siyo wale ambao hawakumtii yeye?
Tunaona kwamba hawakuweza kuingia katika raha yake kwa sababu ya kutokuamini.