< 3 Mojžišova 20 >

1 Mluvil pak Hospodin k Mojžíšovi, řka:
Bwana akamwambia Mose,
2 Synům také Izraelským díš: Kdo by koli z synů Izraelských a z příchozích, kteříž by byli pohostinu v Izraeli, dal z semene svého modle Moloch, smrtí umře. Lid země té kamením jej uhází.
“Sema na wana wa Israeli: ‘Mwisraeli yeyote au mgeni anayeishi katika Israeli ambaye atamtoa yeyote miongoni mwa watoto wake kuwa sadaka kwa mungu Moleki, mtu huyo lazima auawe. Watu wa jumuiya hiyo watampiga kwa mawe.
3 Nebo já postavím tvář svou proti takovému, a vyhladím ho z prostředku lidu jeho, proto že z semene svého dal modle Moloch, a tak zprznil svatyni mou, a poškvrnil jména svatosti mé.
Mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu huyo, nami nitamkatilia mbali na watu wake. Kwa maana kwa kumtoa mmoja wa watoto wake kwa mungu Moleki, amenajisi madhabahu yangu na kulinajisi Jina langu takatifu.
4 Jestliže by pak lid země té všelijak přehlídal to na člověku tom, kterýž by dal z semene svého modle Moloch, a nezahubil by ho:
Ikiwa watu wa jumuiya watafumba macho wakati mtu huyo anapomtoa mmoja wa watoto wake kwa mungu Moleki, nao wakaacha kumuua,
5 Tedy já postavím tvář svou proti muži tomu a proti čeledi jeho, a vyhladím ho i všecky, kteříž smilníce, odcházeli po něm, aby smilnili, následujíce Molocha, z prostředku lidu jeho.
mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu huyo pamoja na jamaa yake, nami nitawakatilia mbali yeye na watu wote waliofanya ukahaba na Moleki.
6 Duše, kteráž by se obrátila k hadačům a věšťcům, aby smilnila, postupujíc po nich: postavím tvář svou proti duši té, a vyhladím ji z prostředku lidu jejího.
“‘Mimi nitauelekeza uso wangu dhidi ya mtu anayeenda kwa waaguzi na wenye pepo, na hivyo kujifanyia ukahaba kwa kuwafuata, nami nitamkatilia mbali na watu wake.
7 A protož posvěťte se a buďte svatí, nebo já jsem Hospodin Bůh váš.
“‘Jitakaseni basi, nanyi kuweni watakatifu, kwa sababu mimi ndimi Bwana Mungu wenu.
8 A ostříhejte ustanovení mých, a čiňte je: Já jsem Hospodin posvětitel váš.
Shikeni amri zangu na kuzifuata. Mimi ndimi Bwana, niwafanyaye ninyi watakatifu.
9 Kdož by koli zlořečil otci svému neb matce své, smrtí umře. Otci svému a matce své zlořečil, krev jeho bude na něm.
“‘Ikiwa mtu yeyote atamlaani baba yake au mama yake, lazima auawe. Amemlaani baba yake au mama yake, nayo damu yake itakuwa juu ya kichwa chake mwenyewe.
10 Muž pak, kterýž by se cizoložství dopustil s ženou něčí, že zcizoložil s ženou bližního svého, smrtí umře cizoložník ten i cizoložnice.
“‘Ikiwa mtu atazini na mke wa mtu mwingine, yaani mke wa jirani yake, wazinzi hao wawili lazima wauawe.
11 A kdož by koli obcoval s ženou otce svého, hanbu otce svého odkryl. Smrtí umrou oba dva, krev jejich bude na ně.
“‘Kama mtu atakutana kimwili na mke wa baba yake, hakumheshimu baba yake. Mwanaume huyo na mwanamke huyo wote wauawe; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.
12 Kdož by pak obcoval s nevěstou svou, smrtí umrou oba dva. Mrzkosti se dopustili, krev jejich bude na ně.
“‘Ikiwa mtu atakutana kimwili na mke wa mwanawe, lazima wote wawili wauawe. Walichokifanya ni upotovu; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.
13 A kdož by se scházel s pohlavím mužským jako s ženou, ohavnost učinili oba dva. Smrtí umrou, krev jejich bude na ně.
“‘Kama mwanaume akikutana kimwili na mwanaume mwenzake kama vile mwanaume afanyavyo na mwanamke, wanaume hao wawili wamefanya lililo chukizo sana. Lazima wauawe; nayo damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.
14 A kdož by vzal ženu a matku její, nešlechetnost jest. Ohněm spálí i jej i je, aby nebylo nešlechetností u prostřed vás.
“‘Ikiwa mwanaume ataoa binti pamoja na mama yake, huo ni uovu. Wote watatu ni lazima wachomwe moto, ili kwamba pasiwepo na uovu katikati yenu.
15 Kdož by pak obcoval s hovadem, smrtí umře, a hovado zabijete.
“‘Kama mwanaume akikutana kimwili na mnyama, ni lazima auawe, na pia ni lazima mnyama huyo auawe.
16 Tolikéž žena, kteráž by přistoupila k některému hovadu, aby obcovala s ním, zabiješ ji i to hovado. Smrtí umrou, krev jejich bude na ně.
“‘Kama mwanamke atamsogelea mnyama kukutana naye kimwili, muueni mwanamke huyo pamoja na mnyama pia. Lazima wauawe; damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.
17 Kdož by koli vezma sestru svou, dceru otce svého, aneb dceru matky své, viděl by hanbu její, a ona také viděla by hanbu jeho, mrzkost jest. Protož vyhlazeni budou před očima synů lidu svého; nebo hanbu sestry své odkryl, nepravost svou ponese.
“‘Ikiwa mtu anamwoa dada yake, binti aliyezaliwa na baba yake au mama yake, nao wakakutana kimwili, ni aibu. Lazima wakatiliwe mbali machoni pa watu wao. Huyo mwanaume amemwaibisha dada yake, hivyo atawajibika kwa ajili ya uovu huo.
18 A kdož by koli spal s ženou v její nemoci a obnažil by hanbu její, a tok její by odkryl, i ona ukázala by krvotok svůj: vyhlazeni budou oba z prostředku lidu svého.
“‘Ikiwa mwanaume atalala na mwanamke aliye katika hedhi yake na kukutana naye kimwili, amefunua mtiririko wa hedhi yake, naye huyo mwanamke amejifunua uchi wake. Wote wawili lazima wakatiliwe mbali na watu wao.
19 Hanby sestry matky své a sestry otce svého neodkryješ. Nebo kdož by to učinil, krevní přítelkyni svou by obnažil; protož nepravost svou ponesou.
“‘Usikutane kimwili na dada wa mama yako wala wa baba yako, kwa maana hilo litamwaibisha jamaa wa karibu; ninyi wawili mtawajibika kwa ajili ya uovu huo.
20 Kdož by pak spal s ženou strýce svého, hanbu strýce svého odkryl. Ponesou hřích svůj, bez dětí zemrou.
“‘Ikiwa mwanaume atakutana kimwili na shangazi yake, amemwaibisha mjomba wake. Nao watawajibika kwa ajili ya uovu huo; watakufa bila kuzaa mtoto.
21 Tolikéž kdož by vzal manželku bratra svého, mrzkost jest. Hanbu bratra svého obnažil, protož bez dětí budou.
“‘Ikiwa mwanaume ataoa mke wa ndugu yake, hili ni tendo chafu; amemwaibisha ndugu yake. Nao hawatazaa mtoto.
22 Ostříhejtež tedy všech ustanovení mých a všech soudů mých, a čiňte je, aby nevyvrátila vás země, do níž já uvozuji vás, abyste v ní bydlili.
“‘Zishikeni amri na sheria zangu zote na kuzifuata, ili nchi ninayowaleta kuishi isiwatapike.
23 Aniž choďte v ustanoveních národu toho, kterýž já vyvrhu od tváři vaší; nebo všecky ty věci činili, a měl jsem je v ošklivosti.
Kamwe msiishi kwa kufuata desturi za mataifa nitakayoyafukuza mbele yenu. Kwa sababu walifanya mambo haya yote, nami nikachukizwa sana nao.
24 Vám jsem pak řekl: Vládnouti budete zemí jejich, a já dám ji vám, abyste ji dědičně obdrželi, zemi tekoucí mlékem a strdí. Já jsem Hospodin Bůh váš, kterýž jsem vás oddělil od jiných národů.
Lakini niliwaambia ninyi, “Mtaimiliki nchi yao; nitawapa ninyi kuwa urithi, nchi inayotiririka maziwa na asali.” Mimi ndimi Bwana Mungu wenu, ambaye amewatenga kutoka mataifa.
25 Protož vy mějte rozdíl mezi hovadem čistým a nečistým, a mezi ptákem čistým a nečistým, a nepoškvrňujte duší svých hovady a ptactvem, a tím vším, což se plazí po zemi, kteréž jsem já vám oddělil, abyste je měli za nečisté.
“‘Kwa hiyo, ninyi lazima mweze kutofautisha kati ya wanyama walio safi na wasio safi, pia kati ya ndege wasio safi na walio safi. Msijitie unajisi kutokana na mnyama yeyote, au ndege, wala kitu chochote kitambaacho juu ya ardhi, vile ambavyo nimevitenga kuwa najisi kwa ajili yenu.
26 Ale budete mi svatí; nebo svatý jsem já Hospodin, a oddělil jsem vás od jiných národů, abyste byli moji.
Mtakuwa watakatifu kwangu, kwa sababu Mimi, Bwana, ni mtakatifu, nami nimewatenga kutoka mataifa kuwa wangu mwenyewe.
27 Muž pak neb žena, kteříž by měli ducha čarodějného a věštího, smrtí umrou. Kamením uházejí je, krev jejich bude na ně.
“‘Mwanaume au mwanamke ambaye ni mchawi, mwaguzi au mwenye kupunga pepo miongoni mwenu lazima auawe. Mtawapiga kwa mawe; nayo damu yao itakuwa juu ya vichwa vyao wenyewe.’”

< 3 Mojžišova 20 >