< Jan 19 >

1 Tedy vzal Pilát Ježíše, a zbičoval.
Basi Pilato alimchukua Yesu na kumchapa.
2 A žoldnéři zpletše korunu z trní, vstavili na hlavu jeho, a pláštěm šarlatovým přioděli jej.
Wale maaskari wakasokota miiba na kutengeneza taji. Wakaiweka juu ya kichwa cha Yesu na kumvalisha vazi la rangi ya zambarau.
3 A říkali: Zdráv buď, králi Židovský. A bili jej hůlkami.
Wakamjia na kusema, “Wewe mfalme wa Wayahudi! na kisha kumpiga kwa mikono yao.
4 I vyšel opět ven Pilát, a řekl jim: Aj, vyvedu jej vám ven, abyste poznali, žeť na něm žádné viny nenalézám.
Kisha Pilato alitoka nje na kuwaambia watu, “Tazama nawaleteeni huyu mtu kwenu ili mjue kwamba mimi sikuona hatia yoyote ndani yake.”
5 Tedy vyšel Ježíš ven, nesa tu korunu trnovou, a ten plášť šarlatový. I řekl jim Pilát: Aj člověk.
Kwa hiyo Yesu akatoka nje; alikuwa amevaa taji ya miiba na vazi la zambarau. Ndipo Pilato akawaambia, “Tazameni mtu huyu hapa!”
6 A jakž jej uzřeli přední kněží a služebníci, zkřikli, řkouce: Ukřižuj, ukřižuj ho. Dí jim Pilát: Vezměte vy jej a ukřižujte, nebo já na něm viny nenalézám.
Kwa hiyo wakati kuhani mkuu na wakuu walipomwona Yesu, wakapiga kelele wakisema, “Msulubishe, msulubishe.” Pilato akawaambia, “Mchukueni ninyi wenyewe mkamsulubishe, kwa kuwa mimi sioni hatia ndani yake.”
7 Odpověděli jemu Židé: My zákon máme, a podlé zákona našeho máť umříti, nebo Synem Božím se činil.
Wayahudi wakamjibu Pilato, “Sisi tunayo sheria, na kwa sheria hiyo inampasa kufa kwa sababu yeye alijifanya kuwa mwana wa Mungu.”
8 A když Pilát uslyšel tuto řeč, více se obával.
Pilato aliposikia maneno haya alizidi kuogopa,
9 I všel do radného domu zase, a řekl Ježíšovi: Odkud jsi ty? Ale Ježíš nedal jemu odpovědi.
akaingia Praitorio tena na kumwambia Yesu, “Wewe unatoka wapi? Hata hivyo, Yesu hakumjibu.
10 Tedy řekl jemu Pilát: Nemluvíš se mnou? Nevíš-liž, že mám moc ukřižovati tě, a moc mám propustiti tebe?
Kisha Pilato akamwambia, “Je, wewe huongei na mimi? Je, wewe hujui kuwa mimi nina mamlaka ya kukufungua na mamlakaya kukusulubisha?”
11 Odpověděl Ježíš: Neměl bys nade mnou moci nižádné, byť nebylo dáno s hůry; protož kdo mne tobě vydal, většíť hřích má.
Yesu akamjibu, “Usingekuwa na nguvu dhidi yangu kama usingepewa toka juu. Kwa hiyo, mtu aliyenitoa kwako ana dhambi kubwa.”
12 Od té chvíle hledal Pilát propustiti ho. Ale Židé volali, řkouce: Propustíš-li tohoto, nejsi přítel císařův; každý, kdož se králem činí, protiví se císaři.
Kutokana na jibu hili, Pilato akataka kumwacha huru, lakini Wayahudi wakapiga kelele wakisema, “Kama utamwacha huru basi wewe si rafiki wa Kaisari: Kila ajifanyaye kuwa mfalme hunena kinyume cah kaisari.”
13 Tedy Pilát uslyšev tu řeč, vyvedl ven Ježíše, a sedl na soudné stolici na místě, kteréž slove Litostrotos, a Židovsky Gabbata.
Pilato alipoyasikia maneno haya, akamleta Yesu nje kisha akakaa kwenye kiti cha hukumu mahali pale panapojulikana kama sakafu, lakini kwa Kiebrania, Gabatha.
14 A bylo v pátek před velikonocí, okolo šesté hodiny. I řekl Židům: Aj, král váš.
Siku ya maandalizi ya pasaka ilipofika, panapo muda wa saa ya sita. Pilato akawaambia Wayahudi, “Tazameni mfalme wenu huyu hapa!”
15 Oni pak zkřikli: Vezmi, vezmi, ukřižuj jej. Řekl jim Pilát: Krále vašeho ukřižuji? Odpověděli přední kněží: Nemámeť krále, než císaře.
Wakapiga kelele, “Mwondoshe, mwondoshe, msulubishe!” Pilato akawaambia, “Je, nimsulubishe mfalme wenu?” Naye Kuhani mkuu akajibu, “Sisi hatuna mfalme isipokuwa Kaisari.”
16 Tehdy vydal jim ho, aby byl ukřižován. I pojali Ježíše a vedli.
Ndipo Pilato alipomtoa Yesu kwao ili asulibiwe.
17 A nesa kříž svůj, šel na místo, kteréž slove popravné, a Židovsky Golgota.
Nao wakamchukua Yesu, naye akatoka, hali ameubeba msalaba wake mwenyewe mpaka kwenye eneo liitwalo fuvu la kichwa, kwa Kihebrania huitwa Golgotha.
18 Kdež ukřižovali ho, a s ním jiné dva s obou stran, a v prostředku Ježíše.
Ndipo walipomsulibisha Yesu, pamoja naye wanaume wawili, mmoja upende huu na mwingine upande huu, na Yesu katikati yao.
19 Napsal pak i nápis Pilát, a vstavil na kříž. A bylo napsáno: Ježíš Nazaretský, král Židovský.
Kisha Pilato akaandika alama na kuiwekwa juu ya msalaba. Hapo paliandikwa: YESU MNAZARETH, MFALME WA WAYAHUDI.
20 Ten pak nápis mnozí z Židů čtli; nebo blízko města bylo to místo, kdež ukřižován byl Ježíš. A bylo psáno Židovsky, Řecky a Latině.
Wengi wa Wayahudi waliisoma alama hiyo kwani mahali pale aliposulibishwa Yesu palikuwa karibu na mji. Alama hiyo iliadikwa kwa Kiebrania, kwa Kirumi na kwa Kiyunani.
21 Tedy přední kněží Židovští řekli Pilátovi: Nepiš: Král Židovský, ale že on řekl: Král Židovský jsem.
Kisha wakuu wa makuhani wa Wayahudi wakamwambia Pilato, “Usiandike, 'Mfalme wa Wayahudi; bali yeye alisema mimi ni mfalme wa Wayahudi.”
22 Odpověděl Pilát: Co jsem psal, psal jsem.
Naye Pilato akawajibu, “Niliyoandika nimeandika.”
23 Žoldnéři pak, když Ježíše ukřižovali, vzali roucha jeho, (a učinili čtyři díly, každému rytíři díl, ) a sukni. Byla pak sukně nesšívaná, ale od vrchu všecka naskrze setkaná.
Baada ya askari kumsulibisha Yesu, walichukua mavazi yake na kuyagawa katika mafungu manne, kila askari fungu moja, vivyo hivyo na kanzo, Sasa ile kanzu haikuwa imeshonwa bali ilkuwa imefumwa yote tokea juu.
24 I řekli mezi sebou: Neroztrhujme jí, ale losujme o ni, čí bude. Aby se naplnilo písmo, řkoucí: Rozdělili sobě roucho mé, a o můj oděv metali los. Tedy žoldnéři tak učinili.
Kisha wakasemezana wao kwa wao, “Tusiipasue, bali tupigeni kura ili kuona itakuwa ya nani.” Hili lilitokea ili lile andiko litimizwe, lile lisemalo waligawanya nguo zangu, na vazi langu wakalipigia kura.”
25 Stály pak u kříže Ježíšova matka jeho a sestra matky jeho, Maria Kleofášova, a Maria Magdaléna.
Askari walifanya mambo haya. Mama yake Yesu, dada wa mama yake, Mariamu mke wa Kleopa na Mariamu Magdalena - wanawake hawa walikuwa wamesimama karibu na msalaba wa Yesu.
26 Tedy Ježíš uzřev matku, a učedlníka tu stojícího, kteréhož miloval, řekl matce své: Ženo, aj, syn tvůj.
Yesu alipomwona mama yake pamoja na yule mwanafunzi aliyempenda wakisimama karibu, akamwambia mama yake, “Mwanamke, tazama, ona mwanao huyu hapa!”
27 Potom řekl učedlníkovi: Aj, matka tvá. A od té hodiny přijal ji učedlník ten k sobě.
Kisha akamwambia yule mwanfunzi, “Tazama, huyu hapa mama yako. “Tokea saa hiyo yule mwanafunzi akamchukua kwenda nyumbani kwake.
28 Potom věda Ježíš, že již všecko dokonáno jest, aby se naplnilo písmo, řekl: Žízním.
Baada ya hilo, Hali Yesu akijua kuwa yote yamekwisha kumalizika ili kutimiza maandiko, akasema, “Naona kiu.”
29 Byla pak tu postavena nádoba plná octa. Tedy oni naplnivše hubu octem, a obloživše yzopem, podali ústům jeho.
Chombo kilichokuwa kimejaa Siki kilikuwa kimewekwa pale, kwa hiyo wakaweka sifongo iliyojaa siki juu ya ufito wa hisopo, wakamwekea mdomoni mwake.
30 A když okusil Ježíš octa, řekl: Dokonánoť jest. A nakloniv hlavy, ducha Otci poručil.
Naye Yesu alipoionja hiyo, akasema, “Imekwisha.” Kisha akainamisha kichwa chake, akaikabidhi roho yake.
31 Židé pak, aby nezůstala na kříži těla na sobotu, poněvadž byl den připravování, (byl zajisté veliký ten den sobotní, ) prosili Piláta, aby zlámáni byli hnátové jejich, a byli složeni.
Kwa vile ilikuwa ni wakati wa maandalio, na kwa sababu miili haikutakiwa kubaki juu ya msalaba wakati wa Sabato (kwa kuwa Sabato ilikuwa siku ya muhimu), wayahudi walimwomba Pilato kuwa miguu yao wale wliokuwa wamesulibishwa ivunjwe, na kwamba miili yao ishushwe.
32 I přišli žoldnéři, a prvnímu zajisté zlámali hnáty, i druhému, kterýž ukřižován byl s ním.
Ndipo askari walipokuja na kuvunja miguu ya mtu wa kwanza na wa pili aliyekuwa amesulibiwa pamoja na Yesu.
33 Ale k Ježíšovi přišedše, jakž uzřeli jej již mrtvého, nelámali hnátů jeho.
Walipomfikia Yesu, walimkuta tayari alikuwa amekwisha kufa, kwa hiyo hawakuvunja miguu yake.
34 Ale jeden z žoldnéřů bok jeho kopím otevřel, a hned vyšla krev a voda.
Hata hivyo, mmoja wa askari alimchoma Yesu ubavuni kwa mkuki, na mara yakatoka maji na damu.
35 A ten, kterýž viděl, svědectví vydal, a pravé jest svědectví jeho. Onť ví, že pravé věci praví, abyste vy věřili.
Naye aliyeona hili ametoa ushuhuda, na ushuhuda wake ni wa kweli. Yeye anajua kuwa alichokisema ni cha kweli ili nanyi pia muamini.
36 Stalo se pak to, aby se naplnilo to písmo: Kost jeho nebude zlámána.
Mambo haya yalikuwa ili lile neno lililonenwa lipate kutimia, “Hakuna hata wake mmoja utakaovunjwa.”
37 A opět jiné písmo dí: Uzříť, v koho jsou bodli.
Tena andiko lingine husema, “Watamtazama yeye waliyemchoma”
38 Potom pak prosil Piláta Jozef z Arimatie, (kterýž byl učedlník Ježíšův, ale tajný, pro strach Židovský, ) aby sňal tělo Ježíšovo. I dopustil Pilát. A on přišed, sňal tělo Ježíšovo.
Baada ya mambo haya Yusufu wa Arimathaya, kwa vile alikuwa mwanafunzi wa Yesu, lakini kwa siri kwa kuwaogopa Wayahudi, alimwomba Pilato kwamba auchukue mwili wa Yesu. Naye Pilato akampa ruhusa. Kwa hiyo Yusufu akaja kuuondoa mwili wa Yesu.
39 Přišel pak i Nikodém, (kterýž byl prvé přišel k Ježíšovi v noci, ) nesa smíšení mirry a aloes okolo sta liber.
Naye Nicodemo ambaye hapo awali alimfuata Yesu usiku naye akaja. Yeye alileta mchanganyiko wa manemane na udi, yapata uzito wa ratili mia moja.
40 Tedy vzali tělo Ježíšovo, a obvinuli je prostěradly s těmi vonnými věcmi, jakž obyčej jest Židům se pochovávati.
Kwa hiyo wakauchukua mwili wa Yesu wakaufanga kwenye sanda ya kitani na pamoja na yale manukato, kama ilivyokuwa desturi ya wayahudi wakati wa kuzika.
41 A byla na tom místě, kdež ukřižován byl, zahrada, a v zahradě hrob nový, v němž ještě žádný nebyl pochován.
Mahali ambapo Yesu alisulibiwa kulikuwa na bustani; ndani ya ile bustani kulikuwa na kaburi jipya ambalo hakuna mtu alikuwa amawahi kuzikwa humo.
42 Protož tu pro den připravování Židovský, že blízko byl ten hrob, položili Ježíše.
Basi, kwa kuwa ilikuwa siku ya maandalio kwa Wayahudi, na kwa vile lile kaburi lilikuwa karibu, basi wakamlaza Yesu ndani yake.

< Jan 19 >