< Ezechiel 46 >
1 Takto praví Panovník Hospodin: Brána síně vnitřní, kteráž patří k východu, bude zavřená po šest dní všedních, v den pak sobotní otevřína bude; též v den novměsíce otvírána bude.
“‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Lango la ukumbi wa ndani linaloelekea upande wa mashariki litakuwa linafungwa kwa siku sita za juma, ila siku ya Sabato na siku ya Mwezi Mwandamo litafunguliwa.
2 I přijde kníže cestou síně brány zevnitř, a postaví se u veřeje té brány, a budou obětovati kněží obět zápalnou jeho, i oběti pokojné jeho, a pokloně se na prahu brány, potom vyjde. Brána pak nebude zavírána do večera,
Mkuu anayetawala ataingia kupitia baraza ya njia ya lango la ukumbi na kusimama karibu na nguzo ya lango. Makuhani watatoa sadaka za mkuu anayetawala za kuteketezwa na sadaka za amani. Mkuu anayetawala atasujudu kwenye kizingiti cha njia ya lango, kisha atatoka nje, lakini lango halitafungwa mpaka jioni.
3 Aby se klaněl lid země té u dveří brány té ve dny sobotní, i na novměsíce před Hospodinem.
Siku za Sabato na za Mwezi mwandamo watu wote wa nchi wataabudu mbele za Bwana penye lile ingilio la ile njia.
4 Obět pak zápalná, kterouž obětovati má kníže Hospodinu v den sobotní, šest beránků bez vady a skopec bez poškvrny,
Sadaka ya kuteketezwa aletazo mkuu anayetawala kwa Bwana siku ya Sabato itakuwa ni wana-kondoo sita na kondoo dume mmoja, wote wasiwe na dosari.
5 A obět suchá, efi na skopce, i na beránky obět suchá, podlé toho, jakž naděleno, a oleje hin na efi.
Sadaka ya nafaka inayotolewa pamoja na huyo kondoo dume itakuwa efa moja na sadaka ya nafaka inayotolewa na hao wana-kondoo itakuwa kiasi apendacho mtu pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa.
6 Ke dni pak novměsíce ať jest volek mladý bez poškvrny, a šest beránků i skopec bez poškvrny.
Siku ya mwezi mwandamo atatoa fahali mchanga, wana-kondoo sita na kondoo dume, wote wasiwe na dosari.
7 Též ať obětuje efi oběti suché při volku, a efi při skopci i při beráncích, seč bude moci býti, a oleje hin na efi.
Atatoa kuwa sadaka ya nafaka efa moja pamoja na fahali mmoja, efa moja na kondoo dume mmoja na pamoja na wana-kondoo kama atakavyo kutoa, pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa.
8 Kníže pak vcházeje, cestou síňce též brány půjde, a cestou její odejde.
Wakati mkuu anayetawala aingiapo, atapitia kwenye baraza ya njia ya lango, naye atatoka nje kwa njia hiyo hiyo.
9 Ale když vcházeti bude lid země té před Hospodina na slavnosti, ten kdož vejde cestou brány půlnoční, aby se klaněl, vyjde cestou brány polední; a ten kdož vejde cestou brány polední, vyjde cestou brány půlnoční. Nenavrátí se cestou té brány, kterouž všel, ale naproti ní vyjde.
“‘Wakati watu wa nchi wanapokuja mbele za Bwana katika sikukuu zilizoamriwa, yeyote aingiaye kwa lango la kaskazini kuabudu atatoka nje kwa lango la kusini na yeyote aingiaye kwa lango la kusini atatoka nje kwa lango la kaskazini. Hakuna mtu yeyote atakayerudi kwa kupitia lango lile aliloingilia, lakini kila mmoja atatoka nje kwa lango linalokabili lile aliloingilia.
10 A když oni vcházeti budou, kníže mezi nimi vcházeti bude, a když odcházeti budou, odejde.
Mkuu anayetawala atakuwa miongoni mwao, akiingia nao ndani wanapoingia, naye atatoka nao nje wanapotoka.
11 Též na svátky i na slavnosti ať jest suchá obět, efi na volka a efi na skopce, a na beránky, což naděleno, a oleje hin na efi.
“‘Kwenye sikukuu na kwenye sikukuu zilizoamriwa, sadaka ya nafaka itakuwa efa moja pamoja na fahali mmoja, efa moja pamoja na kondoo dume mmoja, pamoja na idadi ya wana-kondoo kama mtu apendavyo kutoa, pamoja na hini ya mafuta kwa kila efa.
12 Bude-li pak obětovati kníže obět dobrovolnou, zápal aneb oběti pokojné dobrovolně Hospodinu, tedy ať jest mu otevřína brána, kteráž k východu patří, a ať obětuje zápal svůj aneb pokojné oběti své, tak jakž obětuje v den sobotní. Potom odejde, a brána bude zavřína po odchodu jeho.
Mkuu anayetawala anapotoa sadaka ya hiari kwa Bwana, ikiwa ni sadaka ya kuteketezwa au sadaka ya amani, lango linaloelekea mashariki litafunguliwa kwa ajili yake. Atatoa sadaka yake ya kuteketezwa au sadaka yake ya amani kama afanyavyo katika siku ya Sabato. Kisha atatoka nje, naye akiisha kutoka nje, lango litafungwa.
13 K tomu beránka ročního bez poškvrny obětovati bude v zápal každý den Hospodinu; každého jitra beránka obětovati bude.
“‘Kila siku utamtoa mwana-kondoo wa mwaka mmoja asiyekuwa na dosari kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa kwa Bwana, utaitoa kila siku asubuhi.
14 Též suchou obět přičiní k němu, každého jitra šestý díl efi, též oleje třetinu hin k skropení mouky bělné, suchou obět Hospodinu, nařízením věčným ustavičně.
Pia kila siku asubuhi pamoja na hiyo sadaka utatoa sadaka ya nafaka, ikiwa na sehemu ya sita ya efa pamoja na theluthi moja ya hini ya mafuta ya kuchanganya na ule unga. Utoaji wa sadaka hii ya nafaka kwa Bwana ni amri ya daima.
15 A tak budou obětovati beránka i obět suchou, i olej každého jitra, zápal ustavičný.
Kwa hiyo mwana-kondoo na sadaka ya nafaka na mafuta vitatolewa kila siku asubuhi kwa ajili ya sadaka ya daima ya kuteketezwa.
16 Taktoť praví Panovník Hospodin: Dá-li kníže dar někomu z synů svých, dědictvíť jeho jest, synů jeho buď, k vládařství jejich dědičnému.
“‘Hili ndilo Bwana Mwenyezi asemalo: Ikiwa mkuu atawalaye atatoa zawadi kutoka kwenye urithi wake na kumpa mmoja wa wanawe, hiyo zawadi itakuwa pia kwa wazao wake, itakuwa mali yao kwa urithi.
17 Jestliže pak dá dar z dědictví svého některému z služebníků svých, také bude jeho až do léta svobodného, kdyžto navrátí se knížeti tomu; však dědictví jeho budou míti synové jeho.
Hata hivyo, kama atatoa zawadi kutoka urithi wake na kumpa mmoja wa watumishi wake, mtumishi anaweza kuiweka mpaka mwaka wa uhuru, kisha itarudishwa kwa mkuu anayetawala. Urithi wake ni wa wanawe peke yao, ni mali yao.
18 Aniž bude bráti kníže z dědictví lidu, z vládařství jejich je vytiskuje; z svého vládařství dědictví dá synům svým, aby nebyl rozptylován lid můj žádný z vládařství svého.
Mkuu anayetawala hana ruhusa kuchukua urithi wowote wa watu na kuwaondoa kwenye mali zao. Mkuu atawalaye atawapa wanawe urithi wao, kutoka kwenye mali zake mwenyewe, ili kwamba pasiwe na mtu wangu yeyote atakayetengwa na urithi wake.’”
19 Potom vedl mne průchodem, kterýž jest po straně brány, k kněžím do komůrek svatých, kteréž patřily na půlnoci, a aj, tu bylo místo po dvou bocích k západu.
Kisha mtu yule akanileta kwa kupitia kwenye ingilio lililokuwa kando ya lango mpaka kwenye vyumba vitakatifu vinavyoelekea kaskazini, ambavyo ni vya makuhani, naye akanionyesha mahali fulani upande wa mwisho wa magharibi.
20 I řekl mi: Toto jest místo, kdež vaří kněží oběti za vinu a za hřích, kdež smaží oběti suché, aby nevynášeli do síně zevnitřní ku posvěcování lidu.
Akaniambia, “Mahali hapa ndipo makuhani watakapotokosea sadaka ya hatia na sadaka ya dhambi na kuoka sadaka ya nafaka, kuepuka kuzileta katika ukumbi wa nje na kushirikisha utakatifu kwa watu.”
21 Vyvedl mne též do síně zevnitřní, a vodil mne po čtyřech koutech síně, a aj, síň byla v každém rohu té síně.
Baada ya hapo akanileta kwenye ukumbi wa nje na kunizungusha kwenye pembe zake nne, nami nikaona katika kila pembe ya huo ukumbi kulikuwa na ukumbi mwingine.
22 Ve čtyřech úhlech té síně byly síně s komíny, čtyřidcíti loket zdélí a třidcíti zšíří; míra jednostejná těch čtyř síní nárožních.
Katika pembe nne za huo ukumbi wa nje kulikuwa na kumbi nyingine, zenye urefu wa dhiraa arobaini na upana wake dhiraa thelathini, ambapo hizo kumbi kwenye hizo pembe nne zilikuwa na vipimo vilivyo sawa.
23 A v těch čtyřech byly kuchyňky vůkol, též ohniště zdělána v těch kuchyňkách vůkol.
Mzunguko wa ndani wa hizo kumbi nne ulikuwa na ukingo wa jiwe, zikiwa na sehemu zilizojengwa kwa ajili ya moto kuzunguka chini ya huo ukingo.
24 I řekl mi: Ta jsou místa těch, kteříž vaří, kdežto vaří služebníci domu oběti lidu.
Akaniambia, “Hizi ndizo sehemu za kupikia ambazo wale wanaohudumu kwenye Hekalu watatokosea dhabihu za watu.”