< Jevrejima 2 >
1 Zato treba da mi svesrdnije prianjamo uz ono što čusmo da ne bismo promašili.
Kwa hiyo ni lazima tuweke kipaumbele zaidi kwa yale tuliyosikia, ili kwamba tusije tukatengwa mbali nayo.
2 Jer ako je riječ po anđelima izrečena bila čvrsta te je svaki prijestup i neposluh primio pravednu plaću,
Kwa maana ikiwa ujumbe uliozungumzwa na malaika ni halali, na kila kosa na uasi hupokea adhabu tu,
3 kako li ćemo mi umaći ako zanemarimo toliko spasenje? Spasenje koje je počeo propovijedati Gospodin, koje su nam potvrdili slušatelji,
tutapataje kuepuka kama tusipojali wokovu huu mkuu? —wokuvu ambao kwanza ulitangazwa na Bwana na kuthibitishwa kwetu na wale waliousikia.
4 a suposvjedočio Bog znamenjima i čudesima, najrazličitijim silnim djelima i darivanjima Duha Svetoga po svojoj volji.
Mungu pia aliuthibitisha kwa ishara, maajabu, na kwa matendo makuu mbalimbali, na kwa zawadi za Roho Mtakatifu alizozigawa kulingana na mapenzi yake mwenyewe.
5 Nije doista anđelima podložio budući svijet o kojem govorimo.
Mungu hakuuweka ulimwengu ujao, ambao tunaongelea habari zake, chini ya malaika.
6 Netko negdje posvjedoči: Što je čovjek da ga se spominješ, sin čovječji te ga pohađaš.
Badala yake, mtu fulani ameshuhudia mahali fulani akisema, “Mtu ni nani, hata uweze kumkumbuka? Au mwana wa mtu, hata umtunze?
7 Ti ga tek za malo učini manjim od anđela, slavom i časti njega ovjenča,
mtu kuwa mdogo kuliko malaika; umemvika taji ya utukufu na heshima. (Zingatia: Katika nakala halisi za kwanza, mstari huu haupo. “Na umemuweka juu ya kazi ya mikono yako.)
8 njemu pod noge sve podloži. Kad mu, doista, sve podloži, ništa ne ostavi što mu ne bi bilo podloženo. Sad još ne vidimo da mu je sve podloženo,
Umeweka kila kitu chini ya miguu yake.” Kwa hiyo Mungu ameweka kila kitu chini ya mtu. Hakuacha kitu chochote ambacho hakiko chini yake. Lakini sasa hivi hatuoni bado kila kitu kikiwa chini yake.
9 ali Njega, za malo manjeg od anđela, Isusa, vidimo zbog pretrpljene smrti slavom i časti ovjenčana da milošću Božjom bude svakome na korist što je on smrt okusio.
Hata hivyo, tunaona ambaye alikuwa amefanywa kwa muda, chini kuliko malaika—Yesu, ambaye, kwa sababu ya mateso yake na kifo chake, amevikwa taji ya utukufu na heshima. Hivyo sasa kwa neema ya Mungu, Yesu ameonja kifo kwa ajili ya kila mtu.
10 Dolikovalo je doista da Onaj radi kojega je sve i po kojemu je sve - kako bi mnoge sinove priveo k slavi - po patnjama do savršenstva dovede Početnika njihova spasenja.
Ilikuwa sahihi kwamba Mungu, kwa sababu kila kitu kipo kwa ajili yake na kupitia yeye, alipaswa kuwaleta watoto wengi katika utukufu, na kwamba alipaswa kumfanya kiongozi katika wokovu wao kuwa mkamilifu kupitia mateso yake.
11 Ta i Posvetitelj i posvećeni - svi su od jednoga! Zato se on i ne stidi zvati ih braćom,
Kwa maana wote wawili yule anayeweka wakfu na wale ambao wanawekwa wakfu, wote wanatoka kwenye asili moja, Mungu. Kwa sababu hii yule anayewaweka wakfu kwa Mungu haoni aibu kuwaita ndugu.
12 kad veli: Braći ću svojoj naviještat ime tvoje, hvalit ću te usred zbora.
Anasema, “Nitatangaza jina lako kwa ndugu zangu, nitaimba kuhusu wewe kutoka ndani ya kusanyiko.”
13 I još: Ja ću se u njega uzdati, i još: Evo, ja i djeca koju mi Bog dade.
Tena asema, “Nitaamini katika yeye.” Na tena, “Tazama, hapa nipo na watoto ambao Mungu amenipa.”
14 Pa budući da djeca imaju zajedničku krv i meso, i sam on tako postade u tome sudionikom da smrću obeskrijepi onoga koji imaše moć smrti, to jest đavla,
Kwa hiyo, kwa kuwa watoto wa Mungu wote hushiriki mwili na damu, kadhalika Yesu alishiriki vitu vilevile, ili kwamba kupitia kifo apate kumdhohofisha yule ambaye ana mamlaka juu ya mauti, ambaye ni ibilisi.
15 pa oslobodi one koji - od straha pred smrću - kroza sav život bijahu podložni ropstvu.
Hii ilikuwa hivyo ili awaweke huru wale wote ambao kupitia hofu ya kifo waliishi maisha yao yote katika utumwa.
16 Ta ne zauzima se dašto za anđele, nego se zauzima za potomstvo Abrahamovo.
Kwa hakika siyo malaika anaowasaidia. Badala yake, anawasaidia wazao wa Abraham.
17 Stoga je trebalo da u svemu postane braći sličan, da milosrdan bude i ovjerovljen Veliki svećenik u odnosu prema Bogu kako bi okajavao grijehe naroda.
Kwa hiyo, ilikuwa lazima yeye awe kama ndugu zake katika njia zote, ili aweze kuwa kuhani mkuu mwenye huruma na mwaminifu kwa vitu vya Mungu, na ili kwamba awe na uwezo wa kutoa msamaha kwa dhambi za watu.
18 Doista, u čemu je iskušan trpio, može iskušavanima pomoći.
Kwa sababu Yesu mwenyewe ameteseka, na kujaribiwa, ana uwezo wa kuwasaidia wale wanaojaribiwa.