< Jevrejima 13 >
1 Bratoljublje neka je trajno!
Endeleeni kupendana kidugu.
2 Gostoljublja ne zaboravljajte: njime neki, i ne znajući, ugostiše anđele!
Msisahau kuwakaribisha wageni; maana kwa kufanya hivyo watu wengine walipata kuwakaribisha malaika bila kujua.
3 Sjećajte se uznika kao suuznici; zlostavljanih - ta i sami ste u tijelu!
Wakumbukeni wale waliofungwa kana kwamba mmefungwa pamoja nao. Wakumbukeni wale wanaoteseka kana kwamba nanyi mnateseka kama wao.
4 Ženidba neka bude u časti u sviju i postelja neokaljana! Jer bludnicima će i preljubnicima suditi Bog.
Ndoa inapaswa kuheshimiwa na watu wote, na haki zake zitekelezwe kwa uaminifu. Mungu atawahukumu waasherati na wazinzi.
5 U življenju ne budite srebroljupci, zadovoljni onim što imate! Ta on je rekao: Ne, neću te zapustiti i neću te ostaviti.
Msiwe watu wa kupenda fedha; toshekeni na vile vitu mlivyo navyo. Mungu mwenyewe amesema: “Sitakuacha kamwe, wala sitakutupa.”
6 Zato možemo pouzdano reći: Gospodin mi je pomoćnik, ja ne strahujem: što mi tko može?
Ndiyo maana tunathubutu kusema: “Bwana ndiye msaada wangu, sitaogopa. Binadamu atanifanya nini?”
7 Spominjite se svojih glavara koji su vam nevješćivali riječ Božju: promatrajući kraj njihova života, nasljedujte njihovu vjeru.
wakumbukeni viongozi wenu waliowatangazieni ujumbe wa Mungu. Fikirieni juu ya mwenendo wao, mkaige imani yao.
8 Isus Krist jučer i danas isti je - i uvijeke. (aiōn )
Yesu Kristo ni yuleyule, jana, leo na milele. (aiōn )
9 Ne dajte se zanijeti različitim tuđim naucima! Jer bolje je srce utvrđivati milošću nego jelima, koja nisu koristila onima što su ih obdržavali.
Msipeperushwe huku na huku kwa mafundisho tofauti ya kigeni. Neema ya Mungu ndiyo inayoimarisha roho zetu na wala si masharti juu ya chakula; masharti hayo hayakumsaidia kamwe mtu yeyote aliyeyafuata.
10 Imamo žrtvenik s kojega nemaju pravo jesti služitelji Šatora.
Sisi tunayo madhabahu ambayo wale wanaotumikia bado katika hema la Wayahudi, hawana haki ya kula vitu vyake.
11 Jer tijela životinja, kojih krv veliki svećenik unosi za grijeh u Svetinju, spaljuju se izvan tabora.
Kuhani Mkuu wa Kiyahudi huleta damu ya wanyama katika Mahali Patakatifu na kuitoa dhabihu kwa ajili ya dhambi; lakini nyama za hao wanyama huteketezwa nje ya kambi.
12 Zato i Isus, da bi vlastitom krvlju posvetio narod, trpio je izvan vrata.
Ndiyo maana Yesu pia, kusudi apate kuwatakasa watu kwa damu yake mwenyewe, aliteswa na kufa nje ya mji.
13 Stoga iziđimo k njemu izvan tabora noseći njegovu muku
Basi, tumwendee huko nje ya kambi tukajitwike laana yake.
14 jer nemamo ovdje trajna grada, nego onaj budući tražimo.
Maana hapa duniani hatuna mji wa kudumu; lakini tunautafuta ule unaokuja.
15 Po njemu dakle neprestano prinosimo Bogu žrtvu hvalbenu, to jest plod usana što ispovijedaju ime njegovo.
Basi, kwa njia ya Yesu, tumtolee Mungu dhabihu ya sifa daima, yaani sifa zinazotolewa na midomo inayoliungama jina lake.
16 Dobrotvornosti i zajedništva ne zaboravljajte jer takve su žrtve mile Bogu!
Msisahau kutenda mema na kusaidiana, maana hizi ndizo dhabihu zinazompendeza Mungu.
17 Poslušni budite svojim glavarima i podložni jer oni bdiju nad vašim dušama kao oni koji će polagati račun; neka to čine s radošću, a ne uzdišući jer vam to ne bi bilo korisno.
Watiini viongozi wenu na kushika amri zao; wao huchunga roho zenu usiku na mchana, na watatoa ripoti ya utumishi wao mbele ya Mungu. Kama mkiwatii watafanya kazi zao kwa furaha, la sivyo, watazifanya kwa huzuni, na hiyo haitakuwa na faida kwenu.
18 Molite za nas! Uvjereni smo doista da imamo dobru savjest i u svemu se želimo dobro ponašati.
Tuombeeni na sisi. Tuna hakika kwamba tunayo dhamiri safi, maana twataka kufanya lililo sawa daima.
19 Usrdnije vas pak molim: učinite to kako bih vam se što brže vratio.
Nawasihi sana mniombee ili Mungu anirudishe kwenu upesi iwezekanavyo.
20 A Bog mira, koji po krvi vječnoga Saveza od mrtvih izvede velikoga Pastira ovaca, Gospodina našega Isusa, (aiōnios )
Mungu amemfufua Bwana wetu Yesu Kristo ambaye ni Mchungaji Mkuu wa kondoo kwa sababu ya kumwaga damu yake iliyothibitisha agano la milele. (aiōnios )
21 osposobio vas za svako dobro djelo da vršite volju njegovu, činio u nama što je njemu milo, po Isusu Kristu, komu slava u vijeke vjekova. Amen. (aiōn )
Mungu wa amani awakamilishe katika kila tendo jema ili mtekeleze mapenzi yake; yeye na afanye ndani yetu kwa njia ya Kristo yale yanayompendeza mwenyewe. Utukufu uwe kwake, milele na milele! Amina. (aiōn )
22 Molim vas, braćo, podnesite ovu riječ ohrabrenja: ta samo vam ukratko napisah!
Basi, ndugu, nawasihi mpokee kwa utulivu ujumbe huu wa kuwatieni moyo. Hii ni barua fupi tu ambayo nimewaandikieni.
23 Znajte: naš je brat Timotej oslobođen. Ako uskoro stigne, s njime ću vas pohoditi.
Napenda kuwajulisheni kwamba ndugu yetu Timotheo amekwisha funguliwa gerezani. Kama akifika hapa mapema, nitakuja naye nitakapokuja kwenu.
24 Pozdravite sve svoje glavare i sve svete! Pozdravljaju vas ovi iz Italije.
Wasalimieni viongozi wenu wote pamoja na watu wa Mungu! Ndugu wa Italia wanawasalimuni.
Tunawatakieni nyote neema ya Mungu.