< Djela apostolska 10 >
1 U Cezareji bijaše neki čovjek imenom Kornelije, satnik takozvane italske čete,
Katika mji wa Kaisaria palikuwa na mtu jina lake Kornelio, ambaye alikuwa jemadari wa kile kilichojulikana kama kikosi cha Kiitalia.
2 pobožan i bogobojazan sa svim svojim domom. Dijelio je mnoge milostinje narodu i bez prestanka se molio Bogu.
Yeye alikuwa mcha Mungu pamoja na wote wa nyumbani mwake. Aliwapa watu sadaka nyingi na kumwomba Mungu daima.
3 U viđenju negdje oko devete ure dana ugleda on jasno anđela Božjega gdje dolazi k njemu i veli mu: “Kornelije!”
Siku moja alasiri, yapata saa tisa, aliona maono waziwazi, malaika wa Mungu akimjia na kumwambia, “Kornelio!”
4 Zagleda se u nj pa mu prestrašen reče: “Što je, Gospodine?” A on njemu: “Molitve su tvoje i milostinje uzišle kao žrtva podsjetnica pred Boga.
Kornelio akamkazia macho kwa hofu akasema, “Kuna nini, Bwana?” Malaika akamwambia, “Sala zako na sadaka zako kwa maskini zimefika juu na kuwa ukumbusho mbele za Mungu.
5 Zato sada pošalji ljude u Jopu i dozovi Šimuna koji se zove Petar.
Sasa tuma watu waende Yafa wakamwite mtu mmoja jina lake Simoni aitwaye Petro.
6 On je gost u nekog Šimuna kožara čija je kuća uz more.”
Yeye anaishi na Simoni mtengenezaji ngozi ambaye nyumba yake iko kando ya bahari.”
7 Čim ode anđeo koji mu je govorio, pozove on dvojicu slugu i jednoga pobožna, privržena vojnika,
Yule malaika aliyekuwa akizungumza naye alipoondoka, Kornelio akawaita watumishi wake wawili pamoja na askari mmoja mcha Mungu aliyekuwa miongoni mwa wale waliomtumikia.
8 sve im ispripovjedi i posla ih u Jopu.
Akawaambia mambo yote yaliyotukia, kisha akawatuma waende Yafa.
9 Sutradan, dok su oni putovali i približavali se gradu, oko šeste ure uziđe Petar na krov moliti.
Siku ya pili yake, walipokuwa wameukaribia mji, wakati wa adhuhuri, Petro alipanda juu ya nyumba kuomba.
10 Ogladnje i zaželje se jela. Dok mu pripremahu, pade on u zanos.
Alipokuwa akiomba akahisi njaa, akatamani kupata chakula. Lakini wakati walikuwa wakiandaa chakula, akalala usingizi mzito sana.
11 Gleda on nebo rastvoreno i posudu neku poput velika platna: uleknuta s četiri okrajka, silazi na zemlju.
Akaona mbingu zimefunguka na kitu kama nguo kubwa kikishushwa duniani kwa ncha zake nne.
12 U njoj bijahu svakovrsni četveronošci, gmazovi zemaljski i ptice nebeske.
Ndani yake walikuwepo aina zote za wanyama wenye miguu minne, nao watambaao nchini, na ndege wa angani.
13 I glas će mu neki: “Ustaj, Petre! Kolji i jedi!”
Ndipo sauti ikamwambia “Petro, ondoka, uchinje na ule.”
14 Petar odvrati: “Nipošto, Gospodine! Ta nikad još ne okusih ništa okaljano i nečisto”.
Petro akajibu, “La hasha Bwana! Sijawahi kamwe kula kitu chochote kilicho najisi.”
15 A glas će mu opet, po drugi put: “Što Bog očisti, ti ne zovi okaljanim!”
Ile sauti ikasema naye mara ya pili, “Usikiite najisi kitu chochote Mungu alichokitakasa.”
16 To se ponovi do triput, a onda je posuda ponesena na nebo.
Jambo hili lilitokea mara tatu na ghafula ile nguo ikarudishwa mbinguni.
17 Dok se Petar dvoumio što bi imalo značiti viđenje koje vidje, eto ljudi koje je poslao Kornelije: pošto se raspitaše za Šimunovu kuću, pojave se na vratima,
Wakati Petro akiwa bado anajiuliza kuhusu maana ya maono haya, wale watu waliokuwa wametumwa na Kornelio wakaipata nyumba ya Simoni mtengenezaji wa ngozi wakawa wamesimama mbele ya lango.
18 zovnu te upitaju je li ondje ugošćen neki Šimun, nazvan Petar.
Wakabisha hodi na kuuliza kama Simoni aliyeitwa Petro alikuwa anaishi hapo.
19 Dok je Petar sveudilj razmišljao o viđenju, reče mu Duh: “Evo, neka te trojica traže.
Wakati Petro akiwa anafikiria juu ya yale maono, Roho Mtakatifu akamwambia, “Simoni, wako watu watatu wanaokutafuta.
20 De ustani, siđi i pođi s njima ne skanjujući se jer ja sam ih poslao.”
Inuka na ushuke, usisite kwenda nao kwa kuwa mimi nimewatuma.”
21 Petar siđe k ljudima i reče: “Evo me! Ja sam onaj kojega tražite! Zbog čega ste došli?”
Petro akashuka na kuwaambia wale watu waliokuwa wametumwa kutoka kwa Kornelio, “Mimi ndiye mnayenitafuta. Mmekuja kwa sababu gani?”
22 Oni odgovore: “Satnik Kornelije, muž pravedan i bogobojazan, za kojega svjedoči sav narod židovski, primi od svetog anđela naputak da te dozove u dom svoj i čuje od tebe riječi.”
Wale watu wakamjibu, “Tumetumwa na Kornelio yule jemadari. Yeye ni mtu mwema anayemcha Mungu, na anaheshimiwa na Wayahudi wote. Yeye ameagizwa na malaika mtakatifu akukaribishe nyumbani kwake, ili asikilize maneno utakayomwambia.”
23 Tada ih Petar pozva unutra i ugosti. Sutradan usta i krenu s njima; pratila ga neka braća iz Jope.
Basi Petro akawakaribisha wakafuatana naye ndani, akawapa pa kulala. Kesho yake akaondoka pamoja nao, na baadhi ya ndugu kutoka Yafa wakafuatana naye.
24 Drugi dan stiže u Cezareju. Kornelije ih je čekao sazvavši rodbinu i prisne prijatelje.
Siku iliyofuata wakawasili Kaisaria. Kornelio alikuwa akiwangoja pamoja na jamaa yake na marafiki zake wa karibu.
25 Kad je Petar ulazio, pohrli mu Kornelije u susret, padne mu k nogama i pokloni se.
Petro alipokuwa akiingia ndani, Kornelio alikuja kumlaki, akaanguka miguuni pake kwa heshima.
26 Petar ga pridigne govoreći: “Ustani! I ja sam čovjek.”
Lakini Petro akamwinua akamwambia, “Simama, mimi ni mwanadamu tu.”
27 I razgovarajući s njime, uđe i nađe sabrane mnoge
Petro alipokuwa akizungumza naye akaingia ndani na kukuta watu wengi wamekusanyika.
28 te im reče: “Vi znate kako je Židovu zabranjeno družiti se sa strancem ili k njemu ulaziti, ali meni Bog pokaza da nikoga ne zovem okaljanim ili nečistim.
Akawaambia, “Mnajua kabisa kwamba ni kinyume cha sheria yetu Myahudi kuchangamana na mtu wa Mataifa au kumtembelea. Lakini Mungu amenionyesha kwamba nisimwite mtu yeyote kuwa najisi au asiye safi.
29 Stoga, pozvan, i dođoh bez pogovora. Da čujemo dakle zbog čega me pozvaste!”
Ndiyo sababu ulipotuma niitwe nilikuja bila kupinga lolote. Basi sasa naomba unieleze kwa nini umeniita?”
30 Kornelije reče: “Prije četiri dana baš u ovo doba, o devetoj uri, molio sam se u kući kad gle: čovjek neki u sjajnoj odjeći stane preda me
Kornelio akajibu, “Siku nne zilizopita, nilikuwa nyumbani nikisali saa kama hii, saa tisa alasiri. Ghafula mtu aliyevaa nguo zilizongʼaa akasimama mbele yangu,
31 i reče: 'Kornelije, uslišana ti je molitva i milostinje su tvoje spomenute pred Bogom!
akasema, ‘Kornelio, maombi yako yamesikiwa na sadaka zako kwa maskini zimekumbukwa mbele za Mungu.
32 Pošalji dakle u Jopu i dozovi Šimuna koji se zove Petar. On je gost u kući Šimuna kožara uz more.'
Basi tuma watu waende Yafa wakaulize mtu mmoja Simoni aitwaye Petro, yeye ni mgeni katika nyumba ya Simoni mtengenezaji ngozi, ambaye nyumba yake iko kando ya bahari.’
33 Odmah sam dakle poslao k tebi, a ti si dobro učinio što si došao. Evo nas dakle sviju pred Bogom da čujemo sve što ti zapovjedi Gospodin!”
Nilituma watu kwako mara moja, nawe umefanya vyema kuja. Basi sasa sisi sote tuko hapa mbele za Mungu kuyasikiliza yote ambayo Bwana amekuamuru kutuambia.”
34 Petar tada prozbori i reče: “Sad uistinu shvaćam da Bog nije pristran,
Ndipo Petro akafungua kinywa chake akasema, “Mungu hana upendeleo,
35 nego - u svakom je narodu njemu mio onaj koji ga se boji i čini pravdu.
Lakini katika kila taifa, kila mtu amchaye na kutenda yaliyo haki hukubaliwa naye.
36 Riječ posla sinovima Izraelovim navješćujući im evanđelje: mir po Isusu Kristu; on je Gospodar sviju.
Ninyi mnajua ule ujumbe uliotumwa kwa Israeli, ukitangaza habari njema za amani kwa Yesu Kristo. Yeye ni Bwana wa wote.
37 Vi znate što se događalo po svoj Judeji, počevši od Galileje, nakon krštenja koje je propovijedao Ivan:
Mnajua yale yaliyotukia katika Uyahudi wote kuanzia Galilaya baada ya mahubiri ya Yohana Mbatizaji:
38 kako Isusa iz Nazareta Bog pomaza Duhom Svetim i snagom, njega koji je, jer Bog bijaše s njime, prošao zemljom čineći dobro i ozdravljajući sve kojima bijaše ovladao đavao.”
Jinsi Mungu alivyomtia Yesu wa Nazareti mafuta katika Roho Mtakatifu na jinsi alivyokwenda huku na huko akitenda mema na kuponya wote waliokuwa wameonewa na nguvu za ibilisi, kwa sababu Mungu alikuwa pamoja naye.
39 “Mi smo svjedoci svega što on učini u zemlji judejskoj i Jeruzalemu. I njega smakoše, objesivši ga na drvo!
“Sisi ni mashahidi wa mambo yote aliyoyafanya katika Uyahudi na Yerusalemu. Wakamuua kwa kumtundika msalabani.
40 Bog ga uskrisi treći dan i dade mu da se očituje -
Lakini Mungu alimfufua kutoka kwa wafu siku ya tatu na akamwezesha kuonekana na watu.
41 ne svemu narodu, nego svjedocima od Boga predodređenima - nama koji smo s njime zajedno jeli i pili pošto uskrsnu od mrtvih.”
Hakuonekana kwa watu wote, lakini kwetu sisi tuliochaguliwa na Mungu kuwa mashahidi, ambao tulikula na kunywa naye baada ya kufufuka kwake kutoka kwa wafu.
42 “On nam i naloži propovijedati narodu i svjedočiti: Ovo je onaj kojega Bog postavi sucem živih i mrtvih!”
Naye alituamuru kuhubiri kwa watu wote na kushuhudia kwamba ndiye alitiwa mafuta na Mungu kuwa hakimu wa walio hai na wafu.
43 “Za nj svjedoče svi proroci: da tko god u nj vjeruje, po imenu njegovu prima oproštenje grijeha.”
Manabii wote walishuhudia juu yake kwamba kila mtu amwaminiye hupokea msamaha wa dhambi katika Jina lake.”
44 Dok je Petar još govorio te riječi, siđe Duh Sveti na sve koji su slušali tu besjedu.
Wakati Petro alikuwa akisema maneno haya, Roho Mtakatifu aliwashukia wote waliokuwa wakisikiliza ule ujumbe.
45 A vjernici iz obrezanja, koji dođoše zajedno s Petrom, začudiše se što se i na pogane izlio dar Duha Svetoga.
Wale wa tohara walioamini waliokuja na Petro walishangaa kwa kuona kuwa kipawa cha Roho Mtakatifu kimemwagwa juu ya watu wa Mataifa.
46 Jer čuli su ih govoriti drugim jezicima i veličati Boga. Tada Petar reče:
Kwa kuwa waliwasikia wakinena kwa lugha mpya na kumwadhimisha Mungu. Ndipo Petro akasema,
47 “Može li tko uskratiti vodu da se ne krste ovi koji su primili Duha Svetoga kao i mi?”
“Je, kuna mtu yeyote anayeweza kuzuia watu hawa wasibatizwe kwa maji? Wamempokea Roho Mtakatifu kama sisi tulivyompokea.”
48 I zapovjedi da se krste u ime Isusa Krista. Tada ga zamole da ostane ondje nekoliko dana.
Kwa hiyo akaamuru wabatizwe kwa jina la Yesu Kristo. Wakamsihi Petro akae nao kwa siku chache.