< 1 Ljetopisa 28 >

1 David sakupi u Jeruzalem sve izraelske knezove, plemenske knezove i poglavare od redova koji su služili kralja, tisućnike, stotnike i nadstojnike nad svim imanjem i blagom kraljevim i blagom njegovih sinova, zajedno s dvoranima i junacima i svim hrabrim vojnicima.
Daudi akakusanya waamuzi wote wa Israeli Yerusalemu: waamuzi wa makabila, maafisa wa vitengo walio mtumikia mfalme katika kazi walizo pangiwa, wakuu wa maelfu na mamia, wasimamizi wa mali zote za mfalme na mwanae, na maafisa na wanaume wa mapambano, ukijumuisha wale wenye ujuzi sana.
2 Ustavši na noge, kralj David reče: “Čujte me, moja braćo i moj narode! Ja sam bio namislio u svom srcu da sagradim dom gdje bi počivao Kovčeg saveza Jahvina i da bude podnožje nogama našega Boga te sam pripravio što treba za gradnju.
Daudi mfalme akainuka kwa miguu yake na kusema, “Sikilizeni mimi, kaka zangu na watu wangu. Ilikuwa dhumuni langu kujenga hekalu kwa ajili ya sanduku la agano la Yahweh; stuli ya miguu kwa ajili ya Mungu wetu, na nimefanya maandalizi kuijenga.
3 Ali mi je Bog rekao: 'Nećeš ti sagraditi Doma mome imenu jer si ratnik i prolijevao si krv.'
Lakini Mungu akaniambia, 'Hautajenga hekalu kwa ajili ya jina la langu, kwasababu wewe ni mwanaume wa vita na umemwaga damu.'
4 Jahve, Izraelov Bog, izabrao je mene od sveg moga roda da budem kralj nad Izraelom zauvijek; jer je Judu izabrao za kneza, a iz Judina doma dom moga oca; između sinova moga oca bilo mu je drago da mene postavi kraljem nad svim Izraelom.
Bado Yahweh, Mungu wa Israeli, alinichagua kutoka katika familia ya baba yangu kuwa mfalme wa Israeli milele. Amechagua kabila la Yuda kama kiongozi. Katika kabila la Yuda, na nyumba ya baba yangu, kutoka kwa wana wa baba yangu, amenichagua kuwa mfalme wa Israeli.
5 Tako je između mojih sinova, jer mi je mnogo sinova dao Jahve, izabrao moga sina Salomona da sjedi na prijestolju Jahvina kraljevstva nad Izraelom.
Kutoka kwa wana wengi ambao Yahweh amenipa, amemchagua Sulemani, mwanangu, kuketi katika kiti cha enzi cha ufalme wa Yahweh, juu ya Israeli.
6 I rekao mi je: 'Tvoj sin Salomon sagradit će meni Dom i moja predvorja; jer sam njega izabrao sebi za sina i ja ću mu biti otac.
Aliniambia, 'Sulemani mwanae atanijengea nyumba yangu na nyuani mwangu, kwa kuwa nimemchagua kuwa mwana wangu, nami nitakuwa baba yake.
7 Utvrdit ću njegovo kraljevstvo zauvijek ako bude postojano vršio moje zapovijedi i moje zakone kao danas.'
Nitaimarisha ufalme wake, akidumu kutii sheria na amri zangu, kama ulivyo siku ya leo.'
8 Sada, dakle, pred očima sveg Izraela, Jahvina zbora, i pred svojim Bogom, koji nas sluša, velim: držite i tražite sve zapovijedi Jahve, svoga Boga, da biste zadržali u posjedu ovu dobru zemlju i ostavili je u baštinu svojim sinovima nakon sebe dovijeka.
Kisha sasa, katika macho ya Waisraeli wote, ili kusanyiko la yahweh, na katika uwepo wa Mungu wetu, nyinyi nyote lazima mshike na kufanya amri zote za Yahweh Mungu wenu. Fanyeni hivi ili mmiliki nchi nzuri na kuacha urithi wa watoto wenu baada yenu milele.
9 A ti, sine moj Salomone, poznaj Boga, svoga oca, i služi mu čitavim srcem i spremnom dušom, jer Jahve ispituje sva srca i zna sve misli i namjere; ako ga budeš tražio, dat će ti se da ga nađeš; ako li ga ostaviš, odbacit će te zauvijek.
Kwako wewe, Sulemani mwanangu, mtii Mungu wa baba yako, mtumikie kwa moyo wako wote na roho ya utayari. Fanya hivi kwasababu yahweh anachunguza mioyo yote na kufahamu amasa ya kila wazo la mtu. Ukimtafuta, ataonekana kwako, lakini ukimtelekeza, atakukataa milele.
10 Uvidi sada da te Jahve izabrao da gradiš Dom za Svetište, budi junak i radi!”
Elewa kuwa Yahweh amekuchagua kujenga hekalu ili kama sehemu yake takatifu. Kuwa imara na ufanye.”
11 Tada David predade sinu Salomonu uzorak trijema, njegovih kuća, riznica, gornjih soba, ćelija i doma Pomirilišta;
Kisha Daudi akamkabidhi Sulemani mwanae mipango ya baraza la hekalu, jengo la hekalu, vyumba vya hifadhi, vyumba vya juu, vyumba vya ndani, na chumba chenye mfuniko wa maombezi.
12 uzorak svega što bijaše smislio u duhu za predvorja Jahvina Doma, za sve sobe unaokolo, za riznicu Doma Božjega, za riznicu posvećenih stvari,
Alimpatia mipango aliyo chora ya nyuani kwa ajili ya nyumba ya Yahweh, vyumba vyote vilivyo zunguka, vyumba vya hifadhi katika nyumba ya Mungu, na hazina za vitu vya Yahweh.
13 za svećeničke i levitske redove, za svaki posao u službi oko Doma Jahvina:
Alimpatia masharti kwa vitengo vya makuhani na Walawi, kwa majukumu walio pangiwa katika nyumba ya Yahweh, na kwa vyombo vyote vinavyo tumika katika nyumba ya Yahweh.
14 zlato u šipkama, zlato potrebno za sve zlatno posuđe ove ili one službe; srebro u šipkama potrebno za sve srebrno posuđe, za sve posuđe ove ili one službe;
Alimpa uzito wote wa vifaa vya dhahabu kwa kila huduma na vifaa vyote vya fedha, na vitu vyote kwa kila namna ya huduma.
15 šipke za zlatne svijećnjake sa zlatnim svjetiljkama, prema težini svakoga svijećnjaka i njegovih svjetiljaka, i za srebrne svijećnjake prema težini svakoga svijećnjaka i njegovih svjetiljaka i prema namjeni svakog svijećnjaka;
Haya maelekezo yalitolewa kwa uzito, ukijumuisha maelekezo yote ya vinara vya taa vya dhahabu na taa za dhahabu, maelekezo kwa uzito kwa kila vinara vya taa, kwa vinara vya taa vya fedha, na maelekezo kwa matumizi sahihi ya vinara vya taa vyote.
16 zlato u šipkama za stolove na kojima će stajati prineseni hljebovi, za svaki stol; srebro za srebrne stolove,
Alitoa uzito wa dhahabu kwa meza za mkate wa uwepo, kwa kila meza, na uzito wa fedha kwa meza za fedha.
17 za viljuške i kotliće, za čaše od čista zlata, za zlatne pehare, zlato u šipkama za svaki pehar; za srebrne pehare, srebro u šipkama za svaki pehar,
Alitoa uzito wa dhahabu safi kwa uma za nyama, bakuli, na vikombe. Alitoa uzito kwa kila bakuli ya dhahabu, na uzito kwa kila bakuli ya fedha.
18 za kadioni žrtvenik žeženoga zlata u šipkama; za uzorak od kola sa zlatnim kerubinima koji će raširenim krilima zaklanjati Jahvin Kovčeg.
Alitoa uzito wa dhahabu ya kutakasika kwa madhabahu ya uvumba, na kwa dhahabu kwa ajili ya mchoro wa makerubi waliye tanda mabawa yao na kufunika sanduku la agano la Yahweh.
19 Sve to u skladu s onim što Jahve napisa vlastitom rukom da bi razjasnio cijelo djelo za koje on pribavi uzorak.
Daudi akasema, “Nimeeka haya katika maandishi kama Yahweh alivyo ni elekeza na kunipa kuelewa kuhusu mchoro.”
20 Tada David reče svome sinu Salomonu: “Budi junak, hrabar, i radi! Ne boj se i ne plaši se, jer će Jahve, Bog, moj Bog, biti s tobom! Neće te napustiti niti te ostaviti dok ne svršiš sav posao za službu oko Jahvina Doma.
Daudi akasema kwa Sulemani mwanae, “Kuwa hodari na mjasiri. Fanya kazi. Usiogope au kuwa na wasiwasi, kwa kuwa Yahweh Mungu, Mungu wangu, yupo nawe. Hatakuacha wala kukutelekeza mpaka kazi ya huduma ya hekalu la Yahweh imekamilika.
21 Evo svećeničkih i levitskih redova za svaku službu u Božjem Domu; imaš uza se za svaki posao svakovrsnih ljudi, spremnih i vještih svakoj službi, knezovi i sav narod pod tvojim su zapovjedništvom.”
Ona, hivi ni vitengo vya makuhani na Walawi kwa huduma katika hekalu la Mungu. Watakuwa nawe, pamoja na wanaume walio tayari na wenye ujuzi, kukusaidia katika kazi na kutenda huduma. Waamuzi na watu wote wako tayari kufuata amri zako.”

< 1 Ljetopisa 28 >