< 啟示錄 17 >
1 拿着七碗的七位天使中,有一位前來對我說:「你到這裏來,我將坐在眾水上的大淫婦所要受的刑罰指給你看。
Mmoja wa malaika saba aliyekuwa na vitasa saba alikuja na kuniambia, “Njoo, nitakuonesha hukumu ya kahaba mkuu akaaye juu ya maji mengi,
2 地上的君王與她行淫,住在地上的人喝醉了她淫亂的酒。」
ambaye wafalme wa nchi wamefanya mambo ya uzinzi naye na juu ya mvinyo wa uzinzi wake wakaao duniani wameleweshwa.”
3 我被聖靈感動,天使帶我到曠野去,我就看見一個女人騎在朱紅色的獸上;那獸有七頭十角,遍體有褻瀆的名號。
Malaika akanichukua katika Roho mpaka nyikani, na nilimwona mwanamke amekaa juu ya mnyama mwekundu aliyejaa majina ya matukano. Mnyama alikuwa na vichwa saba na pembe kumi.
4 那女人穿着紫色和朱紅色的衣服,用金子、寶石、珍珠為妝飾;手拿金杯,杯中盛滿了可憎之物,就是她淫亂的污穢。
Mwanamke alivikwa nguo ya zambarau na nyekundu na amepambwa kwa dhahabu, mawe ya thamani, na lulu. Alikuwa ameshikilia mkononi mwake kikombe cha dhahabu kilichojaa vitu vya machukizo ya uchafu wa uasherati wake.
5 在她額上有名寫着說:「奧祕哉!大巴比倫,作世上的淫婦和一切可憎之物的母。」
Juu ya paji la uso wake limeandikwa jina la siri: “BABELI MKUU, MAMA WA MAKAHABA NA YA VITU VYA MACHUKIZO YA NCHI.”
6 我又看見那女人喝醉了聖徒的血和為耶穌作見證之人的血。 我看見她,就大大地希奇。
Nikaona ya kuwa mwanamke huyo alikuwa amelewa kwa damu ya waumini na damu ya waliokufa kwa ajili ya Yesu. Wakati nilipomwona, nilikuwa na mshangao mkuu.
7 天使對我說:「你為甚麼希奇呢?我要將這女人和馱着她的那七頭十角獸的奧祕告訴你。
Lakini malaika akaniambia, “Kwa nini unashangaa? Nitakueleza maana ya mwanamke na mnyama amchukuaye (mnyama huyo mwenye vichwa saba na zile pembe kumi).
8 你所看見的獸,先前有,如今沒有,將要從無底坑裏上來,又要歸於沉淪。凡住在地上、名字從創世以來沒有記在生命冊上的,見先前有、如今沒有、以後再有的獸,就必希奇。 (Abyssos )
Mnyama uliyemwona alikuwepo, hayupo tena sasa, lakini yuko tayari kupanda kutoka katika shimo lisilo na mwisho. Kisha ataendelea na uharibifu. Wale wakaao juu ya nchi, wale ambao majina yao hayakuandikwa kwenye kitabu cha uzima tangu kuwekwa misingi ya ulimwengu - watashangaa wamwonapo mnyama aliyekuwepo, kwamba hayupo sasa, lakini yupo karibu kuja. (Abyssos )
9 智慧的心在此可以思想。那七頭就是女人所坐的七座山,
Wito huu ni kwa ajili ya akili zilizo na hekima. Vichwa saba ni milima saba ambapo mwanamke alikaa juu yake.
10 又是七位王;五位已經傾倒了,一位還在,一位還沒有來到;他來的時候,必須暫時存留。
Nayo pia ni wafalme saba. Wafalme watano wameanguka, mmoja yupo, na mwingine hajaja bado; wakati atakapokuja, atakaa kwa muda mfupi tu.
11 那先前有如今沒有的獸,就是第八位;他也和那七位同列,並且歸於沉淪。
Mnyama aliyekuwepo, lakini sasa hayupo, yeye pia ni mfalme wa nane; lakini ni mmoja wa wale wafalme saba, na anaenda kwenye uharibifu.
12 你所看見的那十角就是十王;他們還沒有得國,但他們一時之間要和獸同得權柄,與王一樣。
Zile pembe kumi ulizoziona ni wafalme kumi ambao hawajapokea ufalme, lakini watapokea mamlaka kama wafalme kwa saa moja pamoja na mnyama.
Hawa wana shauri moja, na watampa nguvu zao na mamlaka yule mnyama.
14 他們與羔羊爭戰,羔羊必勝過他們,因為羔羊是萬主之主、萬王之王。同着羔羊的,就是蒙召、被選、有忠心的,也必得勝。」
Watafanya vita baina yao na Mwana kondoo. Lakini Mwana kondoo atawashinda kwa sababu ni Bwana wa mabwana na Mfalme wa wafalme - na katika yeye tuliitwa, tulichaguliwa, waaminifu.”
15 天使又對我說:「你所看見那淫婦坐的眾水,就是多民、多人、多國、多方。
Malaika akaniambia, “Yale maji uliyoyaona, hapo alipoketi yule kahaba ni watu, makutano, mataifa na lugha.
16 你所看見的那十角與獸必恨這淫婦,使她冷落赤身,又要吃她的肉,用火將她燒盡。
Zile pembe kumi ulizoziona - hizo na yule mnyama watamchukia yule kahaba. Nao watamfanya kuwa mpweke na uchi, watamla mwili wake, na watauteketeza kwa moto.
17 因為上帝使諸王同心合意,遵行他的旨意,把自己的國給那獸,直等到上帝的話都應驗了。
Maana Mungu ameweka mioyoni mwao kubeba kusudi lake kwa makubaliano ya kumpa mnyama nguvu zao kumtawala mpaka maneno ya Mungu yatakapotimia.
Yule mwanamke uliyemwona ni mji ule mkubwa utawalao juu ya wafalme wa nchi.”