< 詩篇 96 >
1 你們要向耶和華唱新歌! 全地都要向耶和華歌唱!
Oh, mwimbieni Yahwe wimbo mpya; mwimbieni Yahwe, nchi yote.
2 要向耶和華歌唱,稱頌他的名! 天天傳揚他的救恩!
Mwimbieni Yahwe, tukuzeni jina lake; tangazeni wokovu wake siku hadi siku.
3 在列邦中述說他的榮耀! 在萬民中述說他的奇事!
Tangazeni utukufu wake kati ya mataifa, matendo yake ya ajabu kati ya mataifa.
4 因耶和華為大,當受極大的讚美; 他在萬神之上,當受敬畏。
Maana Yahwe ni mkuu na wakusifiwa sana. Ni wakuhofiwa kuliko miungu mingine.
Maana miungu yote ya mataifa ni sanamu, bali ni Yahwe aliye zifanya mbingu.
6 有尊榮和威嚴在他面前; 有能力與華美在他聖所。
Heshima na adhama ziko mbele zake. Nguvu na uzuri zimo katika patakatifu pake.
7 民中的萬族啊,你們要將榮耀、能力歸給耶和華, 都歸給耶和華!
Mpeni Yahwe sifa, enyi ukoo wa watu, mpeni sifa Yahwe kwa ajili ya utukufu wake na nguvu.
8 要將耶和華的名所當得的榮耀歸給他, 拿供物來進入他的院宇。
Mpeni Yahwe utukufu ambao unastahili jina lake. Leteni matoleo na muingie nyuani mwake.
9 當以聖潔的妝飾敬拜耶和華; 全地要在他面前戰抖!
Mpigieni magoti Yahwe mkiwa mmevaa mavazi ambayo yanaheshimu utakatifu wake. Nchi yote tetemekeni mbele zake.
10 人在列邦中要說:耶和華作王! 世界就堅定,不得動搖; 他要按公正審判眾民。
Semeni kati ya mataifa, Yahwe anatawala.” Ulimwengu pia umeimarishwa; hauwezi kutikiswa. Yeye huwahukumu watu kwa haki.
11 願天歡喜,願地快樂! 願海和其中所充滿的澎湃!
Mbingu na zifurahi, na nchi ishangilie; bahari na ivume na vyote viijazavyo vipige kelele kwa shangwe.
12 願田和其中所有的都歡樂! 那時,林中的樹木都要在耶和華面前歡呼。
Mashamba yashangilie na vyote vilivyomo. Kisha miti ya mstuni ipige kelele kwa furaha
13 因為他來了,他來要審判全地。 他要按公義審判世界, 按他的信實審判萬民。
mbele za Yahwe, maana yeye anakuja. Anakuja kuihukumu nchi. Naye atauhukumu ulumwengu kwa haki na mataifa kwa uaminifu wake.