< 詩篇 35 >

1 大衛的詩。 耶和華啊,與我相爭的,求你與他們相爭! 與我相戰的,求你與他們相戰!
Yahwe, uwashughulikie wale wanao nishughulikia mimi; upigane nao wanao pigana nami.
2 拿着大小的盾牌, 起來幫助我。
Uikamate ngao yako ndogo na ngao kubwa; inuka unisaidie.
3 抽出槍來,擋住那追趕我的; 求你對我的靈魂說:我是拯救你的。
Uutumie mkuki wako na shoka lako la vita kwa wale wanao nifukuzia; uuambie moyo wangu, “Mimi ni wokovu wako.”
4 願那尋索我命的,蒙羞受辱! 願那謀害我的,退後羞愧!
Waaibishwe na kudharauliwa wale wanaoutafuta uhai wangu. Warudishwe nyuma na wafedheheshwe wanao panga kunidhuru.
5 願他們像風前的糠, 有耶和華的使者趕逐他們。
Wao wawe makapi mbele ya upepo, malaika wakiwafutilia mbali.
6 願他們的道路又暗又滑, 有耶和華的使者追趕他們。
Njia yao na iwe giza na utelezi, malaika wa Yahwe wakiwafukuzia.
7 因他們無故地為我暗設網羅, 無故地挖坑,要害我的性命。
Wamenitegea mtego bila sababu; bila sababu wamechimba shimo kwa ajili ya uhai wangu.
8 願災禍忽然臨到他身上! 願他暗設的網纏住自己! 願他落在其中遭災禍!
Uharibifu na uwapate wao kwa kushitukiza. Mtego ambao wameutega na uwanase wao. Na wadumbukie humo, ili kwamba waangamizwe.
9 我的心必靠耶和華快樂, 靠他的救恩高興。
Bali mimi nitakuwa nafuraha ndani ya Yahwe na ndani ya wokovu wake.
10 我的骨頭都要說: 耶和華啊,誰能像你 救護困苦人脫離那比他強壯的, 救護困苦窮乏人脫離那搶奪他的?
Mifupa yangu yote itasema, “Yahwe, ni nani kama wewe, uokoaye walio onewa mkononi mwa walio na nguvu kuwazidi wao na masikini na wahitaji mkononi mwa wale wanaojaribu kuwaibia?”
11 凶惡的見證人起來, 盤問我所不知道的事。
Mashahidi wa uongo wamesimama; wananishitakia uongo.
12 他們向我以惡報善, 使我的靈魂孤苦。
Kwa ajili ya wema wananilipa mabaya. Nina huzuni nyingi.
13 至於我,當他們有病的時候, 我便穿麻衣,禁食,刻苦己心; 我所求的都歸到自己的懷中。
Lakini, walipokuwa akiugua, nilivaa magunia; nilifunga kwa ajili yao huku kichwa changu kikiinamia kifuani kwangu.
14 我這樣行,好像他是我的朋友,我的弟兄; 我屈身悲哀,如同人為母親哀痛。
Nilienenda katika huzuni kana kwamba walikuwa ni ndugu zangu; niliinama chini nikiomboleza kana kwamba ni kwa ajili ya mama yangu.
15 我在患難中,他們卻歡喜,大家聚集。 我所不認識的那些下流人聚集攻擊我; 他們不住地把我撕裂。
Bali mimi nilipokuwa mashakani, walifurahi sana na kukutanika pamoja; walikutanika pamoja kinyume na mimi, nami nilishangazwa nao. Walinirarua bila kuacha.
16 他們如同席上好嬉笑的狂妄人向我咬牙。
Kwa dharau kabisa walinidhihaki; walinisagia meno yao.
17 主啊,你看着不理要到幾時呢? 求你救我的靈魂脫離他們的殘害! 救我的生命脫離少壯獅子!
Bwana, mpaka lini utaendelea kutazama? uiokoe roho yangu na mashambulizi yao ya maagamizi uyaokoe maisha yangu na simba.
18 我在大會中要稱謝你, 在眾民中要讚美你。
Nami nitakushukuru wewe katika kusanyiko kubwa; nitakusifu kati ya watu wengi.
19 求你不容那無理與我為仇的向我誇耀! 不容那無故恨我的向我擠眼!
Usiwaache maadui zangu wadanganyifu kufurahi juu yangu; usiwaache waendelee na mipango yao ya uovu.
20 因為他們不說和平話, 倒想出詭詐的言語害地上的安靜人。
Kwa maana hawaongei amani, bali wanabuni maneno ya uongo kwa wale wanaoishi kwa amani katika ardhi yetu.
21 他們大大張口攻擊我,說: 阿哈,阿哈,我們的眼已經看見了!
Midomo yao inapaza sauti ikinishtaki; wakisema, Aha, Aha, macho yetu yameona.”
22 耶和華啊,你已經看見了,求你不要閉口! 主啊,求你不要遠離我!
Yahwe wewe umeona, usikae kimya; Bwana, usiwe mbali nami.
23 我的上帝我的主啊,求你奮興醒起, 判清我的事,伸明我的冤!
Inuka mwenyewe na usimame kunitetea; Mungu wangu na Bwana wangu, unitetee.
24 耶和華-我的上帝啊,求你按你的公義判斷我, 不容他們向我誇耀!
Kwa sabababu ya haki yako, Yahwe Mungu wangu, unitetee; usiwaache wafurahi kwa ajili yangu.
25 不容他們心裏說:阿哈,遂我們的心願了! 不容他們說:我們已經把他吞了!
Usiwaache waseme mioyoni mwao, “Aha, tumepata tulicho kihitaji.” Usiwaache waseme, tumemmeza.”
26 願那喜歡我遭難的一同抱愧蒙羞! 願那向我妄自尊大的披慚愧,蒙羞辱!
Uwaaibishe na kuwa fendhehesha wale wanaotaka kunidhuru. Wale wote wanao ni dhihaki wafunikwe kwa aibu na kudharauliwa.
27 願那喜悅我冤屈得伸的歡呼快樂; 願他們常說:當尊耶和華為大! 耶和華喜悅他的僕人平安。
Nao wote wanao tamani kudhihirishwa kwangu washangilie na wafurahi; siku zote waseme, “Usifiwe Yahwe, yeye ajifurahishaye katika mafanikio ya mtumishi wake.
28 我的舌頭要終日論說你的公義, 時常讚美你。
Kisha nitatangaza matendo yako ya haki na kukusifu wewe wakati wote.

< 詩篇 35 >