< 詩篇 25 >

1 大衛的詩。 耶和華啊,我的心仰望你。
Kwako, Yahwe, nayainua maisha yangu!
2 我的上帝啊,我素來倚靠你; 求你不要叫我羞愧, 不要叫我的仇敵向我誇勝。
Mungu wangu, ninaamini katika wewe. Usiniache niaibishwe; usiwaache maadui zangu wafurahie ushindi wao kwangu.
3 凡等候你的必不羞愧; 惟有那無故行奸詐的必要羞愧。
Asiaibishwe mtu yeyote anaye kutumaini bali waaibishwe wale watendao hila bila sababu!
4 耶和華啊,求你將你的道指示我, 將你的路教訓我!
Unijulishe njia zako, Yahwe; unifundishe njia zako.
5 求你以你的真理引導我,教訓我, 因為你是救我的上帝。 我終日等候你。
Uniongoze kwenye kweli yako na unifundishe, kwa kuwa wewe ni Mungu wa wokovu wangu; ninakutumainia wewe siku zote za maisha yangu.
6 耶和華啊,求你記念你的憐憫和慈愛, 因為這是亙古以來所常有的。
Kumbuka, Yahwe, matendo yako ya huruma na uaminifu wa agano lako; kwa kuwa vimekuwapo siku zote.
7 求你不要記念我幼年的罪愆和我的過犯; 耶和華啊,求你因你的恩惠,按你的慈愛記念我。
Usizikumbuke dhambi za ujana wangu wala uasi wangu; Uniweke akilini mwako pamoja na uaminifu wa agano kwa zababu ya uzuri wa wako, Yahwe!
8 耶和華是良善正直的, 所以他必指示罪人走正路。
Yahwe ni mzuri na mwenye haki; kwa hiyo yeye huwafundisha njia mwenye dhambi.
9 他必按公平引領謙卑人, 將他的道教訓他們。
Yeye huwaelekeza wanyenyekevu kwa kile kilicho sahihi na yeye huwafundisha wao njia yake.
10 凡遵守他的約和他法度的人, 耶和華都以慈愛誠實待他。
Njia zote za Yahwe ni za upendo wa kudumu na niaminifu kwa wote wanao tunza agano na maagizo ya amri zake.
11 耶和華啊,求你因你的名赦免我的罪, 因為我的罪重大。
Kwa ajili ya jina lako, Yahwe, unisamehe dhambi zangu, kwa kuwa ni nyingi mno.
12 誰敬畏耶和華, 耶和華必指示他當選擇的道路。
Ni nani ambaye anamuogopa Yahwe? Bwana atamfundisha yeye katika njia ambayo anapaswa kuichagua.
13 他必安然居住; 他的後裔必承受地土。
Maisha yake yataenenda katika uzuri; na uzao wake utairithi nchi.
14 耶和華與敬畏他的人親密; 他必將自己的約指示他們。
Urafiki wa Yahwe ni kwa ajili ya wale wanao mheshimu yeye, naye hulifanya agano lake lijulikane kwao.
15 我的眼目時常仰望耶和華, 因為他必將我的腳從網裏拉出來。
Siku zote macho yangu yanamtazama Yahwe, kwa kuwa yeye ataifungua miguu yangu kwenye nyavu.
16 求你轉向我,憐恤我, 因為我是孤獨困苦。
Unigeukie mimi na unihurumie; kwa maana niko peke yangu na niliye matesoni.
17 我心裏的愁苦甚多, 求你救我脫離我的禍患。
Maumivu ya moyo wangu yameongezeka; uniondoe katika dhiki hii!
18 求你看顧我的困苦,我的艱難, 赦免我一切的罪。
Tazama mateso yangu na taabu yangu; unisamehe dhambi zangu zote.
19 求你察看我的仇敵, 因為他們人多,並且痛痛地恨我。
Ona maadui zangu, kwa maana ni wengi; wananichukia kwa chuki ya kikatili.
20 求你保護我的性命,搭救我, 使我不致羞愧,因為我投靠你。
Uyalinde maisha yangu na uniokoe; usiniache niaibishwe, Kwa kuwa kwako nakimbilia usalama!
21 願純全、正直保守我, 因為我等候你。
Uadilifu na unyofu vinihifadhi, kwa kuwa nina kutumainia wewe.
22 上帝啊,求你救贖以色列脫離他一切的愁苦。
Mungu, uiokoe Israeli, na shida yake yote!

< 詩篇 25 >