< 詩篇 22 >

1 大衛的詩,交與伶長。調用朝鹿。 我的上帝,我的上帝!為甚麼離棄我? 為甚麼遠離不救我?不聽我唉哼的言語?
Mungu wangu, Mungu wangu, mbona umeniacha? Kwa nini uko mbali na wokovu wangu na mbali na maneno yangu yenye uchungu?
2 我的上帝啊,我白日呼求,你不應允, 夜間呼求,並不住聲。
Mungu wangu, ninalia mchana kutwa, lakini haunijibu, na wakati wa usiku sinyamazi!
3 但你是聖潔的, 是用以色列的讚美為寶座的。
Bado wewe ni mtakatifu; wewe umekaa kama mfalme pamoja na sifa za Israeli.
4 我們的祖宗倚靠你; 他們倚靠你,你便解救他們。
Mababu zetu walikuamini wewe, na wewe uliwaokoa wao.
5 他們哀求你,便蒙解救; 他們倚靠你,就不羞愧。
Walikulilia wewe nao waka okolewa. Wao walikuamini wewe na hawakuvunjwa moyo.
6 但我是蟲,不是人, 被眾人羞辱,被百姓藐視。
Bali mimi ni funza na sio mtu, nisiye faa kwa ubinadamu na hudharauliwa na watu.
7 凡看見我的都嗤笑我; 他們撇嘴搖頭,說:
Wale wote wanionao hunisuta; hunidhihaki; hunitikisia vichwa vyao.
8 他把自己交託耶和華,耶和華可以救他吧! 耶和華既喜悅他,可以搭救他吧!
Wao husema, “Yeye anamwamini Yahwe; mwache Yahwe amuokoe. Mwache amuokoe yeye, kwa kuwa yeye anampendeza sana Yeye.”
9 但你是叫我出母腹的; 我在母懷裏,你就使我有倚靠的心。
Kwa kuwa wewe ulinileta kutoka tumboni; wewe ulinifanya nikuamini wewe wakati nikiwa nanyonya matiti ya mama yangu.
10 我自出母胎就被交在你手裏; 從我母親生我,你就是我的上帝。
Nimekwisha tupwa kwako wewe tokea tumboni; wewe ni Mungu wangu tangu nikiwa tumboni mwa mama yangu!
11 求你不要遠離我! 因為急難臨近了,沒有人幫助我。
Usiwe mbali na mimi, kwa kuwa shida ikaribu; hayupo hata mmoja wa kusaidia.
12 有許多公牛圍繞我, 巴珊大力的公牛四面困住我。
Maksai wengi wananizunguka mimi; maksai wenye nguvu ya Bashan wananizunguka mimi.
13 牠們向我張口, 好像抓撕吼叫的獅子。
Wao wanafungua midomo yao kwangu kama simba aungurumaye akirarua windo lake.
14 我如水被倒出來; 我的骨頭都脫了節; 我心在我裏面如蠟鎔化。
Ninamwagwa nje kama maji, na mifupa yangu yote imeteguka. Moyo wangu ni kama nta; nao unayeyuka ndani ya sehemu zangu za ndani.
15 我的精力枯乾,如同瓦片; 我的舌頭貼在我牙床上。 你將我安置在死地的塵土中。
Nguvu zangu zimekaushwa kama kipande cha ufinyanzi; ulimi wangu unanata juu ya mdomo wangu. Wewe umenilaza mimi katika vumbi la mauti.
16 犬類圍着我,惡黨環繞我; 他們扎了我的手,我的腳。
Kwa maana mbwa wamenizunguka; kundi la watu waovu limenizunguka; wamenitoboa mikono yangu na miguu yangu.
17 我的骨頭,我都能數過; 他們瞪着眼看我。
Nami ninaweza kuihesabu mifupa yangu. Wao wananitazama na kunishangaa.
18 他們分我的外衣, 為我的裏衣拈鬮。
Wao wanagawa mavazi yangu kati yao wenyewe, wanapiga kura kwa ajili ya mavazi yangu.
19 耶和華啊,求你不要遠離我! 我的救主啊,求你快來幫助我!
Usiwe mbali, Yahwe; tafadhali harakisha kunisaidia mimi, nguvu yangu!
20 求你救我的靈魂脫離刀劍, 救我的生命脫離犬類,
Uiokoe roho yangu na upanga, maisha yangu mwenyewe na makucha ya mbwa mwitu.
21 救我脫離獅子的口; 你已經應允我,使我脫離野牛的角。
Uniokoe na mdomo wa simba; uniokoe na mapembe ya ng'ombe wa porini.
22 我要將你的名傳與我的弟兄, 在會中我要讚美你。
Nami nitalitangaza jina lako kwa ndugu zangu; katikati ya kusanyiko la watu nitakusifu wewe.
23 你們敬畏耶和華的人要讚美他! 雅各的後裔都要榮耀他! 以色列的後裔都要懼怕他!
Ninyi mnao mwogopa Yahwe, msifuni yeye! Ninyi nyote kizazi cha Yakobo, muheshimuni yeye! Simameni katika hofu yake, ninyi nyote kizazi cha Israeli!
24 因為他沒有藐視憎惡受苦的人, 也沒有向他掩面; 那受苦之人呼籲的時候,他就垂聽。
Kwa kuwa haja dharau au kuchukia mateso ya aliye taabishwa; Yahwe hajamficha uso wake yeye; pindi wale walio taabishwa walipo mlilia yeye, yeye alisikia.
25 我在大會中讚美你的話是從你而來的; 我要在敬畏耶和華的人面前還我的願。
Yahwe, katika kusanyiko la watu wako nitakusifu kwa yale uliyo tenda; nami nitatimiza nadhiri zangu mbele ya wale wanao muhofu yeye.
26 謙卑的人必吃得飽足; 尋求耶和華的人必讚美他。 願你們的心永遠活着!
Walio onewa watakula na kutosheka; wale ambao humtafuta Yahwe watamsifu yeye. Mioyo yenu iishi milele.
27 地的四極都要想念耶和華,並且歸順他; 列國的萬族都要在你面前敬拜。
Watu wote wa duniani watakumbuka na kumrudia Yahwe; familia zote za mataifa watapiga magoti chini mbele yako.
28 因為國權是耶和華的; 他是管理萬國的。
Kwa kuwa utawala ni wa Yahwe; yeye ni mtawala wa mataifa.
29 地上一切豐肥的人必吃喝而敬拜; 凡下到塵土中-不能存活自己性命的人 -都要在他面前下拜。
Watu wote wa duniani waliofanikiwa wata sherekea na wata abudu; wale wote washukao katika mavumbi watapiga magoti mbele zake, wale ambao hawawezi kulinda maisha yao wenyewe.
30 他必有後裔事奉他; 主所行的事必傳與後代。
Kizazi kijacho kitamtumikia yeye; wao watakiambia kizazi kinachofuatia kuhusu Bwana.
31 他們必來把他的公義傳給將要生的民, 言明這事是他所行的。
Wao watakuja na kuzungumza kuhusu haki yake; wao watawaambia watu ambao bado hawaja zaliwa yale ambayo Yahwe ameyafanya!

< 詩篇 22 >