< 詩篇 104 >
1 我的心哪,你要稱頌耶和華! 耶和華-我的上帝啊,你為至大! 你以尊榮威嚴為衣服,
Nitamsifu Yahwe maisha yangu yote, Ewe Yahwe Mungu wangu, wewe ni mkubwa sana; umevikwa kwa utukufu na enzi.
Unajifunika mwenyewe kwa nuru kama kwa mavazi; umetandaza mbingu kama pazia za hema.
3 在水中立樓閣的棟樑, 用雲彩為車輦, 藉着風的翅膀而行,
Umeweka mawinguni mihimili ya vyumba vyako; huyafanya mawingu gari lako; hutembea juu ya mbawa za upepo.
Yeye huufanya upepo kuwa wajumbe wake, miale ya moto kuwa watumishi wake.
Aliiweka misingi ya nchi, nayo haitahamishwa kamwe.
Wewe uliifunika nchi kwa maji kama kwa mavazi; maji yalifunika milima.
7 你的斥責一發,水便奔逃; 你的雷聲一發,水便奔流。
Kukemea kwako kulifanya maji kupungua; kwa sauti ya radi yako yakaondoka kasi.
Milima iliinuka, na mabonde yakaenea mahali ambapo wewe ulikwisha pachagua kwa ajili yao.
9 你定了界限,使水不能過去, 不再轉回遮蓋地面。
Umeweka mipaka kwa ajili yao ambao hayawezi kuupita; hayawezi kuifunika nchi tena.
Yeye alifanya chemchemi kutiririsha maji mabondeni; mito kutiririka katikati ya milima.
Inasambaza maji kwa ajili ya wanyama wote wa shambani; punda wa porini hukata kiu yao.
Kandokando ya mito ndege hujenga viota vyao; huimba kati ya matawi.
13 他從樓閣中澆灌山嶺; 因他作為的功效,地就豐足。
Humwagilia milima kutoka katika chumba chake cha maji mawinguni. Nchi imejazwa kwa matunda ya kazi yake.
14 他使草生長,給六畜吃, 使菜蔬發長,供給人用, 使人從地裏能得食物,
Huzifanya nyasi kukua kwa ajili ya mifugo na mimea kwa ajili ya binadamu kulima ili kwamba mwanadamu aweze kuzalisha chakula toka nchini.
15 又得酒能悅人心, 得油能潤人面, 得糧能養人心。
Hutengeneza mvinyo kumfurahisha mwanadamu, mafuta yakumfanya uso wake ung'ae, na chakula kwa ajili ya kuimarisha uhai wake.
16 佳美的樹木,就是黎巴嫩的香柏樹, 是耶和華所栽種的,都滿了汁漿。
Miti ya Yahwe hupata mvua nyingi; Mierezi ya Lebanoni aliyoipanda.
Hapo ndege hutengeneza viota vyao. Na korongo, misunobari ni nyuma yake.
Mbuzi mwitu huishi kwenye milima mrefu; na urefu wa milima ni kimilio la wibari.
Aliuchagua mwezi kuweka alama ya majira; jua latambua kuchwa kwake.
Wewe hufanya giza la usiku ambapo wanyama wote wa msituni hutoka nje.
Wana simba huunguruma kwa ajili ya mawindo na hutafuta chakula chao kutoka kwa Mungu.
Jua linapochomoza, huenda zao na kujilaza mapangoni mwao.
Wakati huo huo, watu hutoka nje kuelekea kazi zao na utumishi wake mpaka jioni.
24 耶和華啊,你所造的何其多! 都是你用智慧造成的; 遍地滿了你的豐富。
Yahwe, ni jinsi gani kazi zako zilivyo nyingi na za aina mbalimbali! Kwa hekima ulizifanya zote; nchi inafurika kwa kazi zako.
25 那裏有海,又大又廣; 其中有無數的動物, 大小活物都有。
Kule kuna bahari, yenye kina kirefu na pana, ikiwa na viume vingi visivyo hesabika, vyote vidogo na vikubwa.
Meli husafili humo, na ndimo alimo Lewiathani uliye muumba acheze baharini.
Hawa wote hukutazama wewe uwape chakula kwa wakati.
28 你給牠們,牠們便拾起來; 你張手,牠們飽得美食。
Unapowapa chakula, hukusanyika; ufunguapo mkono wako, wanatosheka.
29 你掩面,牠們便驚惶; 你收回牠們的氣,牠們就死亡,歸於塵土。
Unapouficha uso wako, wanateseka; ukiiondoa pumzi yao, wanakufa na kurudi mavumbini.
30 你發出你的靈,牠們便受造; 你使地面更換為新。
Unapotuma Roho yako, wanaumbwa, nawe unaifanya upya nchi.
31 願耶和華的榮耀存到永遠! 願耶和華喜悅自己所造的!
Utukufu wa Yahwe na udumu milele; Yahwe na aufurahie uumbaji wake.
Yeye hutazama nchi, nayo hutikisika; huigusa milima, nayo hutoa moshi.
33 我要一生向耶和華唱詩! 我還活的時候,要向我上帝歌頌!
Nitamwimbia Yahwe maisha yangu yote; nitamwimbia sifa Mungu wangu nigali ninaishi.
Mawazo yangu na yawe matamu kwake; nitafurahia katika Yahwe.
35 願罪人從世上消滅! 願惡人歸於無有! 我的心哪,要稱頌耶和華! 你們要讚美耶和華!
Wenye dhambi na waondoshwe katika nchi, na waovu wasiwepo tena. Ninamsifu Yahwe maisha yangu yote. Msifuni Yahwe.