< 詩篇 101 >
1 大衛的詩。 我要歌唱慈愛和公平; 耶和華啊,我要向你歌頌!
Nitaimba uaminifu wa agano lako na hukumu; kwako, Ee Yahwe, Nitakuimbia sifa.
2 我要用智慧行完全的道。 你幾時到我這裏來呢? 我要存完全的心行在我家中。
Nitatembea katika njia ya uadilifu. Oh, ni lini utakuja kwangu? Nitatembea kwa uadilifu ndani ya nyumba yangu.
3 邪僻的事,我都不擺在我眼前; 悖逆人所做的事,我甚恨惡, 不容沾在我身上。
Sitaweka matendo maovu mbele ya macho yangu; ninachukia uovu usio na maana; hauta shikamana nami.
4 彎曲的心思,我必遠離; 一切的惡人,我不認識。
Watu waliopotoka wataniacha mimi; mimi sichangamani na uovu.
5 在暗中讒謗他鄰居的,我必將他滅絕; 眼目高傲、心裏驕縱的,我必不容他。
Nitamwangamiza yeyote amsengenyaye jirani yake kwa siri. Sitamvumilia yeyote mwenye kiburi.
6 我眼要看國中的誠實人,叫他們與我同住; 行為完全的,他要伺候我。
Nitawachagua walio waaminifu katika nchi wakae upande wangu. Wale watembeao katika njia ya uhadilifu watanitumikia.
7 行詭詐的,必不得住在我家裏; 說謊話的,必不得立在我眼前。
Watu wadanganyifu hawatabaki ndani ya nyumba yangu; waongo hawatakaribishwa mbele ya macho yangu.
8 我每日早晨要滅絕國中所有的惡人, 好把一切作孽的從耶和華的城裏剪除。
Asubuhi hata asubuhi nitawaangamiza waovu wote kutoka nchini; nitawaondoa watendao maovu wote katika mji wa Yahwe.