< 箴言 7 >

1 我兒,你要遵守我的言語, 將我的命令存記在心。
Mwanangu, yatunze maneno yangu na ndani yako udhihifadhi amri zangu.
2 遵守我的命令就得存活; 保守我的法則, 好像保守眼中的瞳人,
Uzilinde amri zangu ili uishi na uyatunzetu mafundisho yangu kama mboni ya jicho.
3 繫在你指頭上, 刻在你心版上。
Uyafunge katika vidole vyako; uyaandike katika kibao cha moyo wako.
4 對智慧說:你是我的姊妹, 稱呼聰明為你的親人,
Mwambie hekima, “wewe ni dada yangu,” na ufahamu mwite jamaa yako,
5 她就保你遠離淫婦, 遠離說諂媚話的外女。
ili ujitunze mwenyewe dhidi ya mwanake haramu, dhidi ya mwanamke mgeni mwenye maneno laini.
6 我曾在我房屋的窗戶內, 從我窗欞之間往外觀看:
Nilikuwa naangalia kwenye wavu wa dirisha la nyumba yangu.
7 見愚蒙人內,少年人中, 分明有一個無知的少年人,
Nikawatazama watu mwenye ukosefu wa uzoefu, na miongoni mwa watu vijana nikamwona kijana asiye na akili.
8 從街上經過,走近淫婦的巷口, 直往通她家的路去,
Kijana huyo alishuka mtaani kwenye kona karibu na yule mwanamke, akaenda kwenye nyumba yake.
9 在黃昏,或晚上, 或半夜,或黑暗之中。
Ilikuwa katika utusiutusi wa siku muda wa jioni, wakati wa usiku na giza.
10 看哪,有一個婦人來迎接他, 是妓女的打扮,有詭詐的心思。
Akakutana na yule mwanake, amevaa kama kahaba, katika moyo wa udanyanyifu.
11 這婦人喧嚷,不守約束, 在家裏停不住腳,
Alikuwa na kelele na upotovu; miguu yake haikutulia kwenye masikani.
12 有時在街市上,有時在寬闊處, 或在各巷口蹲伏,
Alielekea mitaani, kisha sehemu ya sokoni, na katika kila upande alisubiri kwa kuviza.
13 拉住那少年人,與他親嘴, 臉無羞恥對他說:
Basi akamshika na kumbusu, kwa uso wa nguvu akamwambia,
14 平安祭在我這裏, 今日才還了我所許的願。
leo nimetoa sadaka yangu ya amani, nimelipa nadhili yangu,
15 因此,我出來迎接你, 懇切求見你的面,恰巧遇見了你。
hivyo nilikuja kukutana nawe, kuutafuta uso wako kwa hamu, na sasa nimekupata.
16 我已經用繡花毯子 和埃及線織的花紋布鋪了我的床。
Nimeweka matandiko juu ya kitanda changu, kitani za rangi kutoka Misri.
17 我又用沒藥、沉香、桂皮 薰了我的榻。
Kitanda changu nimenyunyizia manemane, udi na mdalasini.
18 你來,我們可以飽享愛情,直到早晨; 我們可以彼此親愛歡樂。
Njoo, tunywe tujishibishe kwa upendo wetu hata asubuhi; tupate furaha kuu kwa matendo ya mahaba.
19 因為我丈夫不在家,出門行遠路;
Maana mume wangu hayupo nyumbani kwake; amekwenda safari ya mbali.
20 他手拿銀囊,必到月望才回家。
Alichukua mkoba wa fedha; atarudi siku ya mwezi mpevu.
21 淫婦用許多巧言誘他隨從, 用諂媚的嘴逼他同行。
katika maneno yake mengi akamshinda; na kwa midomo yake laini anampotosha.
22 少年人立刻跟隨她,好像牛往宰殺之地; 又像愚昧人帶鎖鍊去受刑罰,
Ghafula alimfuata kama maksai anayekwenda kwa mchinjaji, kama ayala aliyekamatwa kwa nguvu,
23 直等箭穿他的肝; 如同雀鳥急入網羅,卻不知是自喪己命。
mpaka mshale upasue ini lake. Alikuwa kama ndege anayekimbili kwenye mtego. Hakujua kuwa itamgharimu maisha yake.
24 眾子啊,現在要聽從我, 留心聽我口中的話。
Na sasa, wanangu, nisikilizeni; zingatieni maneno ya kinywa changu.
25 你的心不可偏向淫婦的道, 不要入她的迷途。
Moyo wako usiyageukie mapito yake; usipotoshwe katika mapito yake.
26 因為,被她傷害仆倒的不少; 被她殺戮的而且甚多。
Amesababisha watu wengi kuanguka kwa kuwajeruhi; ameua watu wengi.
27 她的家是在陰間之路, 下到死亡之宮。 (Sheol h7585)
Nyumba yake ipo juu ya barabara ya kwenda kuzimu; huelekea chini kwenye vyumba vya mauti. (Sheol h7585)

< 箴言 7 >