< 民數記 7 >

1 摩西立完了帳幕,就把帳幕用膏抹了,使它成聖,又把其中的器具和壇,並壇上的器具,都抹了,使它成聖。
Siku ambayo Musa alikamilsha masikani, alitia mafuta na kuiweka wakfu kwa BWANA, pamoja na mapambo yake. Aliifanyia hivyo madhabahu na vyombo vyake. Aliitia mafuta na kuiweka wakfu kwa BWANA.
2 當天,以色列的眾首領,就是各族的族長,都來奉獻。他們是各支派的首領,管理那些被數的人。
Siku hiyo, viongozi wa Israeli na wale vichwa vya familia za mababu walitoa sadaka. Hawa wanaume walikuwa viongozi wa makabila. Walisaidia kuhesabu watu kwenye ile sensa.
3 他們把自己的供物送到耶和華面前,就是六輛篷子車和十二隻公牛。每兩個首領奉獻一輛車,每首領奉獻一隻牛。他們把這些都奉到帳幕前。
Walileta sadaka zao kwa BWANA. Walileta magari sita yaliyofunikwa na mafahari kumi na mbili. Walileta gari moja kwa kila viongozi wawili, kila kiongozi alileta fahari moja. Walileta vitu hivi mbele ya masikani.
4 耶和華曉諭摩西說:
Kisha BWANA akanena na Musa, akamwambia,
5 「你要收下這些,好作會幕的使用,都要照利未人所辦的事交給他們。」
“Uzipokee hizo sadaka kutoka kwao na uzitumie kwa matumizi ya kazi ya hema ya kukutania. Uwape hizo sadaka Walawi, kwa kila mmoja kadri ya uhitaji wa kazi yake.”
6 於是摩西收了車和牛,交給利未人,
Musa akayatwaa yale magari na mafahari. na kuwapatia Walawi.
7 把兩輛車,四隻牛,照革順子孫所辦的事交給他們,
Aliwapa magari mawili na mafahari wanne wale wa uzao wa Gerishoni, kwa sababu ndivyo kazi yao ilivyohitaji.
8 又把四輛車,八隻牛,照米拉利子孫所辦的事交給他們;他們都在祭司亞倫的兒子以他瑪手下。
Aliwapatia uzao wa Merari magari manne na mafahari nane, chini ya uangalizi wa Ithamari mwana wa Haruni kuhani. Alifanya hivi kwa sababu ya uhitaji wa kazi yao.
9 但車與牛都沒有交給哥轄子孫;因為他們辦的是聖所的事,在肩頭上抬聖物。
Lakini wale wa uzao wa Kohathi hakuwapa chochote kwa sababu wao waliangalia vitu vtakatifu amabvyo vilipaswa vibebwe mabagani mwao, siyo kwa magari.
10 用膏抹壇的日子,首領都來行奉獻壇的禮,眾首領就在壇前獻供物。
Viongozi walitoa bidhaa zo zingine kwa ajili ya kuwekwa wakfu kwa madhabahu katika siku ile ambayo Musa aliitia mafuta madhabahu. Viongozi walitoa sadaka zao mbele ya madhabahu hiyo.
11 耶和華對摩西說:「眾首領為行奉獻壇的禮,要每天一個首領來獻供物。」
BWANA akasema na Musa, “kila kiongozi atatoa sadaka kwa siku yake kwa ajili ya kuiweka wakfu madhabahu.”
12 頭一日獻供物的是猶大支派的亞米拿達的兒子拿順。
Katika siku ya kwanza, Nashoni mwana wa Aminadabu, wa kabila ya Yuda, alitoa sadaka yake.
13 他的供物是:一個銀盤子,重一百三十舍客勒,一個銀碗,重七十舍客勒,都是按聖所的平,也都盛滿了調油的細麵作素祭;
Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja ya fedha ambayo uzito wake ni shekeli sabini, kwa kipimo cha mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
14 一個金盂,重十舍客勒,盛滿了香;
Pia alimpa unga wa dhahabu kiasi cha bakuli moja chenye uzani wa shekeli kumi kilichojaa ubani
15 一隻公牛犢,一隻公綿羊,一隻一歲的公羊羔作燔祭;
Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mchanga, kondoo dume mmoja na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.
16 一隻公山羊作贖罪祭;
Alitoa beberu kama kama sadaka ya hatia.
17 兩隻公牛,五隻公綿羊,五隻公山羊,五隻一歲的公羊羔作平安祭。這是亞米拿達兒子拿順的供物。
Alitoa makisai mbili, kondoo waume watano, beberu watano na wanakondoo dume watano wenye umri wa mwaka mmoja mmoja, kama sadaka ya amani. Hii ilikuwa sadaka ya Nashoni mwana wa Aminadabu.
18 第二日來獻的是以薩迦子孫的首領、蘇押的兒子拿坦業。
Siku ya pili, Nethanel mwana wa Zuari, kiongozi wa Isakari, alitoa sadaka yake.
19 他獻為供物的是:一個銀盤子,重一百三十舍客勒,一個銀碗,重七十舍客勒,都是按聖所的平,也都盛滿了調油的細麵作素祭;
Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha ya uzito wa shekeli130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa sheli sabini, kwa kipimo cha mahali patakatifu. Viyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kwa sadaka ya unga.
20 一個金盂,重十舍客勒,盛滿了香;
Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzito wa shekeli kumi, iliyojaa ubani.
21 一隻公牛犢,一隻公綿羊,一隻一歲的公羊羔作燔祭;
Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo mmoja dume.
22 一隻公山羊作贖罪祭;
Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
23 兩隻公牛,五隻公綿羊,五隻公山羊,五隻一歲的公羊羔作平安祭。這是蘇押兒子拿坦業的供物。
Alitoa makisai wawili, Kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hiii likuwa sadaka ya Nethaneli mwana wa Zuari.
24 第三日來獻的是西布倫子孫的首領、希倫的兒子以利押。
Siku ya tatu, Eliabu mwana wa Heloni, kiongozi wa uzao wa Zabuloni alitoa sadaka yake.
25 他的供物是:一個銀盤子,重一百三十舍客勒,一個銀碗,重七十舍客勒,都是按聖所的平,也都盛滿了調油的細麵作素祭;
Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130, na bakuli moja la fedha lenye uzito wa shekeli sabini kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. vyombo vyote hivi vilikuwa vimeja unga mwembemba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
26 一個金盂,重十舍客勒,盛滿了香;
Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
27 一隻公牛犢,一隻公綿羊,一隻一歲的公羊羔作燔祭;
Alitoa sadaka ya fahari mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja.
28 一隻公山羊作贖罪祭;
Alitoa beberu mmoja kama sadaka ya dhambi.
29 兩隻公牛,五隻公綿羊,五隻公山羊,五隻一歲的公羊羔作平安祭。這是希倫兒子以利押的供物。
Alitoa makisai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja. kuwa sadaka ya amani. Hii ilikuwa sadaka ya Eliabu mwana Heloni.
30 第四日來獻的是呂便子孫的首領、示丟珥的兒子以利蓿。
Siku ya nne, Elizuri mwana wa shedeuri, kiongozi wa uzao wa Reubeni, alitoa sadaka yake.
31 他的供物是:一個銀盤子,重一百三十舍客勒,一個銀碗,重七十舍客勒,都是按聖所的平,也都盛滿了調油的細麵作素祭;
Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
32 一個金盂,重十舍客勒,盛滿了香;
Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichoo jaa ubani.
33 一隻公牛犢,一隻公綿羊,一隻一歲的公羊羔作燔祭;
Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, mwanakondoo dume mmoja mchanga wa mwaka mmoja.
34 一隻公山羊作贖罪祭;
Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
35 兩隻公牛,五隻公綿羊,五隻公山羊,五隻一歲的公羊羔作平安祭。這是示丟珥的兒子以利蓿的供物。
Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ilikuwa sadaka ya Elizuri mwana wa Shedeuri.
36 第五日來獻的是西緬子孫的首領、蘇利沙代的兒子示路蔑。
Siku ya tano, Shelumieli mwana wa Zurishadai, kiongozi wa uzao wa Simeoni, alitoa sadaka yake.
37 他的供物是:一個銀盤子,重一百三十舍客勒,一個銀碗,重七十舍客勒,都是按聖所的平,也都盛滿了調油的細麵作素祭;
Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekali 130 na bakuli mojala fedha lenye uzani wa shekeli sabini kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
38 一個金盂,重十舍客勒,盛滿了香;
Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, uliojaa ubani.
39 一隻公牛犢,一隻公綿羊,一隻一歲的公羊羔作燔祭;
Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mchanga, dume la kondoo, na dume la mwanakondoo la mwaka mmoja.
40 一隻公山羊作贖罪祭;
Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
41 兩隻公牛,五隻公綿羊,五隻公山羊,五隻一歲的公羊羔作平安祭。這是蘇利沙代兒子示路蔑的供物。
Alitao maksai wawili, dume wawili wa kondoo, beberu watano, na dume watano wa wanakondoo wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka y amani. Hiindiyo iliyokuwa sadka ya Shelumei mwana wa Zurishadai.
42 第六日來獻的是迦得子孫的首領、丟珥的兒子以利雅薩。
Siku ya sita, Eliasafu mwana wa Deuli, kiongozi wa uzao wa Gadi, alitoa sadaka yake.
43 他的供物是:一個銀盤子,重一百三十舍客勒,一個銀碗,重七十舍客勒,都是按聖所的平,也都盛滿了調油的細麵作素祭;
Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli la shaba lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote vilikuwa vimejaa unga mwembemba uliochanganywa na mafuta kwa ajili ya sadaka ya unga.
44 一個金盂,重十舍客勒,盛滿了香;
Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
45 一隻公牛犢,一隻公綿羊,一隻一歲的公羊羔作燔祭;
Alitoa sadaka ya kuteketezwa ya fahari changa, kondoo dume mmoja, na dume la mwanakondoo mmoja wa mwaka mmoja.
46 一隻公山羊作贖罪祭;
Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
47 兩隻公牛,五隻公綿羊,五隻公山羊,五隻一歲的公羊羔作平安祭。這是丟珥的兒子以利雅薩的供物。
Alitoa maksai wawili, dume watano wa kondoo, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Eliasafu mwana wa Deuli.
48 第七日來獻的是以法蓮子孫的首領、亞米忽的兒子以利沙瑪。
Siku ya saba, Elishama mwana wa Amihudi, kiongozi wa uzao wa Efraimu, alitoa sadaka yake.
49 他的供物是:一個銀盤子,重一百三十舍客勒,一個銀碗,重七十舍客勒,都是按聖所的平,也都盛滿了調油的細麵作素祭;
Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo hivi vyote ilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
50 一個金盂,重十舍客勒,盛滿了香;
Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu, kilichojaa ubani
51 一隻公牛犢,一隻公綿羊,一隻一歲的公羊羔作燔祭;
Alitoa sadaka ya kuteketezwa, fahari mmoja, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.
52 一隻公山羊作贖罪祭;
Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
53 兩隻公牛,五隻公綿羊,五隻公山羊,五隻一歲的公羊羔作平安祭。這是亞米忽兒子以利沙瑪的供物。
Alitoa maksai wawili, kondo dume watano, beberu watano, na na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo ilikuwa sdaka ya Elishama mwana wa Amidu.
54 第八日來獻的是瑪拿西子孫的首領、比大蓿的兒子迦瑪列。
Siku y a nane, Gamaliel mwana wa Pedazuri, kiongozi wa uzao wa Manase, alitoa sadaka yake.
55 他的供物是:一個銀盤子,重一百三十舍客勒,一個銀碗,重七十舍客勒,都是按聖所的平,也都盛滿了調油的細麵作素祭;
Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
56 一個金盂,重十舍客勒,盛滿了香;
Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
57 一隻公牛犢,一隻公綿羊,一隻一歲的公羊羔作燔祭;
Alitoa sadaka ya kuteketezwa ya fahari mmoja, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.
58 一隻公山羊作贖罪祭;
Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
59 兩隻公牛,五隻公綿羊,五隻公山羊,五隻一歲的公羊羔作平安祭。這是比大蓿兒子迦瑪列的供物。
Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Gamaliel mwana wa Pedazuri.
60 第九日來獻的是便雅憫子孫的首領、基多尼的兒子亞比但。
Siku ya tisa, Abidani mwana wa Gidioni, kiongozi wa uzao wa Benjamini, alitoa sadaka yake.
61 他的供物是:一個銀盤子,重一百三十舍客勒,一個銀碗,重七十舍客勒,都是按聖所的平,也都盛滿了調油的細麵作素祭;
Sadaka yake ilikuwa sahani moja yafedha yenye uzani wa sheli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzito wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
62 一個金盂,重十舍客勒,盛滿了香;
Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
63 一隻公牛犢,一隻公綿羊,一隻一歲的公羊羔作燔祭;
Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, kondoo dume mmoja, na mwanakondoo dume mmoja wa mwaka mmoja.
64 一隻公山羊作贖罪祭;
Alitoa beberu mmoja kuwa sadaka ya dhambi.
65 兩隻公牛,五隻公綿羊,五隻公山羊,五隻一歲的公羊羔作平安祭。這是基多尼兒子亞比但的供物。
Alitoa makisai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Abidani mwana wa Gidioni.
66 第十日來獻的是但子孫的首領、亞米沙代的兒子亞希以謝。
Siku ya kumi, Ahizeri mwana wa Amishadai kiongozi wa Dani alitoa sadaka yake.
67 他的供物是:一個銀盤子,重一百三十舍客勒,一個銀碗,重七十舍客勒,都是按聖所的平,也都盛滿了調油的細麵作素祭;
Alitoa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekeli 130 na bakuli moja lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
68 一個金盂,重十舍客勒,盛滿了香;
Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzito wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
69 一隻公牛犢,一隻公綿羊,一隻一歲的公羊羔作燔祭;
Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, dume moja la kondoo, na dume moja la mwanakondoo wa mwaka mmoja.
70 一隻公山羊作贖罪祭;
Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
71 兩隻公牛,五隻公綿羊,五隻公山羊,五隻一歲的公羊羔作平安祭。這是亞米沙代兒子亞希以謝的供物。
Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja, kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Ahizeri mwana wa Amishadai.
72 第十一日來獻的是亞設子孫的首領、俄蘭的兒子帕結。
Siku ya kumi na moja. Pagieli mwana wa Okrani kiongozi wa uzao wa Asheri alaitoa sadaka yake.
73 他的供物是:一個銀盤子,重一百三十舍客勒,一個銀碗,重七十舍客勒,都是按聖所的平,也都盛滿了調油的細麵作素祭;
Sadaka yake ilikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabani, kwa kipimo cha shekeli ya mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi ilikuwa vimejaa unga mwembamba uliochanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
74 一個金盂,重十舍客勒,盛滿了香;
Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
75 一隻公牛犢,一隻公綿羊,一隻一歲的公羊羔作燔祭;
Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga. dume la kondoo moja, dume moja la mwanakondoo wa mwaka mmoja.
76 一隻公山羊作贖罪祭;
Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
77 兩隻公牛,五隻公綿羊,五隻公山羊,五隻一歲的公羊羔作平安祭。這是俄蘭兒子帕結的供物。
Alitoa maksai wawili, dume watano wa kondoo, na wanakondoo dume watano kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Pagieli mwana wa Okrani.
78 第十二日來獻的是拿弗他利子孫的首領、以南兒子亞希拉。
Siku ya kumi na mbili., Ahira mwana wa Enani, kiongozi wa uzao wa Naftali, alitoa sadaka yake.
79 他的供物是:一個銀盤子,重一百三十舍客勒,一個銀碗,重七十舍客勒,都是按聖所的平,也都盛滿了調油的細麵作素祭;
Sadaka yake ailikuwa sahani moja ya fedha yenye uzani wa shaekeli 130 na bakuli moja la fedha lenye uzani wa shekeli sabini, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu. Vyombo vyote hivi vilikuwa vimejaa unga mwembamba ulichanganywa na mafuta kuwa sadaka ya unga.
80 一個金盂,重十舍客勒,盛滿了香;
Pia alitoa kijiko kimoja cha dhahabu chenye uzani wa shekeli kumi, kilichojaa ubani.
81 一隻公牛犢,一隻公綿羊,一隻一歲的公羊羔作燔祭;
Alitoa sadaka ya kuteketezwa fahari mmoja mchanga, dume moja la kondoo, na mwanakondoo dume moja wa mwaka mmoja.
82 一隻公山羊作贖罪祭;
Alitoa beberu moja kuwa sadaka ya dhambi.
83 兩隻公牛,五隻公綿羊,五隻公山羊,五隻一歲的公羊羔作平安祭。這是以南兒子亞希拉的供物。
Alitoa maksai wawili, kondoo dume watano, beberu watano, na wanakondoo dume watano wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ndiyo iliyokuwa sadaka ya Ahra mwana wa Enani.
84 用膏抹壇的日子,以色列的眾首領為行獻壇之禮所獻的是:銀盤子十二個,銀碗十二個,金盂十二個;
Viongozi wa Israeli waliviweka wakfu hivi vitu vyote siku ambayo Musa alimimina mafuta kwenye madhabahu. Waliziweka wakfu zile sahani kumi na mbili za fedha, Bakuli kumi na mbili za fedha, na vijiko kumi na vili vya dhahabu.
85 每盤子重一百三十舍客勒,每碗重七十舍客勒。一切器皿的銀子,按聖所的平,共有二千四百舍客勒。
Zile sahani za fedha kila moja ilikuwa na uzani wa shaekeli 130 na kila bakuli ye fedha ilikuwa na uzani wa shekeli sabini. Vyombo vyote vya fedh vilikuwa na ujumla ya uzani wa shekeli 2, 400, kwa kipimo cha shekeli za mahali patakatifu.
86 十二個金盂盛滿了香,按聖所的平,每盂重十舍客勒,所有的金子共一百二十舍客勒。
Vile vijiko vya dhahabu vilivyokuwa vimejaa ubani, vilikuwa na uzani wa shekeli kumi kila kimoja. Vijiko vyote vya dhahabu vilikuwa na uzani wa shekeli 120.
87 作燔祭的,共有公牛十二隻,公羊十二隻,一歲的公羊羔十二隻,並同獻的素祭作贖罪祭的公山羊十二隻;
Waliwatenga wanyama wote kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, fahari kumi na wawili, kondoo dume kumi na wawili, na wanakondoo dume kumi na wawili wa mwaka mmoja mmoja. Walitoa sadaka yao ya unga. Walitoa beberu kumi na wawili kuwa sadaka ya dhambi.
88 作平安祭的,共有公牛二十四隻,公綿羊六十隻,公山羊六十隻,一歲的公羊羔六十隻。這就是用膏抹壇之後,為行奉獻壇之禮所獻的。
Kutokana na ng'ombe zao, walitoa fahari ishirini na nne, kondoo dume sitini beberu sitini, na wanakondoo dume sitini wa mwaka mmoja mmoja kuwa sadaka ya amani. Hii ilikuwa kwa ajiliya kuiweka wafu ile madhabahu baada ya kumiminiwa mafuta.
89 摩西進會幕要與耶和華說話的時候,聽見法櫃的施恩座以上、二基路伯中間有與他說話的聲音,就是耶和華與他說話。
Musa alipoingia kwenye hema ya kukutania kusema na BWANA, ndipo alipoisikia sauti yake ikisema naye. BWANA alinena naye kutoka juu ya kiti cha rehema kilichokuwa juu ya sanduku la ushahidi, kutoka katikati ya makerubi. Alinena naye.

< 民數記 7 >