< 民數記 3 >
1 耶和華在西奈山曉諭摩西的日子,亞倫和摩西的後代如下:
Sasa hii ndiyo historia ya uzao wa Haruni na Musa wakati BWANA aliposema na Musa kwenye mlima Sinai.
2 亞倫的兒子,長子名叫拿答,還有亞比戶、以利亞撒、以他瑪。
Majina ya watoto wa Haruni walikuwa Nadabu ambaye ndiyo mtoto wa kwanza, na Abihu, na Eliezeri, na Ithamari.
3 這是亞倫兒子的名字,都是受膏的祭司,是摩西叫他們承接聖職供祭司職分的。
Haya ndiyo majina ya wana wa Haruni, makuhani waliokuwa wamepakwa mafuta na kuwekwa wakfu kutumika kama makuhani.
4 拿答、亞比戶在西奈的曠野向耶和華獻凡火的時候就死在耶和華面前了。他們也沒有兒子。以利亞撒、以他瑪在他們的父親亞倫面前供祭司的職分。
Lakini Nadabu na Abihu walikufa mbele ya BWANA walipomtolea moto usiokubalika walipokuwa katika nyika ya Sinai. Nadabu na Abihu hawakuwa na watoto, kwa hiyo Eliazari na Ithamari walitumika kama makuhani pamoja na baba yao.
BWANA alinena na Musa, akamwambia,
6 「你使利未支派近前來,站在祭司亞倫面前好服事他,
“Walete kabila ya Lawi na uwaweke kwa Haruni kuhani ili wamsaidie
Nao lazima wafanye majukumu badala ya Haruni na jumuiya yote mbele ya hema ya kukutania. Lazima watumike hemani.
8 又要看守會幕的器具,並守所吩咐以色列人的,辦理帳幕的事。
Watayatunza mapambo ya hema ya kukutania, na watawatumikia makabila ya Israel kwa huduma ya hemani.
9 你要將利未人給亞倫和他的兒子,因為他們是從以色列人中選出來給他的。
Uwaweke Walawi kwa Haruni na watoto wake. Nimewatoa kikamilifu ili wamsaidie kuwatumikia watu wa Israel.
10 你要囑咐亞倫和他的兒子謹守自己祭司的職任。近前來的外人必被治死。」
Umchague Haruni na watoto wake kuwa makuhani, lakini mgeni yeyote atakayekaribia lazima auawe.”
BWANA alinena na Musa. akamwambia,
12 「我從以色列人中揀選了利未人,代替以色列人一切頭生的;利未人要歸我。
“Tazama, nimewachagua Walawi katika watu wa Israel. Nimefanya hivyo badala ya kuchukua mzaliwa wa kwanza wa kiume wa wana wa Israel. Hawa Walawi ni wangu.
13 因為凡頭生的是我的;我在埃及地擊殺一切頭生的那日就把以色列中一切頭生的,連人帶牲畜都分別為聖歸我;他們定要屬我。我是耶和華。」
Na hata wazaliwa wa kwanza ni mali yangu. Katika siku ambyo niliwavamia wazaliwa wote wa kwanza wa nchi ya Misri, Niliwatenga wazaliwa wa kwanza wa Israeli kwa ajili yangu, watu na wanyama pia. Ni mali yangu. Mimi ndimi BWANA.”
BWANA alinena na Musa katika nyika ya Sinai. Akasema,
15 「你要照利未人的宗族、家室數點他們。凡一個月以外的男子都要數點。」
“Wahesabu uzao wa Lawi katika kila familia, katika nyumba za koo zao. Hesabu kila mume kuanzia mwezi mmoja au zaidi.”
Musa aliwahesabu, kufuata maelekezo ya BWANA, kama alivyoamriwa kufanya.
Majina ya watoto waLawi yalikuwa Gerishoni, Kohathi, na Merari.
Ukoo uliotokana na watoto wa Gerishoni walikuwa ni Libni na Shimei.
19 哥轄的兒子,按着家室,是暗蘭、以斯哈、希伯倫、烏薛。
Ukoo uliotokana na watoto Kohathi walikuwa ni Amramu na, Izihari, Hebroni, na Uzieli.
20 米拉利的兒子,按着家室,是抹利、母示。這些按着宗族是利未人的家室。
Ukoo uliotokana na watoto wa Merari walikuwa ni Mahili na Mushi. Hizi ndizo koo za Walawi, zilizoorodheshwa ukoo kwa ukoo.
21 屬革順的,有立尼族、示每族。這是革順的二族。
Koo za Walibini na Washimei zilitokana na Wagerishoni. Hizi ndizo koo za Wagerishoni.
22 其中被數、從一個月以外所有的男子共有七千五百名。
Wanaume wote wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi walihesabiwa na kufikia idadi ya 7, 500.
Koo za Wagerishoni watapanga upande wa magharibi wa hema.
Eliasafu mwana wa Laeli ataongoza koo za uzao wa Wagerishoni.
25 革順的子孫在會幕中所要看守的,就是帳幕和罩棚,並罩棚的蓋與會幕的門簾,
Familia ya Gerishoni watalilinda hema la kukutania pamoja na hiyo masikani. Watalilinda hema, kifuniko chake, na lile pazia la lango la hema ya kukutania.
26 院子的帷子和門簾(院子是圍帳幕和壇的),並一切使用的繩子。
Wataulinda ua, lile pazia la kwenye lango—ua unaozunguka mahali patakatifu na madhabahu. Watazilinda kamba za hema ya kukutania na vyote vilivyomo.
27 屬哥轄的,有暗蘭族、以斯哈族、希伯倫族、烏薛族。這是哥轄的諸族。
Koo zifuatazo zinatokana na Kohathi: ukoo wa Waamrami, ukoo wa Waizihari ukoo wa Wahebroni, na ukoo wa Wauzieli. Koo hizi zinatokana na Wakohathi.
28 按所有男子的數目,從一個月以外看守聖所的,共有八千六百名。
Wanaume 8, 600 wenye umri wa mwezi mmoja au zaidi walihesabiwa ili kulinda vitu vya BWANA.
Familia ya uzao wa Kohathi watapanga upande wa kusini wa Hema.
Elizafani mwana wa Uzieli ndiye atakayeongoza ukoo wa Wakohathi.
31 他們所要看守的是約櫃、桌子、燈臺、兩座壇與聖所內使用的器皿,並簾子和一切使用之物。
Watalilinda sanduku, meza, vikalishio vya taa, madhabahu, vitu vitakatifu ambvyo hutumika katika huduma yao, pazia, na kazi zote zinazoambatana na hema.
32 祭司亞倫的兒子以利亞撒作利未人眾首領的領袖,要監察那些看守聖所的人。
Eliazari mwana wa Haruni kuhani atawaongoza wanaume wanaowaongoza Walawi. Atawasimamia wanaume wanaongoza eneo takatifu.
33 屬米拉利的,有抹利族、母示族。這是米拉利的二族。
Koo mbili zimetoka kwa Merari: Ukoo wa Mahili na ukoo wa Mushi. Koo hizi zimetokana na Merari,
34 他們被數的,按所有男子的數目,從一個月以外的,共有六千二百名。
Wanaume 6, 200 wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi walihesabiwa.
35 亞比亥的兒子蘇列作米拉利二宗族的首領。他們要在帳幕的北邊安營。
Zurieli mwana wa Abihaili ataongoza ukoo wa Merari. Hawa watapanga upande wa kaskazini mwa hema.
36 米拉利子孫的職分是看守帳幕的板、閂、柱子、帶卯的座,和帳幕一切所使用的器具,
Uzao wa Merari utatunza mbao za hema, mataruma, nguzo, makalishio, viifaa vya ujenzi na vitu vyote vinavyohusika,
na nguzo za ua zinazozunguka hema, makalishio, vigingi na kamba zake.
38 在帳幕前東邊,向日出之地安營的是摩西、亞倫,和亞倫的兒子。他們看守聖所,替以色列人守耶和華所吩咐的。近前來的外人必被治死。
Musa na Haruni na watoto wake watapanga upande wa mashariki wa masikani, mbele ya hema ya kukutania kuelekea mawio ya jua. Wao wataajibika na majukumu ya mahali patakatifu na majukumu ya wana wa Israeli. Mgeni atakayekaribia mahali patakatifu auawe.
39 凡被數的利未人,就是摩西、亞倫照耶和華吩咐所數的,按着家室,從一個月以外的男子,共有二萬二千名。
Musa na Haruni wakawahesabu wanaume wote wa ukoo wa Walawi walikuwa na umri wa mwezi mmoja na zaidi, kama vile BWANA alivyokuwa ameagiza. Walihesabu wanaume ishirini na mbili elfu.
40 耶和華對摩西說:「你要從以色列人中數點一個月以外、凡頭生的男子,把他們的名字記下。
BWANA alisema na Musa, “Wahesabu wanaume wote ambo ni wazaliwa wa kwanza wa Israeli ambao wana umri wa mwezi mmoja na zaidi. Orodhesha majina yao.
41 我是耶和華。你要揀選利未人歸我,代替以色列人所有頭生的,也取利未人的牲畜代替以色列所有頭生的牲畜。」
Unitwalie walawi kwa ajili yangu badala ya wazaliwa wa kwanza wa Israeli, Mimi ndimi BWANA. Na utwae wanyama wa Walawi badala ya wazaliwa wa kwanza wa wanyama wa uzao wa Israeli,”
42 摩西就照耶和華所吩咐的把以色列人頭生的都數點了。
Musa akawahesabu wazaliwa wa kwanza wote wa Israeli kama BWANA alivyomwagiza kufanya.
43 按人名的數目,從一個月以外、凡頭生的男子,共有二萬二千二百七十三名。
Aliwahesabu wazaliwa wote wa kwanza kwa mjina, wenye umri wa mwezi mmoja na zaidi. Alihesabu wanaume 22, 273.
Tena BWANA alinena na Musa. Akasema,
45 「你揀選利未人代替以色列人所有頭生的,也取利未人的牲畜代替以色列人的牲畜。利未人要歸我;我是耶和華。
“Watwae Walawi badala ya wazaliwa wote wa kwanza wa wana wa Israeli. Na utwae wanyama wa Walawi badala ya wanyama wa Waisreli wengine. Walawi ni mali yangu. Mimi ndimi BWANA.
46 以色列人中頭生的男子比利未人多二百七十三個,必當將他們贖出來。
Unikusanyie shekeli tano za wokovu kwa kila hao 273 za hao wazaliwa wa kwanza wa Israeli za hao wanaozidi idadi ya Walawi.
47 你要按人丁,照聖所的平,每人取贖銀五舍客勒(一舍客勒是二十季拉),
Utazitumia hizo shekeli tano kwa kipimo cha mahali patakatifu. Shekeli moja ni sawa na gera ishirini.
Utawalipa hizo shekeli za wokovu kwa Haruni na wanawe.”
Kwa hiyo Musa akakusanya shakeli za wokovu kutoka kwa wale waliozidi idadi ya wale waliookolewa na Walawi.
50 從以色列人頭生的所取之銀,按聖所的平,有一千三百六十五舍客勒。
Musa akakusanya zile fedha kutoka kwa hao wazaliwa wa kwanza wa wana wa Israeli. Alikusanya jumla ya shekeli 1, 365, zenye kipimo sawa na mahali patakatifu. Musa akamlipa Haruni na wanawe hizo shekeli za wokovu.
51 摩西照耶和華的話把這贖銀給亞倫和他的兒子,正如耶和華所吩咐的。
Musa akafanya kila kitu alichoagizwa na neno la BWANA kama BWANA alivyomwagiza.