< 民數記 25 >

1 以色列人住在什亭,百姓與摩押女子行起淫亂。
Israeli akakaa Shitimu, na wanaume wakaanza kufanya ukahaba na wanawake wa Moabu,
2 因為這女子叫百姓來,一同給她們的神獻祭,百姓就吃她們的祭物,跪拜她們的神。
kwa kuwa Wamoabu waliwakaribishsa kutoa sadaka kwa miungu yao. Kwa hiyo watu wakala na kuisujudia miungu ya Moabu.
3 以色列人與巴力‧毗珥連合,耶和華的怒氣就向以色列人發作。
Watu wa Israeli wakaungana kumwabudu Baali wa Peori, na hasira ya BWANA ikawaka dhidi ya Israeli.
4 耶和華吩咐摩西說:「將百姓中所有的族長在我面前對着日頭懸掛,使我向以色列人所發的怒氣可以消了。」
BWANA akamwambia Musa, “Waue viongozi wote wa watu na uwanyonge mbele yangu ili waonekane wakati wa mchana, ili kwamba hasira yangu kali iondoke kwa Israeli.”
5 於是摩西吩咐以色列的審判官說:「凡屬你們的人,有與巴力‧毗珥連合的,你們各人要把他們殺了。」
Kwa hiyo Musa akawaambia viongozi wa Israeli, “Kila mmoja wenu lazima awanyonge watu wake ambao wameshiriki kumwabudu Baali wa Peori.”
6 摩西和以色列全會眾正在會幕門前哭泣的時候,誰知,有以色列中的一個人,當他們眼前,帶着一個米甸女人到他弟兄那裏去。
Kisha mtu mmoja wa Israeli akaleta mwanamke mmoja aliyekuwa miongoni mwa familia yake. Hili lilitokea mbele ya macho ya Musa na watu wa Israeli, wakati walipokuwa wakilia mbele ya lango la hema ya kukutania.
7 祭司亞倫的孫子,以利亞撒的兒子非尼哈看見了,就從會中起來,手裏拿着槍,
Finehasi mwana wa Eliazari, mwana wa Haruni kuhani, alipoona hivyo, akainuka kutoka jamii ya watu akachukua mkuki mkononi mwake.
8 跟隨那以色列人進亭子裏去,便將以色列人和那女人由腹中刺透。這樣,在以色列人中瘟疫就止息了。
Akamfuata yule mwanaume Muisraeli hemani na kuwachoma kwa mkuki wote wawili kwenye miili yao, wote yule Muisraeli na yule mwanamke. Kwa hiyo ile tauni ambayo Mungu alikuwa ameituma kwa watu wa Israeli ikakoma.
9 那時遭瘟疫死的,有二萬四千人。
Idadi ya wale waliokufa kwa tauni walikuwa elfu ishirini na nne.
10 耶和華曉諭摩西說:
BWANA akanena na Musa, akasema,
11 「祭司亞倫的孫子,以利亞撒的兒子非尼哈,使我向以色列人所發的怒消了;因他在他們中間,以我的忌邪為心,使我不在忌邪中把他們除滅。
“Finehasi mwana wa Eliazari mwana wa Haruni, kuhani amaigeuza hasira yangu isiwe kwa wana wa Israeli kwa sababu alikuwa na wivu kati yao juu ya wivu wangu. Kwa hiyo sijawaangamiza watu wa Israeli kwa hasira yangu.
12 因此,你要說:『我將我平安的約賜給他。
Kwa hiyo waambie, 'BWANA anasema, “Tazama, Ninampa Finehasi agano la amani.
13 這約要給他和他的後裔,作為永遠當祭司職任的約;因他為上帝有忌邪的心,為以色列人贖罪。』」
Kwake na kwa wana wake baada yake, litakuwa agano la kudumu la ukuhani kwa sababu alikuwa na wivu juu yangu, Mungu wake. Amewapatanisha wana wa Israeli.
14 那與米甸女人一同被殺的以色列人,名叫心利,是撒路的兒子,是西緬一個宗族的首領。
Sasa yule Muisraeli aliyeuwawa pamoja na Yule mwanamke Mmidiani alikuwa Zimri mwana wa Salu, kiongozi wa familia ya uzao wa Simeoni.
15 那被殺的米甸女人,名叫哥斯比,是蘇珥的女兒;這蘇珥是米甸一個宗族的首領。
Jina la yule Mmidiani aliyeuwawa lilikuwa Cozibi binti wa Zuri, ambaye alikuwa mkuu wa familia wa kabila huko Midiani.
16 耶和華曉諭摩西說:
Kwa hiyo BWANA akanena na Musa na kusema,
17 「你要擾害米甸人,擊殺他們;
“Watendee Wamidiani kama maadui na uwaangamize, kwa kuwa waliwatendea kama maadui
18 因為他們用詭計擾害你們,在毗珥的事上和他們的姊妹、米甸首領的女兒哥斯比的事上,用這詭計誘惑了你們;這哥斯比,當瘟疫流行的日子,因毗珥的事被殺了。」
kwa kuwadanganya. Waliwaongoza katika uovu kwa swala la Peori na kwa swala la dada yao Cozibi, binti wa kiongozi wa Wamidiani, ambaye aliuawa siku ile ya tauni kwa swala la Peori.”

< 民數記 25 >