< 民數記 24 >
1 巴蘭見耶和華喜歡賜福與以色列,就不像前兩次去求法術,卻面向曠野。
Balaamu alipooa kuwa ilimpendeza BWANA kubariki Israeli, hakwenda, kama hapo awali, kwa kutumia uganga, badala yake akatazama jangwani.
2 巴蘭舉目,看見以色列人照着支派居住。上帝的靈就臨到他身上,
Akayainua macho yake na kumwona Isreli akiwa kwenye kambi, kila mmoja kwa kabila yake, na Roho wa Mungu akamjia.
3 他便題起詩歌說: 比珥的兒子巴蘭說, 眼目閉住的人說,
Akapokea huu unabii na kusema, “Balaamu mwana wa Beori anataka kusema, yeye ambaye macho yake yemefunuliwa sana.
4 得聽上帝的言語, 得見全能者的異象, 眼目睜開而仆倒的人說:
Huongea na kusikia maneno ya Mungu. Huona maono toka kwa Mwenyezi, ambaye mbele zake humwinamia na macho yake yakiwa yamefumbuliwa.
5 雅各啊,你的帳棚何等華美! 以色列啊,你的帳幕何其華麗!
Jinsi zilivyo nzuri hema zako, ewe Yakobo, mahali unapoishi, Israeli!
6 如接連的山谷, 如河旁的園子, 如耶和華所栽的沉香樹, 如水邊的香柏木。
Wamesambaa kama bonde, kama bustani zilizo pembezoni mwa mto, Kama miti ya mishubiri iliyopandwa na BWANA, ni kama mfano wa mielezi pembezoni mwa maji.
7 水要從他的桶裏流出; 種子要撒在多水之處。 他的王必超過亞甲; 他的國必要振興。
Maji yanatiririka katika ndoo zao, na mbegu zao zimemwagiwa maji vizuri. Mfalme wao atakuwa juu ya Agagi, na ufalme wao utaheshimiwa.
8 上帝領他出埃及; 他似乎有野牛之力。 他要吞吃敵國, 折斷他們的骨頭, 用箭射透他們。
Mungu anamtoa Misri, na nguvu kama za nyati. Atawameza mataifa wanaopigana nao. Ataivunja mifupa yao katika vipande vipande. atawapiga kwa mishale yake.
9 他蹲如公獅, 臥如母獅,誰敢惹他? 凡給你祝福的,願他蒙福; 凡咒詛你的,願他受咒詛。
Ananyatia kama simba mume, na kamaa simba jike. Ni nani atakayejaribu kumsumbua? Kila mmoja anayembariki na abarikiwe; na kila mmoja anayemlaani na alaaniwe.”
10 巴勒向巴蘭生氣,就拍起手來,對巴蘭說:「我召你來為我咒詛仇敵,不料,你這三次竟為他們祝福。
Hasira za Balaki zikawaka dhidi ya Balaamu naye akaipiga mikono yake kwa pamoja. Balaki akamwambia Balaamu, “Nilkuita ili uwalaani maadui zangu, Lakini tazama, umewabariki mara tatu.
11 如今你快回本地去吧!我想使你得大尊榮,耶和華卻阻止你不得尊榮。」
Kwa hiyo ondoka uende nyumbani uniache sasa hivi. Nilisema ningekupa zawadi kubwa sana, lakini BWANA amekuzuilia kupata zawadi.”
12 巴蘭對巴勒說:「我豈不是對你所差遣到我那裏的使者說:
Ndipo Balaamu alipomjibu Balaki, “Niliwaambia wale wajumbe ulionitumia,
13 『巴勒就是將他滿屋的金銀給我,我也不得越過耶和華的命,憑自己的心意行好行歹。耶和華說甚麼,我就要說甚麼』?」
'Hata kama Balaki atanipa ikulu yake ikiwa imejaa fedha na dhahabu, sitafanya zaidi ya maneno ya BWANA kwa lolote zuri au baya, au kwa chochote ambacho ningetaka kufanya. Ninaweza kusema kile tu ambacho BWANA ananiambia kusema,' Je, sikuwaambia haya?
14 「現在我要回本族去。你來,我告訴你這民日後要怎樣待你的民。」
Kwa hiyo sasa, tazama, nitarudi kwa watu wangu. Lakini kwanza nikuonye kile ambacho hawa watu watawafanyia watu wako katika siku zijazo.”
15 他就題起詩歌說: 比珥的兒子巴蘭說: 眼目閉住的人說,
Balaamu alianza unabii huu. Akisema, “Balaamu mwana wa Beori anasema, Mtu yule aliyefumbuliwa macho yake.
16 得聽上帝的言語, 明白至高者的意旨, 看見全能者的異象, 眼目睜開而仆倒的人說:
Huu ni unabii wa mtu alisikiaye neno la Mungu, aliye na maarifa toka kwake Yeye aliye juu, aliye na maono kutoka kwa Mwenyezi, Yeye ambaye humpigia magoti macho yakiwa yamefumbuliwa.
17 我看他卻不在現時; 我望他卻不在近日。 有星要出於雅各,有杖要興於以色列, 必打破摩押的四角,毀壞擾亂之子。
Ninamwona, lakini hayuko hapa sasa. Ninamtazama, lakini siyo karibu. Nyota itatokea katika Yakobo, na fimbp ya enzi itatokea katika Israeli. Naye atawapigapiga viongozi wa Moabu na kuwaharibu wa uzao wa Sethi
18 他必得以東為基業, 又得仇敵之地西珥為產業; 以色列必行事勇敢。
Ndipo Edomu atakapokuwa miliki ya Israeli, na Seiri pia itakuwa milki yao, maadui wa Israeli, ambao Israeli atawashinda kwa nguvu zake.
19 有一位出於雅各的,必掌大權; 他要除滅城中的餘民。
Kutoka kwa Yakobo atatoka mfalme ambaye utawala wake naye atawaangamiza waliosalia katika mji.”
20 巴蘭觀看亞瑪力,就題起詩歌說: 亞瑪力原為諸國之首, 但他終必沉淪。
Kisha Balaamu akamtazama Amaleki na akaanza kutoa unabii wake. Alisema, “Amaleki alikuwa mkuu katika mataifa, lakini mwisho wake utakuwa uharibifu.”
21 巴蘭觀看基尼人,就題起詩歌說: 你的住處本是堅固; 你的窩巢做在巖穴中。
Kisha Balaamu akawatazama Wakeni na akaanza kutoa unabii wake. Akasema, “Mahali unapoishi pana usalama, na viiota vyake viko kwenye miamba.
Lakini pamoja na hayo, Kaini ataharibiwa na Ashuru atakapowachukua mateka.”
23 巴蘭又題起詩歌說: 哀哉!上帝行這事,誰能得活?
Kisha Balaamu akanza unabii wake wa mwisho. Akasema, “Ole wake atakayesalia Mungu atakapoyafanya haya?
24 必有人乘船從基提界而來, 苦害亞述,苦害希伯; 他也必至沉淪。
Merikebu zitakuja toka pwani ya Kittimu; Zitaivamia Ashuru na kuiharibu Eberi, lakini wao pia wataishia kwenye uharibifu.”
Kisha Balaamu akainuka na kuondoka. Akarudi nyumbani kwake, na Balaki naye akaondoka.