< 民數記 10 >

1 耶和華曉諭摩西說:
BWANA alinena na Musa, akasema,
2 「你要用銀子做兩枝號,都要錘出來的,用以招聚會眾,並叫眾營起行。
“tengenza tarumbeta mbili za fedha. Uzitengeneze kwa kufua hizo fedha. Utazitumia hizo tarumbeta kwa kuwaita watu waje pamoja na kwa kuwaita watu wote wakati wa kuondoka kwenye kambi zao.
3 吹這號的時候,全會眾要到你那裏,聚集在會幕門口。
Makuhani watapiga tarumbeta kwa ajili ya kuwaita watu wote mbele yako kwenye lango la hema ya kukutania.
4 若單吹一枝,眾首領,就是以色列軍中的統領,要聚集到你那裏。
Kama makuhani watapiga tarumbeta moja tu, basi viongozi, vichwa koo za Israeli ndipo watakapokutana kwako.
5 吹出大聲的時候,東邊安的營都要起行。
Utakapopiga tarumbeta ya sauti kuu, ile kambi ya upande wa mashariki itaanza kusafiri.
6 二次吹出大聲的時候,南邊安的營都要起行。他們將起行,必吹出大聲。
Nawe utakapopiga tarumeta kwa sauti kuu mara ya pili, ile kambi ya upande wa kusini wataanza kusafiri. Watapiga tarumbeta kwa sauti kuu ili kuanza safari yao.
7 但招聚會眾的時候,你們要吹號,卻不要吹出大聲。
Watu wote watakapokutana pamoja, piga hizo tarumbeta lakini si kwa sauti kuu.
8 亞倫子孫作祭司的要吹這號;這要作你們世世代代永遠的定例。
Wana wa Haruni, makuhani, watapiga hizo tarumbeta. Huu ndio utakaokuwa utaratibu wa watu wako kwa vizazi vyote.
9 你們在自己的地,與欺壓你們的敵人打仗,就要用號吹出大聲,便在耶和華-你們的上帝面前得蒙紀念,也蒙拯救脫離仇敵。
Nanyi mtakapoenda vitani katika ardhi yenu dhidi ya maadui wenu wanaowakandamiza, ndipo mtakapotoa ishara ya sauti ya tarumbeta. Mimi, BWANA Mungu wako nitawaita kuwakumbuka na kuwaokoa kutoka kwa maadui wenu.
10 在你們快樂的日子和節期,並月朔,獻燔祭和平安祭,也要吹號,這都要在你們的上帝面前作為紀念。我是耶和華-你們的上帝。」
Pia, wakati wa kusherehekea, sikukuu zenu za kawaida na katika miandamo ya miezi, mtapiga tarumbeta zenu kwa heshima ya sadaka zenu za kuteketezwa na kwa sadaka zenu za amani. Huu utakuwa ukumbusho wenu kwangu, Mungu wenu. Mimi ndimi BWANA Mungu wenu.”
11 第二年二月二十日,雲彩從法櫃的帳幕收上去。
Katika siku ya ishrini, mwezi wa pili, mwaka wa pili, Lile wingu liliinuliwa toka masikani ya amri za maagano.
12 以色列人就按站往前行,離開西奈的曠野,雲彩停住在巴蘭的曠野。
Wana wa Israeli wakaendelea na safari yao toka jangwa la Sinai. Lile wingu likasimama kwenye jangwa la Parani.
13 這是他們照耶和華藉摩西所吩咐的,初次往前行。
Walifanya safari yao ya kwanza, kufuatia amri ya BWANA iliyotolewa kupitia kwa Musa.
14 按着軍隊首先往前行的是猶大營的纛。統領軍隊的是亞米拿達的兒子拿順。
Kambi ya mahali pa uzao wa Yuda iliondoka ya kanza, wakiondoa majeshi yao binafsi. Nashoni mwana wa Aminadabu ndiye aliyeongoza jeshi la Yuda.
15 統領以薩迦支派軍隊的是蘇押的兒子拿坦業。
Nethaneli mwana wa Zuari aliongoza jeshi la kabila la uzao wa Isakari.
16 統領西布倫支派軍隊的是希倫的兒子以利押。
Eliabu mwana wa Heloni aliongoza jeshi la kabila la Zabuloni.
17 帳幕拆卸,革順的子孫和米拉利的子孫就抬着帳幕先往前行。
Uzao wa Gerishoni na Merari, ambao walitunza masikani, na kuanza kusafiri.
18 按着軍隊往前行的是呂便營的纛。統領軍隊的是示丟珥的兒子以利蓿。
Baadaye Walifuata jeshi la mahali pa kambi ya Reubeni walianza safari yao. Elizuri mwana wa Shedeuri alliongoza jeshi la Reubebni.
19 統領西緬支派軍隊的是蘇利沙代的兒子示路蔑。
Shelumieli mwana wa Zurishadai aliliongoza jeshi la kabila la uzao wa Simeoni.
20 統領迦得支派軍隊的是丟珥的兒子以利雅薩。
Eliasafu mwana Deuli aliliongoza jeshi la kabila la uzao wa Gadi.
21 哥轄人抬着聖物先往前行。他們未到以前,抬帳幕的已經把帳幕支好。
Kabila la Kohathi nalo lilianza safari. Wao walibebba vyombo vya mahali patakatifu. Wengine waliisimamisha masikani kabla ya Wakohathi kufika kambi inayofuata.
22 按着軍隊往前行的是以法蓮營的纛,統領軍隊的是亞米忽的兒子以利沙瑪。
Majeshi ya kabila la uzao wa Efraimu ndio waliofuata. Elishama mwana wa Amihudi ndiye aliyeongoza jeshi la Efraimu.
23 統領瑪拿西支派軍隊的是比大蓿的兒子迦瑪列。
Gamalieli mwana wa Pedazuri aliongoza jeshi la uzao wa Manase.
24 統領便雅憫支派軍隊的是基多尼的兒子亞比但。
Abidani mwana wa Gidioni aliongoza jeshi la uzao wa kabila la Benjamini.
25 在諸營末後的是但營的纛,按着軍隊往前行。統領軍隊的是亞米沙代的兒子亞希以謝。
Lile jeshi lililoweka kambi mahali pa bango la uzao wa Dani lilikuwa la mwisho kuondoka. Ahizeri mwana wa Amishadai ndiye aliyeongoza jeshi la Dani.
26 統領亞設支派軍隊的是俄蘭的兒子帕結。
Pagieli mwana wa Okirani aliongoza jeshi la wana wa uzao wa Asheri.
27 統領拿弗他利支派軍隊的是以南的兒子亞希拉。
Ahira mwana wa Enani aliongoza jeshi la uzao wa kabila ya Naftali.
28 以色列人按着軍隊往前行,就是這樣。
Hivi ndivyo majeshi ya wana wa Israeli yalivyosafiri.
29 摩西對他岳父-米甸人流珥的兒子何巴-說:「我們要行路,往耶和華所應許之地去;他曾說:『我要將這地賜給你們。』現在求你和我們同去,我們必厚待你,因為耶和華指着以色列人已經應許給好處。」
Musa alinena na Hobibu mwana wa Reueli wa Kabila la Midiani. Reueli alikuwa baba mke wa Musa. Musa akanena na Hobibu akasema, “Tunasafiri kuelekea mahali ambapo BWANA ametuahidi. BWANA alisema kuwa, “Nitawapeni ninyi hilo eneo, 'Njoni pamoja nasi na tutawatendea mema. BWANA ameahidi kuwafanyia mema Waisraeli.”
30 何巴回答說:「我不去;我要回本地本族那裏去。」
Lakini Hobibu akmwambia Musa, “Sitaambatana nanyi.”
31 摩西說:「求你不要離開我們;因為你知道我們要在曠野安營,你可以當作我們的眼目。
Naye Musa akamjibu, “Tafadhali msituache. Mnajua jinsi ilivyo kuweka kambi jangwani. Tunaomba mtujali.
32 你若和我們同去,將來耶和華有甚麼好處待我們,我們也必以甚麼好處待你。」
Kama mtaambatana nasi tutawatendea mema sawa na jinsi BWANA anavyotutendea.”
33 以色列人離開耶和華的山,往前行了三天的路程;耶和華的約櫃在前頭行了三天的路程,為他們尋找安歇的地方。
Walisafiri kutoka mlima wa BWANA kwa siku tatu. Sanduku la agano la BWANA liliwatangulia kwa siku tatu ili kupata mahali pa kupumzika.
34 他們拔營往前行,日間有耶和華的雲彩在他們以上。
Wingu la BWANA lilikuwa juu yao muda wote wa mchana walipokuwa safarini.
35 約櫃往前行的時候,摩西就說:「耶和華啊,求你興起!願你的仇敵四散!願恨你的人從你面前逃跑!」
Kila hilo sanduku liliposafiri kwenda mbele, Musa alisema, “Inuka BWANA, Uwatawanye maadui wako. Uwafanye wale wanaokuchukia kukukimbia.”
36 約櫃停住的時候,他就說:「耶和華啊,求你回到以色列的千萬人中!」
Na kila lile sanduku liliposimama, Musa alisema, “BWANA uwarudie, hawa Waisraeli makumi elfu.”

< 民數記 10 >