< 那鴻書 3 >

1 禍哉!這流人血的城, 充滿謊詐和強暴- 搶奪的事總不止息。
Ole kwa mji uliojaa damu! Wote umejaa uongo na mali za wizi; wahanga wapo kwake daima.
2 鞭聲響亮,車輪轟轟, 馬匹踢跳,車輛奔騰,
Lakini sasa kunasauti ya mijeledi na sauti za kugongesha matairi, farasi wakicheza, na magari ya vita yanaruka ruka.
3 馬兵爭先,刀劍發光, 槍矛閃爍,被殺的甚多, 屍首成了大堆, 屍骸無數,人碰着而跌倒,
Kuna wapanda farasi wanashambulia, Upanga unang'ara, mikuki inametameta, marundo ya maiti, mafungu makubwa ya miili; hakuna ukomo wa miili, washambuliaji wanajikwaa juu yake.
4 都因那美貌的妓女多有淫行, 慣行邪術,藉淫行誘惑列國, 用邪術誘惑多族。
Hii inatokea kwa sababu ya matendo ya tamaa ya kahaba mzuri, mzoefu wa uchawi, mwenye kuuza taifa kwa umalaya wake, na watu kwa njia ya matendo yake ya kichawi.
5 萬軍之耶和華說:我與你為敵; 我必揭起你的衣襟,蒙在你臉上, 使列國看見你的赤體, 使列邦觀看你的醜陋。
“Tazama, mimi nipo kinyume na wewe- hili ni neno la Yehova wa majeshi- sketi yako nitaiinua juu ya uso wako na kuzionyesha sehemu zako za siri kwa mataifa, aibu yako kwa falme.
6 我必將可憎污穢之物拋在你身上, 辱沒你,為眾目所觀。
Nitarusha uchafu wa kuchukiza na kukufanya uwe mbaya sana; nitakufanya uwe mtu wa kutazamwa na kila mmoja.
7 凡看見你的,都必逃跑離開你, 說:尼尼微荒涼了!有誰為你悲傷呢? 我何處尋得安慰你的人呢?
Itakuwa kwamba kila mmoja anayekutazama atakukimbia na kusema, “Ninawi ameharibika; ni nani ataomboleza kwa ajili yake?' Ni wapi nitampata mtu anayeweza kukufariji?”
8 你豈比挪亞們強呢? 挪亞們坐落在眾河之間,周圍有水; 海作她的濠溝, 又作她的城牆。
Ninawi, je wewe ni bora kuliko Noamoni, uliojengwa juu ya Mto Naili, uliokuwa umezungukwa na maji, ambao ulinzi wake ilikuwa bahari, ambao ukuta wake ilikuwa bahari yenyewe?
9 古實和埃及是她無窮的力量; 弗人和路比族是她的幫手。
Ethiopia na Misri zilikuwa nguvu zake, na mwisho wake haukuwepo; Putu na Libya walikuwa rafiki zake.
10 但她被遷移,被擄去; 她的嬰孩在各市口上也被摔死。 人為她的尊貴人拈鬮; 她所有的大人都被鍊子鎖着。
Lakini Noamoni alichukuliwa; alikwenda kwenye mateka; watoto wake wadogo walivunjwa vipande vipande katika kila makao makuu ya mtaa; adui zake walipiga kura kwa watu wake wenye heshima na wakuu wake wote walifungwa minyororo.
11 你也必喝醉,必被埋藏, 並因仇敵的緣故尋求避難所。
Wewe pia utalewa; utajaribu kujificha, na utatafuta makimbilio kutoka kwa adui yako.
12 你一切保障必像無花果樹上初熟的無花果, 若一搖撼就落在想吃之人的口中。
Ngome zako zote zitakuwa kama mitini yenye tini zilizoiva mapema: kama zikitikiswa, zitaangukia kwenye kimywa cha mlaji.
13 你地上的人民如同婦女; 你國中的關口向仇敵敞開; 你的門閂被火焚燒。
Tazama, watu miongoni mwenu ni wanawake; malango ya nchi yako yamefunguliwa sana kwa ajili ya adui zako; moto umeharibu bawaba zake.
14 你要打水預備受困; 要堅固你的保障, 踹土和泥,修補磚窯。
Nenda ukachote maji kwenye boma iliyozingirwa; ziimarishe ngome zako; nenda kwenye udongo na kandamiza matope; finyanga kwa ajili ya matofali.
15 在那裏,火必燒滅你; 刀必殺戮你, 吞滅你如同蝻子。 任你加增人數多如蝻子, 多如蝗蟲吧!
Moto utakuteketeza pale, na upanga utakuangamiza. Utateketezwa kama nzige wachanga wanavyoteketeza kila kitu. Ninyi wenyewe mjitengeneze kuwa wengi kama nzige wachanga, na wengi kama nzinge waliopevuka.
16 你增添商賈,多過天上的星; 蝻子吃盡而去。
Umezidisha wafanyabiashara wako zaidi kuliko nyota mbinguni; lakini wapo kama tunutu: wanapora nchi na kisha kuruka kwenda mbali.
17 你的首領多如蝗蟲; 你的軍長彷彿成群的螞蚱, 天涼的時候齊落在籬笆上, 日頭一出便都飛去, 人不知道落在何處。
Wafalme wenu wapo wengi kama zinge, na wakuu wenu wa majeshi ni kama kundi la wadudu wenye kuweka kambi katika ukuta wakati wa baridi. Lakini jua linapowaka wanaruka kwenda mbali ambako hakuna anayepajua.
18 亞述王啊,你的牧人睡覺; 你的貴冑安歇; 你的人民散在山間,無人招聚。
Mfalme wa Ashuru, wachungaji wako wamelala; watawala wako wamejilaza chini kupumzika. Watu wako wametawanyika juu ya milima, na hakuna hata mmoja wa kuwakusanya.
19 你的損傷無法醫治; 你的傷痕極其重大。 凡聽你信息的必都因此向你拍掌。 你所行的惡誰沒有時常遭遇呢?
Hakuna uponyaji unaowezekana kwa ajili ya vidonda vyako. Vidonda vyako ni vikubwa. Wanaosikia habari juu yako watapiga makofi kwa furaha juu yako. Ni nani aliyejiepusha kwa uovu wako wa daima?

< 那鴻書 3 >