< 彌迦書 6 >
1 以色列人哪,當聽耶和華的話! 要起來向山嶺爭辯, 使岡陵聽你的話。
Sasa sikilizeni kile ambacho Yahwe asemacho, “Inuka na ueleze kesi yako mbele ya milima; acha milima isikie sauti yako.
2 山嶺和地永久的根基啊, 要聽耶和華爭辯的話! 因為耶和華要與他的百姓爭辯, 與以色列爭論。
Sikilizeni madai ya Yahwe, enyi milima, na ninyi misingi mivumilivu ya dunia. Kwa kuwa Yahwe anavumilia pamoja na watu wake, na atapigana katika mahakama juu ya Israeli.”
3 我的百姓啊,我向你做了甚麼呢? 我在甚麼事上使你厭煩? 你可以對我證明。
Watu wangu, nimefanya nini kwenu? nimewachosha mara ngapi? shuhudieni dhidi yangu!
4 我曾將你從埃及地領出來, 從作奴僕之家救贖你; 我也差遣摩西、亞倫,和米利暗在你前面行。
Kwa kuwa niliwaleta kutoka nchi ya Msiri na kuwaokoa kutoka kwenye nyumba ya utumwa. Nawatuma Musa, Aruni, na Mariamu kwako.
5 我的百姓啊,你們當追念摩押王巴勒所設的謀 和比珥的兒子巴蘭回答他的話, 並你們從什亭到吉甲所遇見的事, 好使你們知道耶和華公義的作為。
Watu wangu, kumbukeni ambavyo Balaki mfalme wa Moabu alivyotunga, na vile ambavyo Balamu mwana wa Beori alivyomjibu kama ulipokuwa ukienda kutoka kwa Gilgali, hivyo mnaweza kujua matendo ya haki ya Yahwe.”
6 我朝見耶和華, 在至高上帝面前跪拜,當獻上甚麼呢? 豈可獻一歲的牛犢為燔祭嗎?
Je nilete nini kwa Yahwe, ninapoenda kumwinamia Mungu aliye juu? Je ninaweza kuja kwake na sadaka za kuteketeza, pamoja na ndama wenye mwaka mmoja?
7 耶和華豈喜悅千千的公羊, 或是萬萬的油河嗎? 我豈可為自己的罪過獻我的長子嗎? 為心中的罪惡獻我身所生的嗎?
Je Yahwe atapendezwa na maelfu ya kondoo waume, au na elfu kumi za mito ya mafuta? Je nimtoe mzaliwa wangu wa kwanza kwa ajili ya kosa langu, tunda la mwili wangu kwa ajili ya dhambi yangu mwenyewe?
8 世人哪,耶和華已指示你何為善。 他向你所要的是甚麼呢? 只要你行公義,好憐憫, 存謙卑的心,與你的上帝同行。
Amekwambia, mtu, kile kilicho bora, na kile ambacho Yahwe atakacho kutoka kwako: Kutenda haki, kupenda ukarimu, na kutembea kwa unyenyekevu pamoja na Mungu wako.
9 耶和華向這城呼叫, 智慧人必敬畏他的名。 你們當聽是誰派定刑杖的懲罰。
Sauti ya Yahwe inatangaza kwenye mji-hata sasa hekima hukukiri jina lako: “Kaa tayari kwa ajili ya fimbo, na kwa yule aliyeiweka.
Kuna utajiri katika nyumba za waovu, na kipimo cha uongo hilo ni chukizo mno.
11 我若用不公道的天平和囊中詭詐的法碼, 豈可算為清潔呢?
Ningeweza kumfikira mtu kuwa hana hatia kama anatumia kipimo cha ulaghai, pamoja na mfuko wa kipimo wa udanganyifu?
12 城裏的富戶滿行強暴; 其中的居民也說謊言, 口中的舌頭是詭詐的。
Matajiri wamejaa uharibifu, makazi yao yamesema uongo, na ulimi wao katika midomo yao unaudanganyifu.
13 因此,我擊打你, 使你的傷痕甚重, 使你因你的罪惡荒涼。
Kwa hiyo nimekupiga kwa pigo linaloumiza, nimekufanya gofu kwa sababu ya dhambi zako.
14 你要吃,卻吃不飽; 你的虛弱必顯在你中間。 你必挪去,卻不得救護; 所救護的,我必交給刀劍。
Utakula lakini hutatosheka; utupu wako utabakia ndani yako. Utatunza mizigo mbali lakini hutahifadhi, na kile unachokihifadhi nitakitoa kwa upanga.
15 你必撒種,卻不得收割; 踹橄欖,卻不得油抹身; 踹葡萄,卻不得酒喝。
Utapanda lakini huatavuna; utazikusanya zaituni lakini hutajipaka mafuta; utasindika zabibu lakini hutakunywa divai.
16 因為你守暗利的惡規, 行亞哈家一切所行的, 順從他們的計謀; 因此,我必使你荒涼, 使你的居民令人嗤笑, 你們也必擔當我民的羞辱。
Kanuni zilizotengenezwa na Omri zimetunzwa, na matendo yote ya nyumba ya Ahabu. Mnatembea kwa ushauri wao. Hivyo nitakufanya wewe, mji, gofu, na makazi yako jambo la zomeo, na matabeba dharau kama watu wangu.”