< 馬太福音 5 >

1 耶穌看見這許多的人,就上了山,既已坐下,門徒到他跟前來,
Yesu alipo uona umati, akaondoka na kuelekea Mlimani. Alipokuwa ameketi chini, wanafunzi wake wakaja kwake.
2 他就開口教訓他們,說:
Akafunua kinywa chake na akawafundisha, akisema,
3 虛心的人有福了! 因為天國是他們的。
“Heri walio maskini wa roho maana ufalme wa mbinguni ni wao.
4 哀慟的人有福了! 因為他們必得安慰。
Heri walio na huzuni, maana watafarijiwa.
5 溫柔的人有福了! 因為他們必承受地土。
Heri wenye upole, maana watairithi nchi.
6 飢渴慕義的人有福了! 因為他們必得飽足。
Heri wenye njaa na kiu ya haki, maana hao watashibishwa.
7 憐恤人的人有福了! 因為他們必蒙憐恤。
Heri wenye rehema maana hao watapata Rehema.
8 清心的人有福了! 因為他們必得見上帝。
Heri wenye moyo safi maana watamwona Mungu.
9 使人和睦的人有福了! 因為他們必稱為上帝的兒子。
Heri wapatanishi, maana hao wataitwa wana wa Mungu.
10 為義受逼迫的人有福了! 因為天國是他們的。
Heri wale wanaoteswa kwa ajili ya haki, maana ufalme wa mbinguni ni wao.
11 「人若因我辱罵你們,逼迫你們,捏造各樣壞話毀謗你們,你們就有福了!
Heri ninyi ambao watu watawatukana na kuwatesa, au kusema kila aina ya ubaya dhidi yenu kwa uongo kwa ajili yangu.
12 應當歡喜快樂,因為你們在天上的賞賜是大的。在你們以前的先知,人也是這樣逼迫他們。」
Furahini na kushangilia, maana thawabu yenu ni kubwa juu mbinguni. Kwa kuwa hivi ndivyo watu walivyo watesa manabii walioishi kabla yenu.
13 「你們是世上的鹽。鹽若失了味,怎能叫它再鹹呢?以後無用,不過丟在外面,被人踐踏了。
Ninyi ni chumvi ya dunia. Lakini kama chumvi imepoteza ladha yake, itawezaje kufanyika chumvi halisi tena? Kamwe haiwezi kuwa nzuri kwa kitu kingine chochote tena, isipokuwa ni kutupwa nje na kukanyagwa na miguu ya watu.
14 你們是世上的光。城造在山上是不能隱藏的。
Ninyi ni nuru ya ulimwengu. Mji uliojegwa juu ya mlima haufichiki.
15 人點燈,不放在斗底下,是放在燈臺上,就照亮一家的人。
Wala watu hawawashi taa na kuweka chini ya kikapu, bali kwenye kinara, nayo yawaangaza wote walio ndani ya nyumba.
16 你們的光也當這樣照在人前,叫他們看見你們的好行為,便將榮耀歸給你們在天上的父。」
Acha nuru yenu iangaze mbele za watu kwa namna ambayo kwamba, wayaone matendo yenu mema na kumtukuza Baba yenu aliye mbinguni.
17 「莫想我來要廢掉律法和先知。我來不是要廢掉,乃是要成全。
Msifikiri nimekuja kuiharibu sheria wala manabii. Sijaja kuharibu lakini kutimiza.
18 我實在告訴你們,就是到天地都廢去了,律法的一點一畫也不能廢去,都要成全。
Kwa kweli nawaambia kwamba mpaka mbingu na dunia zote zipite hapana yodi moja wala nukta moja ya sheria itaondoshwa katika sheria hadi hapo kila kitu kitakapokuwa kimekwisha timizwa.
19 所以,無論何人廢掉這誡命中最小的一條,又教訓人這樣做,他在天國要稱為最小的。但無論何人遵行這誡命,又教訓人遵行,他在天國要稱為大的。
Hivyo yeyote avunjaye amri ndogo mojawapo ya amri hizi na kuwafundisha wengine kufanya hivyo ataitwa mdogo katika ufalme wa mbinguni. Lakini yeyote azishikaye na kuzifundisha ataitwa mkubwa katika ufalme wa mbinguni.
20 我告訴你們,你們的義若不勝於文士和法利賽人的義,斷不能進天國。」
Kwa maana nawaambia haki yenu isipozidi haki ya waandishi na Mafarisayo, kwa vyovyote vile hamtaingia katika ufalme wa mbinguni.
21 「你們聽見有吩咐古人的話,說:『不可殺人』;又說:『凡殺人的難免受審判。』
Mmesikia ilinenwa zamani kuwa, “usiue” na 'yeyote auaye yuko katika hatari ya hukumu.'
22 只是我告訴你們,凡向弟兄動怒的,難免受審判;凡罵弟兄是拉加的,難免公會的審判;凡罵弟兄是魔利的,難免地獄的火。 (Geenna g1067)
Lakini nawaambia yeyote amchukiaye ndugu yake atakuwa katika hatari ya hukumu. Na yeyote amwambiaye ndugu yake kuwa, 'Wewe ni mtu usiyefaa!' atakuwa katika hatari ya baraza. Na yeyote asemaye, 'Wewe mjinga!' atakuwa katika hatari ya moto wa jehanamu. (Geenna g1067)
23 所以,你在祭壇上獻禮物的時候,若想起弟兄向你懷怨,
Hivyo kama unatoa sadaka yako katika madhabahu na unakumbuka kuwa ndugu yako ana jambo lolote dhidi yako,
24 就把禮物留在壇前,先去同弟兄和好,然後來獻禮物。
iache sadaka mbele ya madhabahu, kisha shika njia yako. Kapatane kwanza na ndugu yako, na kisha uje kuitoa sadaka yako.
25 你同告你的對頭還在路上,就趕緊與他和息,恐怕他把你送給審判官,審判官交付衙役,你就下在監裏了。
Patana na mshitaki wako upesi, ukiwa pamoja naye njiani kuelekea mahakamani, vinginevyo mshtaki wako anaweza kukuacha mikononi mwa hakimu, na hakimu akuache mikononi mwa askari, nawe utatupwa gerezani.
26 我實在告訴你,若有一文錢沒有還清,你斷不能從那裏出來。」
Amini nawaambieni, kamwe hutawekwa huru hadi umelipa senti ya mwisho ya pesa unayodaiwa.
27 「你們聽見有話說:『不可姦淫。』
Mmesikia imenenwa kuwa, 'Usizini.'
28 只是我告訴你們,凡看見婦女就動淫念的,這人心裏已經與她犯姦淫了。
Lakini nawaambieni yeyote amtazamaye mwanamke kwa kumtamani amekwisha kuzini naye moyoni mwake.
29 若是你的右眼叫你跌倒,就剜出來丟掉,寧可失去百體中的一體,不叫全身丟在地獄裏。 (Geenna g1067)
Na kama jicho lako la kulia linakusababisha kujikwaa, ling'oe na ulitupe mbali nawe. Kwa kuwa ni afadhali kiungo kimoja katika mwili wako kiharibike kuliko mwili mzima kutupwa jehanamu. (Geenna g1067)
30 若是右手叫你跌倒,就砍下來丟掉,寧可失去百體中的一體,不叫全身下入地獄。」 (Geenna g1067)
Na kama mkono wako wa kuume unakusababisha kujikwaa, ukate kisha uutupilie mbali nawe. Maana ni afadhali kiungo kimoja katika mwili wako kiharibike kuliko mwili mzima kutupwa jehanamu. (Geenna g1067)
31 「又有話說:『人若休妻,就當給她休書。』
Imenenwa pia, yeyote amfukuzaye mkewe, na ampe hati ya talaka.'
32 只是我告訴你們,凡休妻的,若不是為淫亂的緣故,就是叫她作淫婦了;人若娶這被休的婦人,也是犯姦淫了。」
Lakini mimi nawaambia, yeyote anaye mwacha mke wake, isipokuwa kwa kwa sababu ya zinaa, amfanya kuwa mzinzi. Na yeyote amuoaye baada ya kupewa talaka afanya uzinzi.
33 「你們又聽見有吩咐古人的話,說:『不可背誓,所起的誓總要向主謹守。』
Tena, mmesikia ilinenwa kwa wale wa zamani, 'Msiape kwa uongo, bali pelekeni viapo vyenu kwa Bwana.'
34 只是我告訴你們,甚麼誓都不可起。不可指着天起誓,因為天是上帝的座位;
Lakini nawaambia, msiape hata kidogo, ama kwa mbingu, kwa sababu ni enzi ya Mungu;
35 不可指着地起誓,因為地是他的腳凳;也不可指着耶路撒冷起誓,因為耶路撒冷是大君的京城;
wala kwa dunia, maana ni mahali pa kuweka kiti cha kukanyagia nyayo zake, ama kwa Jerusalemu, maana ni mji wa mfalme mkuu.
36 又不可指着你的頭起誓,因為你不能使一根頭髮變黑變白了。
Wala usiape kwa kichwa chako, maana huwezi kufanya unywele mmoja kuwa mweupe au mweusi.
37 你們的話,是,就說是;不是,就說不是;若再多說就是出於那惡者 。」
Bali maneno yenu yawe, 'Ndiyo, ndiyo, Hapana, hapana.' Kwa kuwa yazidiyo hayo yatoka kwa yule mwovu.
38 「你們聽見有話說:『以眼還眼,以牙還牙。』
Mmesikia imenenwa kuwa, 'Jicho kwa jicho, na jino kwa jino.'
39 只是我告訴你們,不要與惡人作對。有人打你的右臉,連左臉也轉過來由他打;
Lakini mimi namwambia, Msishindane na mtu mwovu; lakini mtu akikupiga shavu la kulia mgeuzie na jingine pia.
40 有人想要告你,要拿你的裏衣,連外衣也由他拿去;
Na kama yeyote anatamani kwenda na wewe mahakamani na akakunyang'anya kanzu yako, mwachie na joho lako pia.
41 有人強逼你走一里路,你就同他走二里;
Na yeyote akulazimishaye kwenda naye maili moja, nenda naye maili mbili.
42 有求你的,就給他;有向你借貸的,不可推辭。」
Kwa yeyote akuombaye mpatie, na usimwepuke yeyote anayehitaji kukukopa.
43 「你們聽見有話說:『當愛你的鄰舍,恨你的仇敵。』
Mmesikia imenenwa, 'Umpende jirani yako, na umchukie adui yako.'
44 只是我告訴你們,要愛你們的仇敵,為那逼迫你們的禱告。
Lakini nawaambia, wapendeni adui zenu, waombeeni wanao waudhi,
45 這樣就可以作你們天父的兒子;因為他叫日頭照好人,也照歹人;降雨給義人,也給不義的人。
Ili kwamba muwe watoto wa baba yenu aliye mbinguni. Kwa kuwa anafanya jua liwaangazie wabaya na wema, na anawanyeshea mvua waovu na wema.
46 你們若單愛那愛你們的人,有甚麼賞賜呢?就是稅吏不也是這樣行嗎?
Kama mkiwapenda wanaowapenda ninyi, mwapata thawabu gani? Kwani watoza ushuru hawafanyi hivyo?
47 你們若單請你弟兄的安,比人有甚麼長處呢?就是外邦人不也是這樣行嗎?
Na kama mkiwasalimia ndugu zenu tu mwapata nini zaidi ya wengine? Je!, Watu wa mataifa hawafanyi vivyo hivyo?
48 所以,你們要完全,像你們的天父完全一樣。」
Kwa hiyo yawapasa kuwa wakamilifu, kama Baba yenu wa mbinguni alivyo mkamilifu.

< 馬太福音 5 >