< 利未記 26 >

1 「你們不可做甚麼虛無的神像,不可立雕刻的偶像或是柱像,也不可在你們的地上安甚麼鏨成的石像,向它跪拜,因為我是耶和華-你們的上帝。
Msijitengenezee sanamu, wala msisimamishe kinyago cha kuchonga au nguzo ya jiwe ya kuabudia, na msisimamisha sura ya jiwe la kuchonga katika nchi yenu mtayoiinamia, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
2 你們要守我的安息日,敬我的聖所。我是耶和華。
Ni lazima muitunze Sabato Yangu na kupaheshimu patakatifu pangu. Mimi ndimi Yahweh.
3 「你們若遵行我的律例,謹守我的誡命,
Iwapo mtatembea katika sheria zangu na kuzishika amri zangu na kuzitii,
4 我就給你們降下時雨,叫地生出土產,田野的樹木結果子。
Nami nitawapa ninyi mvua katika majira yake; nayo nchi itatoa mazao yake, na miti ya shambani itatoa matunda yake.
5 你們打糧食要打到摘葡萄的時候,摘葡萄要摘到撒種的時候;並且要吃得飽足,在你們的地上安然居住。
Upuraji wenu utaendelea hata wakati wa mavuno ya zabibu, na mavuno ya zabibu yataendelea mpaka majira ya kupada mbegu. Nanyi mtakula mkate na kushiba na kuishi salama mahali mtakapofanya mji wenu katika nchi.
6 我要賜平安在你們的地上;你們躺臥,無人驚嚇。我要叫惡獸從你們的地上熄滅;刀劍也必不經過你們的地。
Nitawapa amani; mtalala bila ya kitu chochote kuwatia hofu. Nitawaondolea mbali wanyama waliohatari katika nchi, na upanga hautapita katika nchi yenu.
7 你們要追趕仇敵,他們必倒在你們刀下。
Mtawafukuza adui zenu, nao wataanguka mbele yenu kwa upanga.
8 你們五個人要追趕一百人,一百人要追趕一萬人;仇敵必倒在你們刀下。
Watu wenu watano watafukuza adui mia moja, na watu wenu mia moja watafukuza adui elfu kumi; adui zenu wataanguka mbele yenu kwa upanga.
9 我要眷顧你們,使你們生養眾多,也要與你們堅定所立的約。
Nitawatazama kwa upendeleo na kuwafanya nyinyi mzae na kuwazidisha nyinyi.
10 你們要吃陳糧,又因新糧挪開陳糧。
Mtakula chakula kilichotunzwa ghalani kwa muda mrefu. Mtayaondoa mazao yaliyohifadhiwa ghalani kwa sababu mtahitaji ghala kwa ajili ya mavuno mapya.
11 我要在你們中間立我的帳幕;我的心也不厭惡你們。
Nitaliweka hema langu katikati yenu, nami stachukizwa nanyi.
12 我要在你們中間行走;我要作你們的上帝,你們要作我的子民。
Nitatembea miongoni mwenu nami nitakuwa Mungu wenu, nanyi mtakuwa watu wangu.
13 我是耶和華-你們的上帝,曾將你們從埃及地領出來,使你們不作埃及人的奴僕;我也折斷你們所負的軛,叫你們挺身而走。」
Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu, aliyewaleta nyinyi kutoka nchi ya Misri, ili kwamba msingeendelea kuwa watumwa wao. Nimevunja makomeo ya nira yenu na nikawafanya mtembee kwa kunyooka.
14 「你們若不聽從我,不遵行我的誡命,
Lakini ikiwa hamtanisikiliza mimi,
15 厭棄我的律例,厭惡我的典章,不遵行我一切的誡命,背棄我的約,
na kutozitii amri hizi, na ikiwa mtayakataa maagizo yangu, na kuzichukia sana sheria zangu, kiasi kwamba hamtaweza kuzitii amri zangu zote, lakini mkalivunja agano langu—
16 我待你們就要這樣:我必命定驚惶,叫眼目乾癟、精神消耗的癆病熱病轄制你們。你們也要白白地撒種,因為仇敵要吃你們所種的。
—kama mtafanya mambo haya, Nami nitafanya hili kwenu: Nitasababisha hofu juu yenu, maradhi na homa kali itakayoangamiza macho na kuondoa uhai wenu. Mtapanda mbegu zenu kwa hasara, kwa sababu adui zenu watakula mazao yake.
17 我要向你們變臉,你們就要敗在仇敵面前。恨惡你們的,必轄管你們;無人追趕,你們卻要逃跑。
Nitakaza uso wangu dhidi yenu, na mtashindwa na adui zenu. Watu wanaowachukia watatawala juu yenu, na mtakimbia hata kama hakutakuwa na yeyote anayewafukuza.
18 你們因這些事若還不聽從我,我就要為你們的罪加七倍懲罰你們。
Iwapo hamtasikiliza maagizo yangu, Nami niwataadhibu vikali mara saba kwa dhambi zenu.
19 我必斷絕你們因勢力而有的驕傲,又要使覆你們的天如鐵,載你們的地如銅。
Nami nitakivunja kiburi chenu katika uwezo wenu. Nitaifanya mbingu juu yenu iwe kama chuma na nchi yenu kama shaba.
20 你們要白白地勞力;因為你們的地不出土產,其上的樹木也不結果子。
Nguvu yenu itatumika bure, kwa sababu nchi yenu haitazalisha mavuno yake, na miti yenu katika nchi haitazaa matunda yake.
21 「你們行事若與我反對,不肯聽從我,我就要按你們的罪加七倍降災與你們。
Iwapo mtataenenda kinyume changu na hamtanisikiliza mimi, nitaleta mapigo mara saba zaidi juu yenu, sawasawa na dhambi zenu.
22 我也要打發野地的走獸到你們中間,搶吃你們的兒女,吞滅你們的牲畜,使你們的人數減少,道路荒涼。
Nitatuma wanyama mapori hatari dhidi yenu, ambao watawaibia watoto wenu, kuangamiza mifugo yenu na kuwafanya mwe wachache katika idadi yenu. Hivyo barabara zenu zitakuwa nyeupe.
23 「你們因這些事若仍不改正歸我,行事與我反對,
Endapo pamoja na mambo haya kuwapata lakini msiyakubali marekebisho yangu na mkazidi kuenenda katika upinzani dhidi yangu,
24 我就要行事與你們反對,因你們的罪擊打你們七次。
ndipo nami pia nitaenenda kinyume chenu, na Mimi mwenyewe nitawaadhibu mara saba kwa sababu ya dhambi zenu.
25 我又要使刀劍臨到你們,報復你們背約的仇;聚集你們在各城內,降瘟疫在你們中間,也必將你們交在仇敵的手中。
Nitaleta upanga juu yenu utakaowaadhibu kwa kisasi kwa sababu ya kulivunja agano. Nanyi mtajikusanya kwenye miji yenu, Nami nitatuma humo maafa miongoni mwenu, na mtachukuliwa mikononi mwa adui yenu.
26 我要折斷你們的杖,就是斷絕你們的糧。那時,必有十個女人在一個爐子給你們烤餅,按分量秤給你們;你們要吃,也吃不飽。
Nitakapokomesha mgao wa chakula, wanawake kumi wataweza kuoka mkate wako katika chombo kimoja cha kuokea na watakugawia mkate wako kwa uzani. Nanyi mtakula lakini hamtatoshelezwa.
27 「你們因這一切的事若不聽從我,卻行事與我反對,
Endapo hamtanisikiliza pamoja na mambo haya kuwapata, lakini mkazidi kuenenda kinyume na mimi,
28 我就要發烈怒,行事與你們反對,又因你們的罪懲罰你們七次。
kisha nami nitakwenda kinyume nanyi katika hasira, Nami nitawaadhibu hata mara saba kulingana na wingi wa dhambi zenu.
29 並且你們要吃兒子的肉,也要吃女兒的肉。
Ndipo mtakapokula nyama ya wana wenu; mtakula nyama ya binti zenu.
30 我又要毀壞你們的邱壇,砍下你們的日像,把你們的屍首扔在你們偶像的身上;我的心也必厭惡你們。
Nitapaangamiza mahali penu pa juu, kuziangusha chini madhabahu zenu za kufukizia uvumba, na kuzitupa maiti zenu juu ya maiti ya sanamu zenu, na Mimi mwenyewe nitawadharau nyinyi.
31 我要使你們的城邑變為荒涼,使你們的眾聖所成為荒場;我也不聞你們馨香的香氣。
Nitaigeuza miji yennu kuwa magofu na kupaharibu patakatifu penu. Nami sitapendezwa na harufu nzuri ya matoleo yenu.
32 我要使地成為荒場,住在其上的仇敵就因此詫異。
Nami nitaiharibu nchi. Adui zenu watakaokuwa wakiishi humo watashtushwa na uharibifu huo.
33 我要把你們散在列邦中;我也要拔刀追趕你們。你們的地要成為荒場;你們的城邑要變為荒涼。
Nami nitawatawanya nyinyi katika mataifa, na nitaufuta upanga wangu na kuwafuatia. Nchi yenu itatelekezwa, na miji yenu itakuwa magofu.
34 「你們在仇敵之地居住的時候,你們的地荒涼,要享受眾安息;正在那時候,地要歇息,享受安息。
Nayo nchi itazifurahia Sabato zake kwa kuwa itakuwa imetelekezwa na ninyi mkiwa katika nchi za daui zenu. Katika nyakati hizo, nchi itapumzika na kufurahia Sabato zake.
35 地多時為荒場,就要多時歇息;地這樣歇息,是你們住在其上的安息年所不能得的。
Maadamu itakuwa imetelekezwa, itakuwa na pumziko, ambalo litakuwa ni pumziko iliyolikosa pamoja na Sabato zenu mlipokuwa mkiishi ndani yake.
36 至於你們剩下的人,我要使他們在仇敵之地心驚膽怯。葉子被風吹的響聲,要追趕他們;他們要逃避,像人逃避刀劍,無人追趕,卻要跌倒。
Na kwa wale watakoachwa humo kwenye nchi za adui zenu, Nitatuma hofu ndani ya mioyo yenu kiasi kwamba hata kama ni maelfu ya majani tu yatakapopeperushwa katika upepo yatawaogofyeni. Nanyi mtaanguka hata kama hakutakuwa na awafukuzaye.
37 無人追趕,他們要彼此撞跌,像在刀劍之前。你們在仇敵面前也必站立不住。
Mtajikwaa kila mmoja juu ya mwenzake kama vile mlikuwa mkiukimbia upanga, hata kama hakutakuwa na awafukuzaye nyinyi. Hamtakuwa na nguvu ya kusimama mbele ya daui zenu.
38 你們要在列邦中滅亡;仇敵之地要吞吃你們。
Nanyi mtaangamia miongoni mwa mataifa, nayo nchi ya adui zenu yenyewe itawamezani.
39 你們剩下的人必因自己的罪孽和祖宗的罪孽在仇敵之地消滅。
Wale watakosalia miongoni mwenu watapotelea katika dhambi zao, huko kwenye nchi za adui zenu, na kwa sababu ya dhambi zao, na kwa sababu ya dhambi za baba zao watapotelea mbali pia.
40 「他們要承認自己的罪和他們祖宗的罪,就是干犯我的那罪,並且承認自己行事與我反對,
Lakini kama watakiri dhambi zao na dhambi ya baba zao, na usaliti wao ambao kwao hawakuwa waaminifu kwangu, pia na mwenendo wao dhidi yangu—
41 我所以行事與他們反對,把他們帶到仇敵之地。那時,他們未受割禮的心若謙卑了,他們也服了罪孽的刑罰,
ambao ulinisababisha kuwa kinyume nao, na kuwaleta katika nchi ya adui zao—iwapo mioyo yao isiyotahiriwa itanynyekezwa,
42 我就要記念我與雅各所立的約,與以撒所立的約,與亞伯拉罕所立的約,並要記念這地。
na iwapo wataikubali adhabu kwa ajili ya dhambi zao, nami nitalikumbuka agano langu na Yakobo, agano langu na Isaka, agano langu na Abrahamu; Pia, nitaikumbuka nchi.
43 他們離開這地,地在荒廢無人的時候就要享受安息。並且他們要服罪孽的刑罰;因為他們厭棄了我的典章,心中厭惡了我的律例。
Nchi itakayotelekezwa na wao, hivyo itapendezwa na Sabato zake inapobaki imetelekezwa na wao. Itawapasa kulipa hatia kwa dhambi zao kwa sababu ni wao wenyewe ndiyo walioyakataa maagizo yangu na kuzichukia sheria zangu.
44 雖是這樣,他們在仇敵之地,我卻不厭棄他們,也不厭惡他們,將他們盡行滅絕,也不背棄我與他們所立的約,因為我是耶和華-他們的上帝。
Lakini pamoja na haya yote, watapokuwa katika nchi ya adui zao, Mimi stawakataa wao, wala sitawachukia ili kuwaangamiza kabisa na kulifutilia mbali agano langu nilililoagana nao, kwa kuwa Mimi ndimi Yahweh Mungu wao.
45 我卻要為他們的緣故記念我與他們先祖所立的約。他們的先祖是我在列邦人眼前、從埃及地領出來的,為要作他們的上帝。我是耶和華。」
Bali kwa ajili yao, nitalikumbuka agano langu na baba zao, niliowaleta kutoka katika nchi ya Misri machoni pa mataifa, ili niwe Mungu wao. Mimi ndimi Yahweh.”
46 這些律例、典章,和法度是耶和華與以色列人在西奈山藉着摩西立的。
Hizi ndizo amri, hukumu, na sheria ambazo Yahweh alifanya baina yake na watu wa Israeli kwenye Mlima Sinai kwa kupitia Musa.

< 利未記 26 >