< 利未記 20 >
Yahweh akazungumza na Musa, akasema,
2 「你還要曉諭以色列人說:凡以色列人,或是在以色列中寄居的外人,把自己的兒女獻給摩洛的,總要治死他;本地人要用石頭把他打死。
“Waambie watu wa Waisraeli, 'mtu yeyote miongoni mwa watu Israeli, au Mgeni yeyote anayeishi miongoni mwa Waisraeli atakayemtoa mtoto wake yeyote kwa Moleki, hakika atauawa. Ni lazima watu wa nchi wamponde kwa mawe.
3 我也要向那人變臉,把他從民中剪除;因為他把兒女獻給摩洛,玷污我的聖所,褻瀆我的聖名。
Pia nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo na kumkatilia mbali kutoka miongoni mwa watu wake kwa sababu amemtoa mtoto wake kwa Moleki, ili kupatia unajisi mahali pangu patakatifu na kulinajisi jina langu takatifu.
4 那人把兒女獻給摩洛,本地人若佯為不見,不把他治死,
Na kama watu wa nchi watayafumba macho yao kwa mtu huyo anapomtoa mmoja wa watoto wake kwa Moleki, kama hawatamwua mtu huyo, ndipo Mimi mwenyewe nitaukaza uso wangu dhidi ya mtu huyo na ukoo wake,
5 我就要向這人和他的家變臉,把他和一切隨他與摩洛行邪淫的人都從民中剪除。
Nami nitamkatilia mbali pamoja na yeyote anayejifanya kahaba ili kufanya umalaya na Moleki.
6 「人偏向交鬼的和行巫術的,隨他們行邪淫,我要向那人變臉,把他從民中剪除。
Mtu yule anayewageukia wanaozungumza na wafu, au na wale wanaozungumza na roho ili kufanya ukahaba nao, Nitakaza uso wangu dhidi ya mtu huyo; Nami nitamkatilia mbali atoke miongoni mwa watu wake.
7 所以你們要自潔成聖,因為我是耶和華-你們的上帝。
Kwa hiyo jitakaseni wenyewe na muwe watakatifu, kwa sababu Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu.
8 你們要謹守遵行我的律例;我是叫你們成聖的耶和華。
Mtazitunza amari zangu na kuzifuta. Mimi ndimi Yahweh anayewatenga ninyi muwe watakatifu.
9 凡咒罵父母的,總要治死他;他咒罵了父母,他的罪要歸到他身上。
Yeyote amlaaniye baba yake au mama yake hakika mtu huyo atauawa. Amemlaani baba yake au mama yake, kwa hiyo ana hatia na anastahili kufa.
Mwanaume yeyote afanyaye uzinzi na mke wa mwanaume mwingine, yaani, yeyote anayezini na mke wa jirani yake—yule mwanaume mzinzi na mwanamke mzinzi ni lazima wote wawili wauawe.
11 與繼母行淫的,就是羞辱了他父親,總要把他們二人治死,罪要歸到他們身上。
Mwanaume yeyote anayelala na mke wa baba yake ili kukutana naye kimwili amemfedhehesha baba yake mwenye. Wote wawili; mwana huyo na mke huyo wa baba yake kwa hakika watauawa. wanahatia na wanastahili kufa.
12 與兒婦同房的,總要把他們二人治死;他們行了逆倫的事,罪要歸到他們身上。
Kama mwanaume atalala na mke wa mwanawe, wote wawili; mwanaume huyo na mke huyo wa mwanawe hakika watauawa. Wametenda upotovu. Wana hatia na wanastahili kufa.
13 人若與男人苟合,像與女人一樣,他們二人行了可憎的事,總要把他們治死,罪要歸到他們身上。
Kama mwanaume analala na mwanaume mwingine kama alalavyo na mwanamke, wote wawili watakuwa wamefanya jambo lililo ovu. Hakika watauawa. Wana hatia na wanastahili kufa.
14 人若娶妻,並娶其母,便是大惡,要把這三人用火焚燒,使你們中間免去大惡。
Ikiwa mwanaume atamwoa mwanamke na pia akamwoa mama wa mwanamke huyo, huu ni uovu. Ni lazima wachomwe kwa moto, wote wawili, mwanaume huyo na manamke huyo, ili kwamba hapatakuwepo na uovu miongoni mwenu.
Ikiwa mwanaume analala na mnyama, hakika atauawa, ni lazima mumuue na mnyama huyo pia.
16 女人若與獸親近,與牠淫合,你要殺那女人和那獸,總要把他們治死,罪要歸到他們身上。
Ikiwa mwanamke anamkaribia mnyama ili kulala naye, ni lazima mmuuwe mwanamke huyo pamoja na mnyama. Kwa hakika ni lazima wauawe. wana hatia na wanastahili kufa.
17 「人若娶他的姊妹,無論是異母同父的,是異父同母的,彼此見了下體,這是可恥的事;他們必在本民的眼前被剪除。他露了姊妹的下體,必擔當自己的罪孽。
Ikiwa mwanaume analala na dada yake, ama ni binti ya baba yake au binti ya mama yake—ikiwa wamelala pamoja, hilo ni jambo la aibu. Ni lazima wakatiliwe mbali watoke machoni pa watu wao, kwa sababu amelala na dada yake. Ni lazima aibebe hatia yake.
18 婦人有月經,若與她同房,露了她的下體,就是露了婦人的血源,婦人也露了自己的血源,二人必從民中剪除。
Kama mwanaume analala na mwanamke katika kipindi cha hedhi yake, na amekutana naye kimwili, atakuwa amefunua mtiririko wa damu yake, chanzo cha damu yake. Ni lizima wote wawili wakatiliwe mbali kutoka mingoni mwa watu wao.
19 不可露姨母或是姑母的下體,這是露了骨肉之親的下體;二人必擔當自己的罪孽。
Usilale na dada ya mama yako, au dada ya baba yako, kwa sababu ungeweza kumwaibisha jamaa yako wa karibu. Ni lazima utabeba hatia yako mwenyewe.
20 人若與伯叔之妻同房,就羞辱了他的伯叔;二人要擔當自己的罪,必無子女而死。
Ikiwa mwanaume analala na shangazi yake, atakuwa amemfedhehesha mjomba wake. Wanapokufa, nitawaadhibu wote wawili, na wanapokufa nitauondolea mbali urithi wa watoto wao ambao wangeliupokea kutoka kwa wazazi wao.
21 人若娶弟兄之妻,這本是污穢的事,羞辱了他的弟兄;二人必無子女。
Ikiwa mwanaume anamwoa mke wa kaka yake wakati ambapo kaka yake angali hai, hilo ni jambo la aibu. Amemfedhehesha kaka yake, na nitaondolea mbali mali yoyote amabayo watoto wao wangerithi kutoka kwa wazazi wao.
22 「所以,你們要謹守遵行我一切的律例典章,免得我領你們去住的那地把你們吐出。
Kwa hiyo imewapasa kuzishika amri na sheria zangu zote; ni lazima mzitii ili kwamba ile nchi ambayo ninawaleta kuishi isiwatapike nyinyi.
23 我在你們面前所逐出的國民,你們不可隨從他們的風俗;因為他們行了這一切的事,所以我厭惡他們。
Msienende katika desturi za mataifa ambayo nitayafukuza mbele yenu, ni kwa sababu wamefanya mambo haya yote, nami mimewachukia wao.
24 但我對你們說過,你們要承受他們的地,就是我要賜給你們為業、流奶與蜜之地。我是耶和華-你們的上帝,使你們與萬民有分別的。
Nami nikawaambia ninyi, “Mtaimiliki nchi yao, nitaitoa kwenu ili muimiliki, nchi itiririkayo amaziwa na asali. Mimi ndimi Yahweh Mungu wenu, aliyewatenga nyinyi kutoka kwa watu wengine.
25 所以,你們要把潔淨和不潔淨的禽獸分別出來;不可因我給你們分為不潔淨的禽獸,或是滋生在地上的活物,使自己成為可憎惡的。
Ni lazima pia mtofautishe kati ya wanya najisi na wale walio safi, na kati ya ndege walio najisi na walio safi. Msijichafue wenyewe kwa wanyama au ndege au kiumbe kitambaacho juu ya nchi kilicho najisi, ambacho nimekitenga kuwa najisi.
26 你們要歸我為聖,因為我-耶和華是聖的,並叫你們與萬民有分別,使你們作我的民。
Mtakuwa watakatifu, kwa kuwa Mimi, Yahweh, ni mtakakatifu, nami nimewatenga nyinyi kutoka kwa watu wengine, kwa kuwa nyinyi ni wangu.
27 「無論男女,是交鬼的或行巫術的,總要治死他們。人必用石頭把他們打死,罪要歸到他們身上。」
Mwanaume au mwanamke anayeongea na wafu au anayeongea na roho hakika atauawa. Watu watawaponda kwa mawe. Wanayo hatia na wanastahili kufa.