< 士師記 20 >
1 於是以色列從但到別是巴,以及住基列地的眾人都出來,如同一人,聚集在米斯巴耶和華面前。
Ndipo watu wote wa Israeli wakatoka kama mtu mmoja, toka Dani mpaka Beer-sheba, pamoja na nchi ya Gileadi; nao wakakusanyika mbele za Bwana huko Mispa.
2 以色列民的首領,就是各支派的軍長,都站在上帝百姓的會中;拿刀的步兵共有四十萬。
Viongozi wa watu wote, wa kabila zote za Israeli, wakachukua nafasi zao kwenye kusanyiko la watu wa Mungu-watu 400, 000 waendao kwa miguu, ambao walikuwa tayari kupigana na upanga.
3 以色列人上到米斯巴,便雅憫人都聽見了。以色列人說:「請你將這件惡事的情由對我們說明。」
Basi wana wa Benyamini waliposikia kwamba watu wa Israeli walikuwa wamepanda Mispa. Wana wa Israeli wakasema, “Tuambieni ni kwa namna gani huu uovu umefanyika.”
4 那利未人,就是被害之婦人的丈夫,回答說:「我和我的妾到了便雅憫的基比亞住宿。
Mlawi, mume wa mwanamke aliyeuawa, akajibu, Nilikuja Gibea katika nchi ya Benyamini, mimi na suria wangu, ili tulale.
5 基比亞人夜間起來,圍了我住的房子,想要殺我,又將我的妾強姦致死。
Wakati wa usiku, viongozi wa Gibea walinishambulia, wakizunguka nyumba na wakakusudia kuniua. Walimkamata na kumbaka suria wangu, naye akafa.
6 我就把我妾的屍身切成塊子,使人拿着傳送以色列得為業的全地,因為基比亞人在以色列中行了兇淫醜惡的事。
Nilimchukua suria wangu na kumkata mwili wake vipande vipande, na kuweka katika kila nchi ya urithi wa Israeli, kwa sababu wamefanya uovu huo na upumbavu katika Israeli.
Sasa, ninyi Waisraeli wote, toeni maneno na ushauri wenu hapa.”
8 眾民都起來如同一人,說:「我們連一人都不回自己帳棚、自己房屋去。
Watu wote wakaondoka pamoja kama mtu mmoja, wakasema, Hakuna hata mmoja wetu atakayeenda hemani kwake, wala hakuna hata mmoja wetu atakayerudi nyumbani kwake.
9 我們向基比亞人必這樣行,照所掣的籤去攻擊他們。
Lakini sasa hivi ndivyo tutakavyoifanyia Gibea tutaishambulia kama kura inavyotuongoza.
10 我們要在以色列各支派中,一百人挑取十人,一千人挑取百人,一萬人挑取千人,為民運糧,等大眾到了便雅憫的基比亞,就照基比亞人在以色列中所行的醜事征伐他們。」
Tutachukua watu kumi katika mia moja katika makabila yote ya Israeli, na mia moja katika elfu, na elfu moja katika elfu kumi, kuwapa chakula kwa ajili ya watu hawa, ili waweze kufika Gibea katika Benyamini, watawaadhibu kwa uovu wao waliofanya katika Israeli.
11 於是以色列眾人彼此連合如同一人,聚集攻擊那城。
Basi askari wote wa Israeli wakakusanyika juu ya mji, kama mtu mmoja.
12 以色列眾支派打發人去,問便雅憫支派的各家說:「你們中間怎麼做了這樣的惡事呢?
Makabila ya Israeli waliwatuma watu kwa kabila lote la Benyamini, wakisema, “Uovu huu uliofanywa kati yenu ni nini?
13 現在你們要將基比亞的那些匪徒交出來,我們好治死他們,從以色列中除掉這惡。」便雅憫人卻不肯聽從他們弟兄以色列人的話。
Kwa hiyo, tupeni watu hao waovu wa Gibea, tupate kuwaua, na hivyo tutaondoa kabisa uovu huu kutoka kwa Israeli.” Lakini Wabenyamini hawakusikiliza sauti ya ndugu zao, watu wa Israeli,
14 便雅憫人從他們的各城裏出來,聚集到了基比亞,要與以色列人打仗。
Ndipo wana wa Benyamini wakakusanyika kutoka mijini kwenda Gibea, wakajiandaa kupigana na wana wa Israeli.
15 那時便雅憫人從各城裏點出拿刀的,共有二萬六千;另外還有基比亞人點出七百精兵。
Watu wa Benyamini wakakusanya kutoka miji yao ili kupigana siku ile, askari elfu ishirini na sita waliopangwa kupigana na upanga. Walakini, kuna watu mia saba waliochaguliwa kutoka kwa wenyeji wa Gibea.
16 在眾軍之中有揀選的七百精兵,都是左手便利的,能用機弦甩石打人,毫髮不差。
Miongoni mwa askari wote hawa walikuwa watu mia saba waliochaguliwa ambao walikuwa wenye shoto. Kila mmoja wao angeweza kupiga unywele kwa mawe na asikose.
17 便雅憫人之外,點出以色列人拿刀的,共有四十萬,都是戰士。
Watu wa Israeli, bila kuhesabu namba kutoka kwa Benyamini, walikuwa na watu 400, 000 waliokuwa wamejifunza kupigana na upanga. Wote hawa walikuwa watu wa vita.
18 以色列人就起來,到伯特利去求問上帝說:「我們中間誰當首先上去與便雅憫人爭戰呢?」耶和華說:「猶大當先上去。」
Watu wa Israeli waliondoka, wakaenda Betheli, wakaomba ushauri kutoka kwa Mungu. Wakauliza, “Ni nani kwanza atakayewaangamiza watu wa Benyamini kwa ajili yetu?” Bwana akasema, “Yuda atashambulia kwanza.”
Watu wa Israeli waliamka asubuhi na wakahamisha kambi yao karibu na Gibea.
20 以色列人出來,要與便雅憫人打仗,就在基比亞前擺陣。
Watu wa Israeli walikwenda kupigana na Benyamini. Wakaweka nafasi zao za vita dhidi yao huko Gibea.
21 便雅憫人就從基比亞出來,當日殺死以色列人二萬二千。
Watu wa Benyamini wakatoka Gibea, nao wakawaua watu elfu ishirini na mbili wa jeshi la Israeli siku ile.
22 以色列人彼此奮勇,仍在頭一日擺陣的地方又擺陣。
Wana wa Israeli walijitia nguvu wenyewe, na wakaunda mstari wa vita mahali pale walipokwisha kuchukua nafasi siku ya kwanza.
23 未擺陣之先,以色列人上去,在耶和華面前哭號,直到晚上,求問耶和華說:「我們再去與我們弟兄便雅憫人打仗可以不可以?」耶和華說:「可以上去攻擊他們。」
Na wana wa Israeli wakaenda, wakalia mbele za Bwana hata jioni. Walitaka mwongozo kutoka kwa Bwana “Je, tunapaswa kwenda tena kupigana na ndugu zetu, watu wa Benyamini?” Naye Bwana akasema, “Wapigeni!”
Basi watu wa Israeli wakapigana na askari wa Benyamini siku ya pili.
25 便雅憫人也在這日從基比亞出來,與以色列人接戰,又殺死他們一萬八千,都是拿刀的。
Siku ya pili, Benyamini alitoka kupigana nao kutoka Gibea, nao wakawaua watu wa Israeli elfu kumi na nane. Wote walikuwa watu ambao walijifunza kupigana na upanga.
26 以色列眾人就上到伯特利,坐在耶和華面前哭號,當日禁食直到晚上;又在耶和華面前獻燔祭和平安祭。
Basi askari wote wa Israeli na watu wote wakaenda Betheli, wakalia, wakakaa mbele za Bwana; nao wakafunga siku hiyo hata jioni, wakatoa sadaka za kuteketezwa na sadaka za amani mbele za Bwana.
27 那時,上帝的約櫃在那裏;亞倫的孫子、以利亞撒的兒子非尼哈侍立在約櫃前。以色列人問耶和華說:「我們當再出去與我們弟兄便雅憫人打仗呢?還是罷兵呢?」耶和華說:「你們當上去,因為明日我必將他們交在你們手中。」
Wana wa Israeli wakamwomba Bwana, - kwa sababu ya sanduku la agano la Mungu lilikuwapo siku hizo;
na Finehasi, mwana wa Eleazari, mwana wa Haruni, aliyekuwa akihudumia mbele ya sanduku siku hizo. “Je twende vitani tena dhidi ya watu wa Benyamini, ndugu zetu, au tuache?” Bwana akasema, “Wapigeni, kwa maana kesho nitawasaidia kuwashinda.
Basi Israeli akaweka watu mahali pa siri karibu na Gibea.
30 第三日,以色列人又上去攻擊便雅憫人,在基比亞前擺陣,與前兩次一樣。
Watu wa Israeli wakapigana na wana wa Benyamini kwa siku ya tatu, nao wakajenga vita vyao juu ya Gibea, kama walivyotangulia.
31 便雅憫人也出來迎敵,就被引誘離城;在田間兩條路上,一通伯特利,一通基比亞,像前兩次,動手殺死以色列人約有三十個。
Watu wa Benyamini wakaenda kupigana na watu, nao wakachukuliwa mbali na mji. Walianza kuua baadhi ya watu. Kulikuwa na watu thelathini wa Israeli ambao walikufa katika mashamba na barabara. Njia moja ilienda Betheli, na nyingine ikaenda Gibea.
32 便雅憫人說:「他們仍舊敗在我們面前。」但以色列人說:「我們不如逃跑,引誘他們離開城到路上來。」
Ndipo wana wa Benyamini wakasema, “Wameshindwa na wanatukimbia, kama hapo awali.” Lakini askari wa Israeli wakasema, “Hebu tukimbie na kuwavuta mbali na mji hadi barabarani.”
33 以色列眾人都起來,在巴力‧他瑪擺陣,以色列的伏兵從馬利‧迦巴埋伏的地方衝上前去。
Watu wote wa Israeli waliondoka kutoka mahali pao na wakajipanga kwa vita huko Baal-Tamari. Basi askari wa Israeli waliokuwa wakijificha mahali pa siri walikimbia kutoka Maare-Geba.
34 有以色列人中的一萬精兵,來到基比亞前接戰,勢派甚是凶猛;便雅憫人卻不知道災禍臨近了。
Wakatoka juu ya Gibea watu kumi elfu waliochaguliwa kutoka Israeli yote, na vita vilikuwa kali, lakini Wabenjamini hawakujua kwamba msiba ulikuwa karibu nao.
35 耶和華使以色列人殺敗便雅憫人。那日,以色列人殺死便雅憫人二萬五千一百,都是拿刀的。
Bwana akamshinda Benyamini mbele ya Israeli. Siku hiyo, askari wa Israeli waliwauawa watu wa Benyamini 25, 100. Wote hawa waliokufa walikuwa wale waliokuwa wamejifunza kupigana na upanga.
36 於是便雅憫人知道自己敗了。先是以色列人;因為靠着在基比亞前所設的伏兵,就在便雅憫人面前詐敗。
Basi askari wa Benyamini waliona wameshindwa. Wana wa Israeli walikuwa wametoa ardhi kwa Benyamini, kwa kuwa walikuwa wakihesabu watu waliowaweka katika nafasi zilizofichwa nje ya Gibea.
Ndipo watu waliokuwa wameficha wakainuka na haraka na wakamkimbia Gibea. Nao wakauawa kila mtu aliyeishi mjini kwa upanga wao.
38 以色列人預先同伏兵約定在城內放火,以煙氣上騰為號。
Ishara iliyopangwa kati ya askari wa Israeli na watu waliojificha kwa siri itakuwa wingu kubwa la moshi litatokea nje ya mji.
39 以色列人臨退陣的時候,便雅憫人動手殺死以色列人,約有三十個,就說:「他們仍像前次被我們殺敗了。」
Ishara ilipokuja askari wa Israeli wakageuka kutoka kwenye vita. Basi Benyamini wakaanza kushambulia na wakawaua watu wa Israeli thelathini, wakasema, “Hakika wanapigwa mbele yetu, kama katika vita vya kwanza.”
40 當煙氣如柱從城中上騰的時候,便雅憫人回頭觀看,見全城的煙氣沖天。
Lakini wakati nguzo ya moshi ilipoanza kuinuka nje ya mji, Wabenjamini waligeuka na kuona moshi ukitanda mbinguni kutoka mji mzima.
41 以色列人又轉身回來,便雅憫人就甚驚惶,因為看見災禍臨到自己了。
Ndipo watu wa Israeli wakawageuka. Wana wa Benyamini waliogopa, kwa sababu waliona kwamba maafa yaliwajia.
42 他們在以色列人面前轉身往曠野逃跑;以色列人在後面追殺。那從各城裏出來的,也都夾攻殺滅他們。
Basi wakakimbia kutoka kwa wana wa Israeli, kuelekea njia ya jangwani. Lakini vita viliwapata. Askari wa Israeli walitoka mijini na wakawaua pale waliposimama.
43 以色列人圍繞便雅憫人,追趕他們,在他們歇腳之處、對着日出之地的基比亞踐踏他們。
Waliwalzungukia wana wa Benjamini na wakawafuata. Nao wakawakanyaga huko Noha, wakawaua mpaka upande wa mashariki wa Gibea.
Kutoka kabila la Benyamini, watu kumi na nane elfu walikufa, wote walikuwa wanaume waliojulikana katika vita.
45 其餘的人轉身向曠野逃跑,往臨門磐去。以色列人在道路上殺了他們五千人,如拾取遺穗一樣,追到基頓又殺了他們二千人。
Wakageuka na kukimbia kuelekea jangwani hadi mwamba wa Rimoni. Waisraeli waliuawa zaidi ya elfu tano kati yao barabarani. Waliendelea kuwafuata, wakifuata kwa njia kuu kwenda Gidomu, na huko waliuawa elfu mbili zaidi.
46 那日便雅憫死了的共有二萬五千人,都是拿刀的勇士。
Askari wote wa Benyamini walioshuka siku hiyo walikuwa watu ishirini na tano waliokuwa wamejifunza kupigana kwa upanga; wote walikuwa wanajulikana katika vita.
47 只剩下六百人,轉身向曠野逃跑,到了臨門磐,就在那裏住了四個月。
Lakini watu mia sita wakageuka na kukimbilia jangwani, kuelekea mwamba wa Rimoni. Wakakaa katika mwamba wa Rimoni kwa muda wa miezi minne.
48 以色列人又轉到便雅憫地,將各城的人和牲畜,並一切所遇見的,都用刀殺盡,又放火燒了一切城邑。
Askari wa Israeli waliwarudia watu wa Benyamini na wakawashinda na kuwaua-mji mzima, ng'ombe, na kila kitu walichopata. Pia walichoma moto kila mji katika njia yao.