< 士師記 2 >

1 耶和華的使者從吉甲上到波金,對以色列人說:「我使你們從埃及上來,領你們到我向你們列祖起誓應許之地。我又說:『我永不廢棄與你們所立的約。
Malaika wa Bwana akatoka Gilgali, akaenda Bokimu, akasema, “Nimekuleta kutoka Misri, na nimekuleta katika nchi niliyoapa kuwapa baba zako.
2 你們也不可與這地的居民立約,要拆毀他們的祭壇。你們竟沒有聽從我的話!為何這樣行呢?』
Nikasema, 'Sitakuvunja kamwe agano langu na wewe. Usifanye agano na wale wanaoishi katika nchi hii. Ziangushe madhabahu zao. Lakini hukusikiliza sauti yangu. Je! ni nini hiki ulichokifanya?
3 因此我又說:『我必不將他們從你們面前趕出;他們必作你們肋下的荊棘。他們的神必作你們的網羅。』」
Basi sasa nasema, “Sitawafukuza Wakanaani mbele yenu, nao watakuwa miiba kwenu, na miungu yao itakuwa mtego kwa ajili yenu.”
4 耶和華的使者向以色列眾人說這話的時候,百姓就放聲而哭;
Malaika wa Bwana alipowaambia maneno hayo kwa watu wote wa Israeli, watu wakapiga kelele na kulia.
5 於是給那地方起名叫波金。眾人在那裏向耶和華獻祭。
Waliita mahali hapo Bokimu. Hapo wakatoa dhabihu kwa Bwana.
6 從前約書亞打發以色列百姓去的時候,他們各歸自己的地業,佔據地土。
Yoshua alipowaruhusu watu waende zao, wana wa Israeli kila mmoja akaenda mahali alipopewa, wakiwa na umiliki wa ardhi yao.
7 約書亞在世和約書亞死後,那些見耶和華為以色列人所行大事的長老還在的時候,百姓都事奉耶和華。
Watu walimtumikia Bwana wakati wa maisha ya Yoshua na wazee walioendelea baada yake, ni wale waliokuwa wameona matendo yote makuu ya Bwana aliyoyafanya kwa Israeli.
8 耶和華的僕人、嫩的兒子約書亞,正一百一十歲就死了。
Yoshua mwana wa Nuni, mtumishi wa Bwana, alikufa akiwa na umri wa miaka 110.
9 以色列人將他葬在他地業的境內,就是在以法蓮山地的亭拿‧希烈,在迦實山的北邊。
Wakamzika ndani ya mpaka wa nchi aliyopewa huko Timnath Heresi, katika mlima wa Efraimu, kaskazini mwa Mlima Gaash.
10 那世代的人也都歸了自己的列祖。後來有別的世代興起,不知道耶和華,也不知道耶和華為以色列人所行的事。
Kizazi hicho chote kilikusanyika kwa baba zao. Kizazi kingine kilichofuata baada yao ambao hakikumjua Bwana au kile alichokifanya kwa Israeli.
11 以色列人行耶和華眼中看為惡的事,去事奉諸巴力,
Watu wa Israeli walifanya yaliyo mabaya machoni pa Bwana, nao wakawatumikia Mabaali.
12 離棄了領他們出埃及地的耶和華-他們列祖的上帝,去叩拜別神,就是四圍列國的神,惹耶和華發怒;
Wakaondoka kwa Bwana, Mungu wa baba zao, aliyewatoa kutoka Misri. Wakaifuata miungu mingine, miungu ya watu waliokuwa karibu nao, nao wakaisujudia. Wakamkasirisha BWANA kwa sababu
13 並離棄耶和華,去事奉巴力和亞斯她錄。
waliondoka kwa Bwana na kumwabudu Baal na Maashtoreti.
14 耶和華的怒氣向以色列人發作,就把他們交在搶奪他們的人手中,又將他們付與四圍仇敵的手中,甚至他們在仇敵面前再不能站立得住。
Hasira ya Bwana ikawaka juu ya Israeli, naye akawapa washambuliaji walioiba mali zao kutoka kwao. Aliwauza kama watumwa waliofanyika kwa nguvu za maadui zao waliowazunguka, hivyo hawakuweza kujikinga dhidi ya adui zao.
15 他們無論往何處去,耶和華都以災禍攻擊他們,正如耶和華所說的話,又如耶和華向他們所起的誓;他們便極其困苦。
Israeli walipokwenda kupigana, mkono wa Bwana ulikuwa dhidi yao kuwashinda, kama alivyowaapia. Na walikuwa katika shida kali.
16 耶和華興起士師,士師就拯救他們脫離搶奪他們人的手。
Ndipo Bwana akawainua waamuzi, waliowaokoa katika mikono ya wale waliokuwa wakiba mali zao.
17 他們卻不聽從士師,竟隨從叩拜別神,行了邪淫,速速地偏離他們列祖所行的道,不如他們列祖順從耶和華的命令。
Hata hivyo hawakuwasikiliza waamuzi wao. Hawakuwa waaminifu kwa Bwana na wakajitoa wenyewe kama makahaba kwa miungu mingine na kuabudu. Waligeuka upesi na kuiacha njia waliyoishi baba zao-wale waliotii amri za Bwana-lakini wao wenyewe hawakufanya hivyo.
18 耶和華為他們興起士師,就與那士師同在。士師在世的一切日子,耶和華拯救他們脫離仇敵的手。他們因受欺壓擾害,就哀聲歎氣,所以耶和華後悔了。
Bwana aliinua waamuzi kwa ajili yao, Bwana akawasaidia waamuzi na kuwakomboa kutoka kwa mikono ya adui zao siku zote muamuzi aliishi. Bwana aliwahurumia walipougua kwa sababu ya wale waliowadhulumu na kuwasumbua.
19 及至士師死後,他們就轉去行惡,比他們列祖更甚,去事奉叩拜別神,總不斷絕頑梗的惡行。
Lakini mwamuzi alipokufa, waligeuka na kufanya mambo ambayo yalikuwa mabaya zaidi kuliko baba zao walivyofanya. Wakaenda kuifuata miungu mingine kuitumikia na kuiabudu. Walikataa kuacha matendo yao yote mabaya au njia zao za ukaidi.
20 於是耶和華的怒氣向以色列人發作。他說:「因這民違背我吩咐他們列祖所守的約,不聽從我的話,
Hasira ya Bwana iliwaka juu ya Israeli; akasema, Kwa sababu taifa hili limevunja masharti ya agano langu ambalo nililiweka kwa ajili ya baba zao-kwa sababu hawakuisikiliza sauti yangu.
21 所以約書亞死的時候所剩下的各族,我必不再從他們面前趕出,
Tangu sasa sitaliondoa mbele yao taifa lolote aliloliacha Yoshua baada ya kufa.
22 為要藉此試驗以色列人,看他們肯照他們列祖謹守遵行我的道不肯。」
Nitafanya hivi ili kuwajaribu Israeli, ikiwa watafuata njia ya Bwana au sivyo, kama vile baba zao walivyoifuata.
23 這樣耶和華留下各族,不將他們速速趕出,也沒有交付約書亞的手。
Ndiyo sababu Bwana aliwaacha mataifa hayo, wala hakuwafukuza haraka na kuwatia mikononi mwa Yoshua.

< 士師記 2 >