< 約書亞記 8 >
1 耶和華對約書亞說:「不要懼怕,也不要驚惶。你起來,率領一切兵丁上艾城去,我已經把艾城的王和他的民、他的城,並他的地,都交在你手裏。
Yahweh akamwambia Yoshua, “Usiogope; usivunjike moyo. Chukua pamoja nawe watu wa vita. Pandeni kwenda Ai. Tazama nimemtia mkononi mwako mfalme wa Ai, watu wake, mji wake na nchi yake.
2 你怎樣待耶利哥和耶利哥的王,也當照樣待艾城和艾城的王。只是城內所奪的財物和牲畜,你們可以取為自己的掠物。你要在城後設下伏兵。」
Mtafanya hivyo pia huko Ai na mfalme wake kama mlivyofanya kwa Yeriko na mfalme wake, isipokuwa mtachukua nyara na mifugo kwa ajili yenu. Pangeni mashambulizi ya uviziaji nyuma ya mji.”
3 於是,約書亞和一切兵丁都起來,要上艾城去。約書亞選了三萬大能的勇士,夜間打發他們前往,
Basi Yoshua aliinuka na akawachukua kwenda Ai watu wote wa vita. Kisha Yoshua akachagua watu elfu thelathini - wenye nguvu na ujasiri - na aliwatuma waende wakati wa usiku.
4 吩咐他們說:「你們要在城後埋伏,不可離城太遠,都要各自準備。
Aliwaamuru, “Tazama, mtalala katika hali ya mashambulizi ya uviziaji dhidi ya mji, kwa nyuma yake. Usiende mbali sana na mji, lakini ninyi nyote muwe tayari.
5 我與我所帶領的眾民要向城前往。城裏的人像初次出來攻擊我們的時候,我們就在他們面前逃跑,
Mimi pamoja na watu wote walio pamoja nami tutaukaribia mji. Na wakati watakapokuja kutushambulia sisi, tutawakimbia kama tulivyofanya hapo mwanzo.
6 他們必出來追趕我們,直到我們引誘他們離開城;因為他們必說:『這些人像初次在我們面前逃跑。』所以我們要在他們面前逃跑,
Watatoka nje watukimbize mpaka hapo tutakapokuwa tumewavuta mbali sana na mji, watasema, “Wanatukimbia kama walivyofanya mara ya mwisho.' Hivyo tutawakimbia na kwenda mbali.
7 你們就從埋伏的地方起來,奪取那城,因為耶和華-你們的上帝必把城交在你們手裏。
Kisha mtapanda kutoka sehemu mliyojificha, na mtauteka mji. Yahweh Mungu wenu atawapa mkononi mwenu.
8 你們奪了城以後,就放火燒城,要照耶和華的話行。這是我吩咐你們的。」
Tazama nimewaamuru, mtakapouteka mji, mtauchoma moto. Mtayafanya haya wakati mtakapotii agizo lililotolewa katika neno la Yahweh.”
9 約書亞打發他們前往,他們就上埋伏的地方去,住在伯特利和艾城的中間,就是在艾城的西邊。這夜約書亞卻在民中住宿。
Yoshua akawatuma, na wakaenda sehemu ya uviziajia, na wakajificha kati ya Betheli na Ai sehemu ya magharibi ya Ai. Yoshua akalala miongoni mwa watu usiku ule.
10 約書亞清早起來,點齊百姓,他和以色列的長老在百姓前面上艾城去。
Yoshua aliamka asubuhi na mapema na akawaandaa tayari wanajeshi wake, Yoshua na wazee wa Israeli walishambuliwa watu wa Ai.
11 眾民,就是他所帶領的兵丁,都上去,向前直往,來到城前,在艾城北邊安營。在約書亞和艾城中間有一山谷。
Watu wote wa vita waliokuwa pamoja naye walipanda na kuukaribia mji. Walisogea karibu na mji na wakapiga kambi sehemu ya kasikazini mwa Ai. Kulikuwa na bonde kati yao na Ai.
12 他挑了約有五千人,使他們埋伏在伯特利和艾城的中間,就是在艾城的西邊,
Alichukua watu wapatao elfu tano hivi na akawaweka katika hali ya kuvizia katika upande wa magharibi mwa mji kati ya Betheli na Ai.
13 於是安置了百姓,就是城北的全軍和城西的伏兵。這夜約書亞進入山谷之中。
Waliwapanga wanajeshi wote, jeshi kuu katika upande wa kasikazini mwa mji, na walinzi wa nyuma upande wa magharibi mwa mji. Yoshua alilala bondeni usiku ule.
14 艾城的王看見這景況,就和全城的人,清早急忙起來,按所定的時候,出到亞拉巴前,要與以色列人交戰;王卻不知道在城後有伏兵。
Na ilikuwa alipoona hilo mfalme wa Ai, yeye pamoja na jeshi lake, waliamka asubuhi na mapema na walitoka kwa haraka kwenda kuwashambulia Israeli katika eneo linalokabili bonde la Mto Yordani. Hakujua kuwa kulikuwa na shambulizi la kuvizia lilikuwa linasubiria kushambulia kutokea kwa nyuma ya mji.
15 約書亞和以色列眾人在他們面前裝敗,往那通曠野的路逃跑。
Yoshua na Waisraeli wote walikubali wenyewe kushindwa mbele yenu, na wakakimbia kuelekea nyikani.
16 城內的眾民都被招聚,追趕他們;艾城人追趕的時候,就被引誘離開城。
Watu wote waliokuwa kwenye mji waliitwa kwa pamoja waende mbele yao, na walienda mbele ya Yoshua na kwa jinsi hiyo walivutwa mbali na mji.
17 艾城和伯特利城沒有一人不出來追趕以色列人的,撇了敞開的城門,去追趕以色列人。
Hapakuwa na mtu mme aliyesalia Ai na Betheli ambaye alikuwa hajaenda nje kuwafuatilia waisraeli. Na walipokuwa wanawafuatilia Waisraeli, Wakatoka na waliuacha mji wazi.
18 耶和華吩咐約書亞說:「你向艾城伸出手裏的短槍,因為我要將城交在你手裏。」約書亞就向城伸出手裏的短槍。
Yahweh akamwambia Yoshua, “Nyosha mkuki huo ulio mkononi mwako kuelekea Ai, kwa kuwa nitaitia Ai mikononi mwako.” Yoshua akaunyosha mkuki uliokuwa mkononi mwake kuuelekea mji.
19 他一伸手,伏兵就從埋伏的地方急忙起來,奪了城,跑進城去,放火焚燒。
Wanajeshi waliojificha katika hali ya kuvizia walitoka upesi katika eneo lao mara tu alipounyosha mkono wake. Walikimbia mbio na kuuingia mji na kuuteka. Na kwa haraka wakauchoma moto mji.
20 艾城的人回頭一看,不料,城中煙氣沖天,他們就無力向左向右逃跑。那往曠野逃跑的百姓便轉身攻擊追趕他們的人。
Watu wa Ai waligeuka na kuangalia nyuma. Waliona moshi kutoka katika mji ukipanda kwenda angani, na hawakuweza kutoroka kwa njia hii au ile. Kwa kuwa wanajeshi wa Israelei waliokuwa wamekimbia katika nyika, sasa walirudi kuwakabili wale waliokuwa wanawafuatilia.
21 約書亞和以色列眾人見伏兵已經奪了城,城中煙氣飛騰,就轉身回去,擊殺艾城的人。
Na wakati Yoshua na Israeli wote walipoona kuwa wale watu wa kuvizia wameuteka mji kwa ule moshi uliokuwa ukipanda, waligeuka nyuma na kuwaua watu wa Ai.
22 伏兵也出城迎擊艾城人,艾城人就困在以色列人中間,前後都是以色列人。於是以色列人擊殺他們,沒有留下一個,也沒有一個逃脫的,
Na wanajeshi wengine wa Israeli, wale waliokuwa wameingia ndani ya mji, walitoka nje ili kuwashambulia. Hivyo, watu wa Ai walikamatwa katikati ya majeshi ya Israeli, baadhi katika upande huu na wengine katika upande ule.
Lakini walimhifadhi mfalme wa Ai, ambaye walimteka akiwa hai, na kisha wakamleta kwa Yoshua.
24 以色列人在田間和曠野殺盡所追趕一切艾城的居民。艾城人倒在刀下,直到滅盡;以色列眾人就回到艾城,用刀殺了城中的人。
Ilikuwa baada ya Israeli walipokuwa wamemaliza kuuwaua wenyeji wote wa Ai katika uwanda kariibu na nyika mahali walipowafuata, na baada ya wao wote, hata yule wa mwisho, walipokuwa wamekwisha kulala kwa ncha ya upanga, Waisraeli wote walirudi Ai. Waliuteka mji kwa ncha ya upanga.
25 當日殺斃的人,連男帶女共有一萬二千,就是艾城所有的人。
Wale wote walikufa siku hiyo walikuwa watu elfu kumi na mbili elfu, wanaume na wanawake, wote ni watu wa Ai.
26 約書亞沒有收回手裏所伸出來的短槍,直到把艾城的一切居民盡行殺滅。
Yoshua hakuukunja mkono wake ambao alikuwa ameunyosha huku akishikilia mkuki wake, mpaka pale alipowateketeza kabisa watu wote wa Ai.
27 惟獨城中的牲畜和財物,以色列人都取為自己的掠物,是照耶和華所吩咐約書亞的話。
Waisraeli walichukua tu wanyama na nyara kutoka katika mji kwa ajili yao wenyewe, kama Yahweh alivyokuwa amemwagiza Yoshua.
28 約書亞將艾城焚燒,使城永為高堆、荒場,直到今日;
Yoshua aliichoma Ai na kuigeuza kuwa kichuguu cha mapango. Ni mahali palipoachwa ukiwa hata leo.
29 又將艾城王掛在樹上,直到晚上。日落的時候,約書亞吩咐人把屍首從樹上取下來,丟在城門口,在屍首上堆成一大堆石頭,直存到今日。
Alimtundika mfalme wa Ai juu ya mti mpaka jioni. Na jua lilipokuwa linaenda kuzama, Yoshua aliwaagiza na wakautoa mwili wa mfalme wakaushusha chini ya mti na kuutupa mbele ya malango ya mji. Huko wakaweka kichuguu kikubwa cha mawe juu yake. Kichuguu hicho kimebaki huko hata leo.
30 那時,約書亞在以巴路山上為耶和華-以色列的上帝築一座壇,
Kisha Yoshua akajenga madhabahu kwa Yahweh, Mungu wa Israeli katika Mlima wa Ebali,
31 是用沒有動過鐵器的整石頭築的,照着耶和華僕人摩西所吩咐以色列人的話,正如摩西律法書上所寫的。眾人在這壇上給耶和華奉獻燔祭和平安祭。
kama vile Musa mtumishi wa Yahweh alivyowaagiza watu wa Israeli, kama ilivyoandikwa katika kitabu cha sheria ya Musa: “Madhabahu ya mawe yasiyochongwa, ambayo juu yake hakuna mtu yeyote aliyetumia zana ya chuma.” Na allimtolea Yahweh sadaka ya kuteketezwa juu yake na wakatoa sadaka ya amani.
32 約書亞在那裏,當着以色列人面前,將摩西所寫的律法抄寫在石頭上。
Na huko aliandika juu ya mawe nakala ya sheria za Musa mbele ya watu wa Israeli.
33 以色列眾人,無論是本地人、是寄居的,和長老、官長,並審判官,都站在約櫃兩旁,在抬耶和華約櫃的祭司利未人面前,一半對着基利心山,一半對着以巴路山,為以色列民祝福,正如耶和華僕人摩西先前所吩咐的。
Waisraeli wote, wazee wao, maafisa, na waamuzi wao walisimama katika sehemu mbili za sanduku mbele ya makuhani na Walawi ambao hulibeba sanduku la Agano la Yahweh - wageni pamoja na wazalia, nusu yao walisimama mbele ya Mlima Gerizimu na nusu walisimama mbele ya Mlima Ebali. Waliwabariki watu wa Israeli kama Musa mtumishi wa Yahweh alivyowaagiza hapo mwanzo.
34 隨後,約書亞將律法上祝福、咒詛的話,照着律法書上一切所寫的,都宣讀了一遍。
Baada ya hayo, Yoshua alisoma maneno yote ya sheria, baraka na laana, kama zilivyoandikwa katika kitabu cha sheria.
35 摩西所吩咐的一切話,約書亞在以色列全會眾和婦女、孩子,並他們中間寄居的外人面前,沒有一句不宣讀的。
Halikusalia hata neno moja katika yote ambayo Musa alimwagiza Yoshua ambalo halikusomwa mbele ya kusanyiko la Waisraeli lilojumuisha wanawake, watoto wadogo na wageni walioishi miongoni mwao.