< 約書亞記 19 >

1 為西緬支派的人,按着宗族,拈出第二鬮。他們所得的地業是在猶大人地業中間。
Upigaji wa pili wa kura uliangukia kwa Simoni na waligawiwa kwa kila ukoo wao. Urithi wao ulikuwa katikati ya urithi ulikuwa ni mali ya kabila la Yuda.
2 他們所得為業之地就是:別是巴(或名示巴)、摩拉大、
Urithi waliokuwa nao ni Beerisheba, Sheba, Molada,
3 哈薩‧書亞、巴拉、以森、
Hazari Shuali, Bala, Ezemu,
4 伊利多拉、比土力、何珥瑪、
Elitoladi, Bethuli na Horma.
5 洗革拉、伯‧瑪加博、哈薩‧蘇撒、
Simoni alikuwa pia na Ziklagi, Bethi Markabothi, Hazari Susa,
6 伯‧利巴勿、沙魯險,共十三座城,還有屬城的村莊;
Bethi Lebaothi, na Sharuheni. Kulikuwa na miji kumi na mitatu pamoja na vijiji vyake. Vile vile
7 又有亞因、利門、以帖、亞珊,共四座城,還有屬城的村莊;
Simoni alimiliki Aini, Rimon, Etheri, na Ashani. Hii ilikuwa ni miji minne pamoja na vijiji vyake.
8 並有這些城邑四圍一切的村莊,直到巴拉‧比珥,就是南地的拉瑪。這是西緬支派按着宗族所得的地業。
Miji hii pamoja na vijiji vilivyoizunguka hata kufika Baalathi Beeri (ambao ndio Rama katika Negevu). Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Simoni, waliopewa kwa koo zao.
9 西緬人的地業是從猶大人地業中得來的;因為猶大人的分過多,所以西緬人在他們的地業中得了地業。
Urithi wa kabila la Simoni ulikuwa sehemu ya himaya ya kabila la Yuda. Hii ni kwasababu nchi waliyopewa kabila la Yuda ilikuwa ni kubwa kwao, na hivyo kabila la Simoni lilipokea urithi wao kutoka katika sehemu yao ya katikati.
10 為西布倫人,按着宗族,拈出第三鬮。他們地業的境界是到撒立;
Upigaji wa kura ya tatu uliangukia kwa kabila la Zabuloni, na walipewa kwa koo zao. Mpaka wa urithi wao ulianzia huko Saridi.
11 往西上到瑪拉拉,達到大巴設,又達到約念前的河;
Mpaka wao ulipanda upande wa magharibi kuelekea Marala na ukaigusa Dabeshethi, na kisha ukasonga kuelekea kijito kilichokuwa mkabala na Yokineamu.
12 又從撒立往東轉向日出之地,到吉斯綠‧他泊的境界,又通到大比拉,上到雅非亞;
Kutoka Saridi mpaka ulizunguka upande wa mashariki kuelekea mashariki na ulienda hadi mpaka wa Kislothi Tabori. Kutoka hapo uliendelea hadi Daberathi na kisha ulipanda hata Yafia.
13 從那裏往東,接連到迦特‧希弗,至以特‧加汛,通到臨門,臨門延到尼亞;
Kutoka hapo ulipita katika upande wa mashariki mwa Gathi Heferi, na kisha ukafika Ethikazini, baadaye ulienda hadi Rimoni na kisha ukageuka kuelekea Nea.
14 又繞過尼亞的北邊,轉到哈拿頓,通到伊弗他‧伊勒谷。
Mpaka ulizunguka kueleka kaskazini ukafika Hanathoni na ulikomea katika bonde la Ifta Eli.
15 還有加他、拿哈拉、伸崙、以大拉、伯利恆,共十二座城,還有屬城的村莊。
Mkoa huu ulijumuisha miji ya Katathi, Nahalali, Shimroni, Idala, na Bethlehemu. Kulikuwa na miji kumi na miwili, pamoja na vijiji vyake.
16 這些城並屬城的村莊就是西布倫人按着宗族所得的地業。
Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Zabuloni, waliopewa kwa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
17 為以薩迦人,按着宗族,拈出第四鬮。
Upigaji kura wa nne uliangukia kwa Isakari, na waligawiwa kufuatana na koo zao.
18 他們的境界是到耶斯列、基蘇律、書念、
Eneo lao lilijumuisha Jezreelli, Kesuloothi, Shunemu,
19 哈弗連、示按、亞拿哈拉、
Hafaraimu, Shioni, na Anaharathi.
20 拉璧、基善、亞別、
Pia ilijumuisha miji ya Rabithi, Kishioni, Ebezi,
21 利篾、隱‧干寧、隱‧哈大、伯‧帕薛;
Remethi, Enganimu, Enihada, na Bethipazezi.
22 又達到他泊、沙哈洗瑪、伯‧示麥,直通到約旦河為止,共十六座城,還有屬城的村莊。
Mpaka wao ulifika Tabor, Shahazuma, na Bethi Shemeshi, na ukakomea katika Yordani. Ilikuwa ni miji kumi na sita, pamoja na vijiji vyake.
23 這些城並屬城的村莊就是以薩迦支派按着宗族所得的地業。
Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Isakari, na walipewa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
24 為亞設支派,按着宗族,拈出第五鬮。
Upigaji wa kura ya tano uliangukia kwa kabila la Asheri, na walipewa kwa koo zao.
25 他們的境界是黑甲、哈利、比田、押煞、
Eneo lao lilijumuisha miji ya Helikathi, Hali, Beteni, Akashafu,
26 亞拉米勒、亞末、米沙勒;往西達到迦密,又到希曷‧立納,
Alameleki, Amadi, na Mshali. Mpaka wa magharibi ulitanuka hadi Karmeli na Shihori Libnathi.
27 轉向日出之地,到伯‧大袞,達到細步綸;往北到伊弗他‧伊勒谷,到伯‧以墨和尼業,也通到迦步勒的左邊;
Kisha ulizunguka upande wa mashariki kueleka Bethi Dagoni na ukaenda hadi Zabuloni, na kisha ukafika katika bonde la ifutaheli, upande wa kaskazini mwa Bethemeki na Neieli. Baadaye uliendelea mbele hata Kabuli kueleka upande wa Kaskazini.
28 又到義伯崙、利合、哈們、加拿,直到西頓大城;
Na kisha ulienda hadi Ebroni, Rehobu, Hammoni, na Kana, hata kufika mji mkubwa wa Sidoni.
29 轉到拉瑪和堅固城泰爾;又轉到何薩,靠近亞革悉一帶地方,直通到海;
Mpaka ulirudi nyuma kuelekea Rama, na kisha ukafika kwenye mji wa Tiro uliokuwa na ngome. Baada ya hapo mpaka ulizunguka kuelekea Hosa na ulikomea katika bahari, katika mkoa wa Akizibu,
30 又有烏瑪、亞弗、利合,共二十二座城,還有屬城的村莊。
Umma, Afeki, na Rehobu. Kulikuwa na miji ishirini na miwili, pamoja na vijiji vyake.
31 這些城並屬城的村莊就是亞設支派按着宗族所得的地業。
Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Asheri, na waliopewa kwa koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
32 為拿弗他利人,按着宗族,拈出第六鬮。
Upigaji wa kura wa mara ya sita uliangukia kwa kabila la Nafutali, na walipewa kufuatana na koo zao.
33 他們的境界是從希利弗從撒拿音的橡樹,從亞大米‧尼吉和雅比聶,直到拉共,通到約旦河;
Mpaka wao ulianzia Helefu, kutoka katika mwaloni huko Zaananimu, ulipanda hadi Adaminekebu na Yabneeli, umbali kama Lakumu; na ulikomea katka Yordani.
34 又轉向西到亞斯納‧他泊,從那裏通到戶割,南邊到西布倫,西邊到亞設,又向日出之地,達到約旦河那裏的猶大。
Mpaka ule ulizunguka upande wa magharibi kuelekea Aznothi Tabori na ulipanda hadi Hukoki; uligusa Zabuloni katika upande wa kusini, na ulifika hata Asheri katika upande wa magharibi, na Yuda katika upande wa mashariki huko katika mto Yordani.
35 堅固的城就是:西丁、側耳、哈末、拉甲、基尼烈、
Miji yenye ngome ilikuwa ni Zidimu, Zeri, Hammathi, Rakathi, Kinnerethi,
36 亞大瑪、拉瑪、夏瑣、
Adama, Rama, Hazori,
37 基低斯、以得來、隱‧夏瑣、
Kedeshi, Edrei, na Eni Hazori.
38 以利穩、密大‧伊勒、和璉、伯‧亞納、伯‧示麥,共十九座城,還有屬城的村莊。
Pia kulikuwa na miji ya Yironi, Migdaleli, Horemu, Bethi Anathi, na Bethi Shemeshi. Kulikuwa na miji kumi na tisa, pamoja na vijiji vyake.
39 這些城並屬城的村莊就是拿弗他利支派按着宗族所得的地業。
Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Nafutali, na walipewa miji pamoja na vijiji vyake kufuatana na koo zao.
40 為但支派,按着宗族,拈出第七鬮。
Upigaji wa kura ya saba uliangukia kwa kabila la Dani, na walipewa kufuatana na koo zao.
41 他們地業的境界是瑣拉、以實陶、伊珥‧示麥、
Eneo lao la urithi lilijumuisha miji ya Zora, Eshitaoli, Iri Shemeshi,
42 沙拉賓、亞雅崙、伊提拉、
Shaalabini, Aijaloni, na Ithila.
43 以倫、亭拿他、以革倫、
Vile vile lilijumuisha miji ya Eloni, Timna, Ekroni,
44 伊利提基、基比頓、巴拉、
Eliteke, Gibethoni, Baalathi,
45 伊胡得、比尼‧比拉、迦特‧臨門、
Yehudi, Bene - Beraki, Gathi Rimoni,
46 美‧耶昆、拉昆,並約帕對面的地界。
Me -Yarkoni, na Rakoni sambamba na eneo la karibu na Yopa.
47 但人的地界越過原得的地界;因為但人上去攻取利善,用刀擊殺城中的人,得了那城,住在其中,以他們先祖但的名將利善改名為但。
Ilitokea wakati mpaka wa kabila la Dani ulipowapotea, kabila la Dani waliishambulia Leshemu, wakapigana nao, na wakauteka. Waliua kila mtu kwa upanga, wakauchukua ukawa mali yao, na wakakaa ndani yake. Wakauita mji ule Dani jina la babu yao badala ya Leshemu.
48 這些城並屬城的村莊就是但支派按着宗族所得的地業。
Huu ulikuwa urithi wa kabila la Dani, waliopewa kufuatana na koo zao - miji pamoja na vijiji vyake.
49 以色列人按着境界分完了地業,就在他們中間將地給嫩的兒子約書亞為業,
Walipomaliza kugawana urithi wa nchi, watu wa Israeli walimpa urithi Yoshua mwana wa Nuni kutoka miongoni mwao.
50 是照耶和華的吩咐,將約書亞所求的城,就是以法蓮山地的亭拿‧西拉城,給了他。他就修那城,住在其中。
Kwa amri ya Yahweh walimpatia mji wa Timnathi Sera ambao aliuomba, ulikuwa katika nchi ya milima ya Efraimu. Aliujenga mji na akaishi huko.
51 這就是祭司以利亞撒和嫩的兒子約書亞,並以色列各支派的族長,在示羅會幕門口,耶和華面前,拈鬮所分的地業。這樣,他們把地分完了。
Na huu ndio urithi ambao Eliazari kuhani, na Yoshua mwana wa Nuni, na viongozi wa makabila ya familia za mababu zao miongoni mwa watu wa Israeli, waligawa kwa kupiga kura huko Shilo, mbele za Yahweh katika mlango wa hema la kukutania. Na hivyo wakamaliza kuigawa nchi.

< 約書亞記 19 >