< 約書亞記 13 >

1 約書亞年紀老邁,耶和華對他說:「你年紀老邁了,還有許多未得之地,
Sasa Yoshua alikuwa mzee wakati Yahweh alipomwambia, “Umekuwa mzee, lakini bado kuna nchi kubwa ya kuteka.
2 就是非利士人的全境和基述人的全地。
Nchi iliyosalia ndio hii: mikoa yote ya Wafilisti, na mikoa ile ya Wageshuri,
3 從埃及前的西曷河往北,直到以革倫的境界,就算屬迦南人之地。有非利士人五個首領所管的迦薩人、亞實突人、亞實基倫人、迦特人、以革倫人之地,並有南方亞衛人之地。
(tangu Shihori, iliyoko mashariki mwa Misri, na upande wa kaskazini kuelekea mpaka wa Ekroni, inayofikiriwa kuwa ni mali ya Wakanaani; wafalme watano wa Wafilisti, wale wafalme wa Gaza, Ashidodi, Ashikeloni, Gathi na Ekroni - miliki ya Waavi.
4 又有迦南人的全地,並屬西頓人的米亞拉到亞弗,直到亞摩利人的境界。
Katika upande wa kusini, kulisalia nchi yote ya Wakanaani, na Meara ambayo ni miliki ya Wasidoni, hadi Afeki, hata mpaka wa Waamori;
5 還有迦巴勒人之地,並向日出的全黎巴嫩,就是從黑門山根的巴力‧迦得,直到哈馬口。
nchi ya Wagebali, Lebanoni kuelekea upande wa mapambazuko ya jua, kutoka Baali- Gadi chini ya Mlima Hermoni mpaka Lebo Hamathi.
6 山地的一切居民,從黎巴嫩直到米斯利弗‧瑪音,就是所有的西頓人,我必在以色列人面前趕出他們去。你只管照我所吩咐的,將這地拈鬮分給以色列人為業。
Pia, wenyeji wote wa nchi ya milima kutoka Lebanoni hadi Misrefothi - Maimu, pamoja na watu wa Sidoni. Nitawafukuza mbele ya jeshi la Israeli. Uwe na uhakika wa kuwapa Waisraeli nchi kama urithi, kama nilivyokuagiza.
7 現在你要把這地分給九個支派和瑪拿西半個支派為業。」
Igawanye nchi hii kama urithi kwa makabila tisa na kwa nusu ya kabila la Manase.
8 瑪拿西那半支派和呂便、迦得二支派已經受了產業,就是耶和華的僕人摩西在約旦河東所賜給他們的:
Pamoja na nusu nyingine ya kabila la Manase, Wareubeni na Wagadi wamekwisha kupokea urithi wao ambao Musa aliwapa katika upande wa mashariki wa Yordani,
9 是從亞嫩谷邊的亞羅珥和谷中的城,並米底巴的全平原,直到底本,
kutoka Aroeri, iliyo katika ukingo wa bonde la mto Arnoni (kujumuisha na mji ambao uko katikati ya bonde), kwa nyanda zote za Medeba hadi Diboni;
10 和在希實本作王亞摩利王西宏的諸城,直到亞捫人的境界;
miji yote ya Sihoni, mfalme wa Waamori, ambaye alitawala katika Heshiboni, hata mpaka wa Waamori,
11 又有基列地、基述人、瑪迦人的地界,並黑門全山、巴珊全地,直到撒迦;
Gileadi na mkoa wa Wageshuri na Maakathi, mlima wote wa Hermoni, Bashani yote mpaka Saleka;
12 又有巴珊王噩的全國-他在亞斯他錄和以得來作王(利乏音人所存留的只剩下他)。這些地的人都是摩西所擊殺、所趕逐的。
ufalme wote wa Ogu katika Bashani, aliyetawala katika Ashitarothi na Edrei - hawa ni wale waliosalia katika Refaimu - ambao Musa aliwapiga na kuwafukuzia mbali.
13 以色列人卻沒有趕逐基述人、瑪迦人;這些人仍住在以色列中,直到今日。
Lakini watu wa Israeli hawakuwafukuza Wageshuri wala Wamakathi. Badala yake, Wageshuri na Wamakathi wanaishi miongoni mwa Waisraeli hadi leo.
14 只是利未支派,摩西 沒有把產業分給他們。他們的產業乃是獻與耶和華-以色列上帝的火祭,正如耶和華所應許他們的。
Kabila la Lawi pekee halikupewa urithi na Musa. Urithi wao ni sadaka za Yahweh, Mungu wa Israeli, zilizotolewa kwa moto, kama Mungu alivyomwagiza Musa.
15 摩西按着呂便支派的宗族分給他們產業。
Musa aliwapa urithi kabila la Rubeni, ukoo kwa ukoo.
16 他們的境界是亞嫩谷邊的亞羅珥和谷中的城,靠近米底巴的全平原;
Miliki yao ilikuwa kutoka Aroeri, juu ya ukingo wa bonde la Mto Arnoni, na mji ulio katikati ya bonde, na nyanda zote za Medeba.
17 希實本並屬希實本平原的各城,底本、巴末‧巴力、伯‧巴力‧勉、
Wareubeni walipata pia Heshiboni, na miji yake yote zilizo katika uwanda, Diboni, na Bamathi Baali, na Bethi Baalimeoni,
18 雅雜、基底莫、米法押、
na Yahazi, na Kedemothi, na Mefaathi,
19 基列亭、西比瑪、谷中山的細列‧哈沙轄、
na Kiriathaimu, na Sibuma, na Zerethishahari juu ya kilima cha bonde.
20 伯‧毗珥、毗斯迦山坡、伯‧耶西末;
Wareubeni walipata pia Bethi Peori, miteremko ya Pisiga, Bethi Yeshimothi,
21 平原的各城,並亞摩利王西宏的全國。這西宏曾在希實本作王,摩西把他和米甸的族長以未、利金、蘇珥、戶珥、利巴擊殺了;這都是住那地屬西宏為首領的。
miji yote ya uwanda, na ufalme wote wa Sihoni, mfalme wa Waamori, ambaye alikuwa ametawala katika Heshiboni, ambaye Musa alikuwa amemshinda pamoja na viongozi wa Midiani, Evi, Rekemu, Zuri, Huri na Reba, wana wa mfalme wa Sihoni, ambao walikuwa wameishi katika nchi.
22 那時以色列人在所殺的人中,也用刀殺了比珥的兒子術士巴蘭。
Pia, watu wa Israeli walimwua kwa upanga Baalam mwana wa Beori, ambaye alifanya mambo ya uaguzi, miongoni mwa wale waliowaua.
23 呂便人的境界就是約旦河與靠近約旦河的地。以上是呂便人按着宗族所得為業的諸城,並屬城的村莊。
Mpaka wa kabila la Rubeni ni Mto Yordani; huu ndio mpaka wao. Huu ulikuwa ni urithi wa kabila la Rubeni, uliotolewa kwa kila ukoo, pamoja na miji na vijiji vyao.
24 摩西按着迦得支派的宗族分給他們產業。
Hiki ndicho Musa alilipa kabila la Gadi, ukoo kwa ukoo:
25 他們的境界是雅謝和基列的各城,並亞捫人的一半地,直到拉巴前的亞羅珥;
Himaya yao ilikuwa Yazeri, miji yote ya Gileadi na nusu ya nchi ya Waamoni, hadi Aroeri, iliyo mashariki mwa Raba,
26 從希實本到拉抹‧米斯巴和比多寧,又從瑪哈念到底璧的境界,
kutoka Heshiboni hadi Ramathi - Mizipe na Betonimu, kutoka Mahanaimu mpaka himaya ya Debiri.
27 並谷中的伯‧亞蘭、伯‧寧拉、疏割、撒分,就是希實本王西宏國中的餘地,以及約旦河與靠近約旦河的地,直到基尼烈海的極邊,都在約旦河東。
Katika bonde, Musa aliwapa Bethi -Haramu, Bethi - Nimra, Sukothi, na Zafoni, ufalme uliobakia wa Sihoni mfalme wa Heshiboni, pamoja na Yordani kama mpaka, katika sehemu za chini za mwisho wa Bahari ya Kinerethi, upande wa mashariki ng'ambo ya Yordani.
28 以上是迦得人按着宗族所得為業的諸城,並屬城的村莊。
Huu ni urithi wa kabila la Gadi, ukoo kwa ukoo, pamoja na miji na vijiji vyao.
29 摩西把產業分給瑪拿西半支派,是按着瑪拿西半支派的宗族所分的。
Musa aliwapa urithi nusu ya kabila la Manase. Urithi uligawiwa kwa nusu ya kabila la watu wa Manase kutokana na kabila zao.
30 他們的境界是從瑪哈念起,包括巴珊全地,就是巴珊王噩的全國,並在巴珊、睚珥的一切城邑,共六十個。
Miliki yao ilikuwa kutoka Mahanaimu, Bashani yote, ufalme wote wa mfalme Ogu wa Bashani, na miji yote ya Yairi, iliyo katika Bashani, miji sitini;
31 基列的一半,並亞斯他錄、以得來,就是屬巴珊王噩國的二城,是按着宗族給瑪拿西的兒子瑪吉的一半子孫。
nusu ya Gileadi, na Ashitarothi na Edrei (miji ya kifalme ya Ogu katika Bashani). Miji hii iligawanywa kwa ukoo wa Makiri mwana wa Manase -nusu ya watu wa Makiri, walipewa kwa kila familia zao.
32 以上是摩西在約旦河東對着耶利哥的摩押平原所分給他們的產業。
Huu ndio urithi ambao Musa aliowagawia katika nyanda za Moabu, ng'ambo ya Yordani mashariki mwa Yeriko.
33 只是利未支派,摩西沒有把產業分給他們。耶和華-以色列的上帝是他們的產業,正如耶和華所應許他們的。
Musa hakulipa urithi kabila la Lawi. kwa kuwa Yahweh, Mungu wa israeli, ni urithi wao, kama vile alivyowaambia.

< 約書亞記 13 >