< 約伯記 41 >

1 你能用魚鉤釣上鱷魚嗎? 能用繩子壓下牠的舌頭嗎?
Je waweza kumvua mamba kwa ndoano ya samaki? Au kumfunga taya zake kwa kamba?
2 你能用繩索穿牠的鼻子嗎? 能用鉤穿牠的腮骨嗎?
Je waweza kuweka kamba katika pua zake, au kumtoboa taya yake kwa ndoano?
3 牠豈向你連連懇求, 說柔和的話嗎?
Je atafanya maombi mengi kwako? Je atazungumza na wewe kwa maneno laini?
4 豈肯與你立約, 使你拿牠永遠作奴僕嗎?
Je atafanya agano na wewe, ili kwamba umchukue kwa ajili ya mtumishi milele?
5 你豈可拿牠當雀鳥玩耍嗎? 豈可為你的幼女將牠拴住嗎?
Je utacheza pamoja naye kama ambavyo ungecheza na ndege? Je utamfunga kwa ajili ya mtumishi wako wa kike?
6 搭夥的漁夫豈可拿牠當貨物嗎? 能把牠分給商人嗎?
Je makundi ya wavuvi waweza kumfanyia biashara? Je watamgawanya ili kufanya biashara miongoni mwa wafanya biashara?
7 你能用倒鉤槍扎滿牠的皮, 能用魚叉叉滿牠的頭嗎?
Je waweza kuijaza ngozi yake kwa vyusa au kichwa chake kwa mikuki ya kuvulia?
8 你按手在牠身上,想與牠爭戰, 就不再這樣行吧!
Weka mkono wako juu yake mara moja, nawe utaikumbuka vita na hautaendelea kufanya hivyo tena.
9 人指望捉拿牠是徒然的; 一見牠,豈不喪膽嗎?
Tazama, matumaini ya kila mtu ambaye hufanya hivyo ni uongo; je si kila mmoja atatupwa chini katika nchi mbele yake?
10 沒有那麼兇猛的人敢惹牠。 這樣,誰能在我面前站立得住呢?
Hakuna aliye mkali ambaye aweza kuthubutu kumtikisa mamba; Ni nani basi awezaye kusimama mbele yake?
11 誰先給我甚麼,使我償還呢? 天下萬物都是我的。
Ni nani kwanza aliyenipa kitu chochote ili kwamba niweze kumlipa? Chochote kilicho chini ya anga ni changu.
12 論到鱷魚的肢體和其大力,並美好的骨骼, 我不能緘默不言。
Sitanyamaza kimya kuhusu miguu ya mamba, wala kuhusu jambo linalohusu nguvu zake, wala kuhusu umbo lake zuri.
13 誰能剝牠的外衣? 誰能進牠上下牙骨之間呢?
Nani awezaye kuiondoa ngozi yake? Nani anaweza kumchoma kwa silaha mara mbili?
14 誰能開牠的腮頰? 牠牙齒四圍是可畏的。
Nani awezaye kuifungua milango ya uso wake, imezungukwa na meno yake ambayo yanaogofya?
15 牠以堅固的鱗甲為可誇, 緊緊合閉,封得嚴密。
Mgongo wake umefanywa kwa magamba yenye mistari, yamefungwa kwa pamoja kama chapa.
16 這鱗甲一一相連, 甚至氣不得透入其間,
Moja li karibu na jingine na ya kuwa hakuna hewa inaweza kupita katikati yake.
17 都是互相聯絡、膠結, 不能分離。
Yameunganishwa moja kwa jingine; yamegandamana kwa pamoja, ili kwamba hayawezi kutenganishwa.
18 牠打噴嚏就發出光來; 牠眼睛好像早晨的光線。
Mwanga hung'ara kutoka katika kupumua kwake; macho yake ni kama kope za mapambazuko ya asubuhi.
19 從牠口中發出燒着的火把, 與飛迸的火星;
Ndani ya mdomo wake hutoka miali ya mwanga, chembe za moto huruka nje.
20 從牠鼻孔冒出煙來, 如燒開的鍋和點着的蘆葦。
Katika pua zake hutoka moshi kama chungu kinachotokota juu ya moto ambao umechochewa ili uwe na joto sana.
21 牠的氣點着煤炭, 有火焰從牠口中發出。
Pumzi yake huwasha mkaa na kuwa mwali; moto hutoka katika mdomo wake.
22 牠頸項中存着勁力; 在牠面前的都恐嚇蹦跳。
Katika shingo yake kuna nguvu, na kitisho hucheza mbele yake.
23 牠的肉塊互相聯絡, 緊貼其身,不能搖動。
Nofu za mwili wake zimeunganishwa pamoja; ziko imara katika yeye; wala haziwezi kuondolewa.
24 牠的心結實如石頭, 如下磨石那樣結實。
Moyo wake ni mgumu kama jiwe - hakika, ni mgumu kama jiwe la chini la kusagia.
25 牠一起來,勇士都驚恐, 心裏慌亂,便都昏迷。
Na anaposimama mwenyewe, hata miungu huogopa; hurudi nyuma kwasababu ya hofu.
26 人若用刀,用槍,用標槍, 用尖槍扎牠,都是無用。
Na ikiwa atapigwa kwa upanga, hauwezi kumfanya kitu chochote, wala mkuki, wala mshale, wala aina yoyote ya silaha iliyochongoka.
27 牠以鐵為乾草, 以銅為爛木。
Yeye hufikiri juu ya chuma kana kwamba ni majani makavu na hufikiri juu ya fedha kana kwamba ni ubao uliooza.
28 箭不能恐嚇牠使牠逃避; 彈石在牠看為碎稭。
Mshale hauwezi akamfanya akimbie; kwake yeye mawe ya kombeo huwa kama makapi.
29 棍棒算為禾稭; 牠嗤笑短槍颼的響聲。
Marungu huyaangalia kama majani makavu; yeye hucheka juu ya mkuki unaovuma.
30 牠肚腹下如尖瓦片; 牠如釘耙經過淤泥。
Sehemu zake za chini zi kama vipande vilivyochongoka vya vyungu; huacha alama zilizosambaa katika udongo kana kwamba alikuwa ni chombo cha kusagia.
31 牠使深淵開滾如鍋, 使洋海如鍋中的膏油。
Yeye hukifanya kilindi kichemke kama chungu cha maji ya moto; huifanya bahari kama chungu cha lihamu.
32 牠行的路隨後發光, 令人想深淵如同白髮。
Yeye huifanya njia ing'are nyuma yake; mtu mmoja angedhani kilindi kuwa cheupe.
33 在地上沒有像牠造的那樣, 無所懼怕。
Hakuna cha kumlinganisha juu ya dunia, ambaye yeye alikuwa ameumbwa kuishi pasipo hofu.
34 凡高大的,牠無不藐視; 牠在驕傲的水族上作王。
Hukiona kila kitu chenye kiburi; yeye ni mfalme juu ya wana wote wa kiburi.”

< 約伯記 41 >