< 約伯記 34 >
Zaidi ya hayo, Elihu aliendelea kusema:
2 你們智慧人要聽我的話; 有知識的人要留心聽我說。
“Sikilizeni maneno yangu, ninyi watu wenye hekima; nisikieni, ninyi mlio na maarifa.
Kwa kuwa sikio huyajaribu maneno kama ambavyo kaakaa huonja chakula.
Na tujichagulie sisi wenyewe yale yenye adili: na tujigundulie miongoni mwetu yale yaliyo mazuri.
Kwa kuwa Ayubu amesema, 'mimi ni mwenye haki, lakini Mungu ameondoa haki zangu.
6 我雖有理,還算為說謊言的; 我雖無過,受的傷還不能醫治。
Pamoja na haki zangu, ninaangaliwa kama mwongo. Kidonda changu hakiponyeki, ingawa mimi sina dhambi.'
Ni mtu gani aliye kama Ayubu ambaye hunywa dharau kama maji,
ambaye huzunguka katika ushirika wa watu ambao ni waovu, na ambaye hutembea pamoja na watu waovu?
Kwa kuwa anasema, ' Hakuna faida kwa mtu kujifurahisha kwa kufanya mambo ambayo Mungu anayataka.'
10 所以,你們明理的人要聽我的話。 上帝斷不致行惡; 全能者斷不致作孽。
Basi nisikilizeni mimi, enyi watu wenye ufahamu: na iwe mbali na Mungu kwamba atatenda uovu;
11 他必按人所做的報應人, 使各人照所行的得報。
na iwe mbali na Mwenye enzi kwamba atatenda dhambi. Kwa kuwa humlipa mtu kutokana na kazi yake; na humfanya mtu apate thawabu za njia zake mwenyewe.
Kwa hakika, Mungu hatendi uovu, wala Mwenye nguvu hajaIpotosha haki.
Ni nani aliyemweka kuwa mtawala wa dunia? Ni nani aliyeiweka dunia yote chini yake?
Ikiwa aliweka makusudio yake juu yake mwenyewe, na kama amejikusanyia mwenyewe nafsi yake na pumzi yake,
basi miili yote itateketea pamoja; mwanadamu angerudi mavumbini tena.
16 你若明理,就當聽我的話, 留心聽我言語的聲音。
Kama sasa mna ufahamu, sikilizeni haya; sikilizeni sauti ya maneno yangu.
17 難道恨惡公平的可以掌權嗎? 那有公義的、有大能的,豈可定他有罪嗎?
Je yeye anayeichukia haki aweza kutawala? Je mtamhukumu Mungu kuwa ni mwenye makosa, ambaye ni mwenye haki na mwenye nguvu?
18 他對君王說:你是鄙陋的; 對貴臣說:你是邪惡的。
Mungu ambaye humwambia mfalme, ' Wewe ni mbaya; au huwaambia wenye kuheshimiwa, 'Ninyi ni waovu'?
19 他待王子不徇情面, 也不看重富足的過於貧窮的, 因為都是他手所造。
Mungu ambaye haoneshi upendeleo kwa viongozi na ambaye hawakubali zaidi watu matajiri kuliko masikini, kwa kuwa wote ni kazi ya mikono yake.
20 在轉眼之間,半夜之中, 他們就死亡。 百姓被震動而去世; 有權力的被奪去非借人手。
Watakufa kwa muda mfupi; wakati wa usiku watu watatikiswa na watapita; watu wenye nguvu watatwaliwa mbali, lakini si kwa mikono ya wanadamu.
Kwa kuwa macho ya Mungu yako juu ya njia za mtu; anaziona hatua zake zote.
Hakuna giza, wala hakuna weusi mzito ambao watenda mabaya wanaweza kujificha wao wenyewe.
Kwa kuwa Mungu hahitaji kumchunguza mtu zaidi; wala hakuna haja kwa mtu yeyote kwenda mbele zake kwa hukumu.
24 他用難測之法打破有能力的人, 設立別人代替他們。
Huwavunja vipande vipande watu wenye nguvu kwa ajili ya njia zao ambazo hazihitaji uchunguzi zaidi; huwaweka watu wengine katika nafasi zao.
25 他原知道他們的行為, 使他們在夜間傾倒滅亡。
Kwa namna hii ana maarifa juu ya matendo yao; huwatupa watu hawa wakati wa usiku; nao wameangamizwa.
Huwaua kwa matendo yao mabaya kama wakosaji dhahiri mbele za watu wengine
kwasababu wamegeuka na kuacha kumfuata yeye na wamekataa kuzisadiki njia zake zozote.
28 甚至使貧窮人的哀聲達到他那裏; 他也聽了困苦人的哀聲。
Na kwa namna hii, wamekifanya kilio cha watu masikini kimfikie; amekisikia kilio cha watu walioteswa.
29 他使人安靜,誰能擾亂呢? 他掩面,誰能見他呢? 無論待一國或一人都是如此-
Na wakati akaapo kimya, nani aweza kumhukumu kuwa mkosaji? Kama akiuficha uso wake, ni nani awezaye kumjua? Anatawala sawa sawa juu ya taifa na mtu pia,
ili kwamba watu wasiomjua Mungu wasije wakatawala, ili kwamba asiwepo mtu wa kuwanasa watu.
Fikiria mtu akimwambia Mungu, ' Mimi ni mwenye hatia kabisa, lakini sitatenda dhambi tena;
32 我所看不明的,求你指教我; 我若作了孽,必不再作?
nifunze kile ambacho siwezi kukiona; nimetenda dhambi, lakini sitafanya tena.'
33 他施行報應, 豈要隨你的心願、叫你推辭不受嗎? 選定的是你,不是我。 你所知道的只管說吧!
Je unadhani kwamba Mungu ataiadhibu dhambi ya mtu huyo, kwa kuwa unayachukia yale ambayo Mungu huyatenda? Ni lazima uchague, siyo mimi. Basi sema yale ambayo unayajua.
Watu wenye ufahamu wataniambia, kwa kweli, kila mtu mwenye hekima ambaye hunisikia atasema,
Ayubu anazungumza bila maarifa; maneno yake hayana hekima.'
Kama Ayubu alijaribiwa kwa kitu kidogo kabisa katika kesi yake kwasababu ya kuongea kwake kama watu waovu.
37 他在罪上又加悖逆; 在我們中間拍手, 用許多言語輕慢上帝。
Kwa kuwa anaongeza uasi juu ya dhambi yake; anapiga makofi ya dharau kati yetu; anaweka maneno kinyume na Mungu.”