< 約伯記 32 >

1 於是這三個人,因約伯自以為義就不再回答他。
Hivyo hawa watu watatu walikoma kumjibu Ayubu kwasababu alikuwa ni mwenye haki katika macho yake mwenyewe.
2 那時有布西人蘭族巴拉迦的兒子以利戶向約伯發怒;因約伯自以為義,不以上帝為義。
Ndipo iliwaka hasira ya Elihu mwana wa Barakeli Mbuzi, wa familia ya Ramu, iliwaka dhidi ya Ayubu kwa kuwa alijihesabia haki mwenyewe kuliko Mungu.
3 他又向約伯的三個朋友發怒;因為他們想不出回答的話來,仍以約伯為有罪。
Hasira ya Elihu iliwaka pia kinyume cha marafiki zake watatu kwasababu hawakupata jibu kwa ajili ya Ayubu, na bado walimhukumu Ayubu.
4 以利戶要與約伯說話,就等候他們,因為他們比自己年老。
Sasa Elihu alikuwa amemsubiri Ayubu ili aweze kuzungumza naye kwa kuwa watu wengine walikuwa wakubwa kuliko yeye.
5 以利戶見這三個人口中無話回答,就怒氣發作。
Hata hivyo, wakati Elihu alipoona ya kuwa hapakuwa na jibu katika midomo ya watu hawa watatu, hasira yake iliwaka.
6 布西人巴拉迦的兒子以利戶回答說: 我年輕,你們老邁; 因此我退讓,不敢向你們陳說我的意見。
Ndipo Elihu mwana wa Barakeli Mbuzi alinena na kusema, “Mimi ni mdogo, na ninyi ni wazee. Hii ndio sababu nilijizuia na sikuthubutu kuzungumza mawazo yangu mwenyewe.
7 我說,年老的當先說話; 壽高的當以智慧教訓人。
Nilisema, “Urefu wa siku utazungumza; na wingi wa miaka utatufundisha hekima.
8 但在人裏面有靈; 全能者的氣使人有聰明。
Lakini kuna roho ndani ya mtu; pumzi ya Mwenye nguvu humpa yeye ufahamu.
9 尊貴的不都有智慧; 壽高的不都能明白公平。
Si tu watu wakubwa ndio wenye hekima, wala watu wazee pekee ambao hufahamu haki.
10 因此我說:你們要聽我言; 我也要陳說我的意見。
Hivyo basi nakwambia wewe, “Nisikilizeni mimi; Nitakwambia pia uelewa wangu.'
11 你們查究所要說的話; 那時我等候你們的話, 側耳聽你們的辯論,
Tazama, niliyasubiria maneno yenu; nilisikiliza hoja zenu wakati mlipokuwa mnafikiri juu ya kile cha kusema.
12 留心聽你們; 誰知你們中間無一人折服約伯, 駁倒他的話。
Hakika, niliwajali sana ninyi, lakini, tazama, hakuna hata mmoja wenu aliyeweza kumshawishi Ayubu wala ambaye aliweza kumjibu maneno yake.
13 你們切不可說:我們尋得智慧; 上帝能勝他,人卻不能。
Iweni waangalifu msije mkasema, 'Tumepata hekima!' Mungu atakuwa amemshinda Ayubu; mtu wa kawaida hawezi akafanya hivyo.
14 約伯沒有向我爭辯; 我也不用你們的話回答他。
Kwa kuwa Ayubu hajasema mojamoja maneno yake juu yangu, basi sitamjibu kwa maneno yenu.
15 他們驚奇不再回答, 一言不發。
Hawa watu watatu wamep igwa bumbuwazi; hawawezi kuendelea kumjibu Ayubu; hawana neno zaidi la kusema.
16 我豈因他們不說話, 站住不再回答,仍舊等候呢?
Je ninapaswa kusubiria kwasababu hawazungumzi, kwa kuwa wamesimama pale kimya na wala hawajibu zaidi?
17 我也要回答我的一分話, 陳說我的意見。
La, nitajibu pia upande wangu; Nitawaambia pia ufahamu wangu.
18 因為我的言語滿懷; 我裏面的靈激動我。
Kwa kuwa nimejawa na maneno mengi, roho ndani yangu inanisukuma.
19 我的胸懷如盛酒之囊沒有出氣之縫, 又如新皮袋快要破裂。
Tazama, kifua changu ni kama divai yenye chachu ambayo haina tundu; kama viriba vipya, kiko tayari kupasuka.
20 我要說話,使我舒暢; 我要開口回答。
Nitazungumza ili kwamba niweze kuburudishwa; nitafungua kimya changu na kusema.
21 我必不看人的情面, 也不奉承人。
Sitaonesha upendeleo; wala sitatoa sifa za majina kwa mtu yeyote.
22 我不曉得奉承; 若奉承,造我的主必快快除滅我。
Kwa kuwa sijui namna ya kutoa sifa; kama nitafanya hivyo, Muumba wangu atanikatilia mimi mbali.

< 約伯記 32 >