< 耶利米書 36 >
1 猶大王約西亞的兒子約雅敬第四年,耶和華的話臨到耶利米說:
Ilikuja tokea katika mwaka wa nne wa Yehoyakimu mwana wa Yosiah mfalme wa Yuda, kwamba neno hili lilikuja kwa Yeremiah kutoka kwa Yahwe, na alisema,
2 「你取一書卷,將我對你說攻擊以色列和猶大,並各國的一切話,從我對你說話的那日,就是從約西亞的日子起直到今日,都寫在其上。
“Chukua kitabu kwa ajili yako na uandike juu yake maneno yote ambayo nimekwisha kukuambia kuhusiana na Israel na Yuda, na kila taifa. Fanya hivi kwa kila kitu nilichokuambia tokea siku za Yosia mpaka siku ile.
3 或者猶大家聽見我想要降與他們的一切災禍,各人就回頭,離開惡道,我好赦免他們的罪孽和罪惡。」
Huenda watu wa Yuda watasikiliza majanga yote ambayo ninakusudia kuleta juu yao. Huenda kila mmoja ataacha njia zake mbaya, ili kwamba niweze kuwasamehe maovu yao na dhambi zao.”
4 所以,耶利米召了尼利亞的兒子巴錄來;巴錄就從耶利米口中,將耶和華對耶利米所說的一切話寫在書卷上。
Kisha Yeremia alimwita Baruku mwana wa Neria, na Baruku aliandika kwenye kitabu, kwa imla ya Yeremia, maneno yote ya Yahwe yalizunguzwa kwake.
5 耶利米吩咐巴錄說:「我被拘管,不能進耶和華的殿。
Kisha Yeremia alitoa amri kwa Baruku. Alisema, “Niko gerezani na siwezi kwenda kwenye nyumba ya Yahwe.
6 所以你要去趁禁食的日子,在耶和華殿中將耶和華的話,就是你從我口中所寫在書卷上的話,念給百姓和一切從猶大城邑出來的人聽。
Kwa hiyo unapaswa uende na kusoma kutoka kwenye kitabu ulichoandika kwa imla yangu. Kwa siku ya kufunga, unapaswa usome maneno ya Yahwe kwenye masikio ya watu katika nyumba yake, na pia kwenye masikio ya Yuda yote waliokuja kutoka katika miji yao. Tangaza maneno haya kwao.
7 或者他們在耶和華面前懇求各人回頭,離開惡道,因為耶和華向這百姓所說要發的怒氣和忿怒是大的。」
Huenda maombi yao ya rehema yatakuja mbele ya Yahwe. Huenda kila mtu ataacha njia mbaya, kwani gathabu na hasira ya Yahwe imetangazwa dhidi ya watu kwa ukali.”
8 尼利亞的兒子巴錄就照先知耶利米一切所吩咐的去行,在耶和華的殿中從書上念耶和華的話。
Kwa hiyo Baruku mwana wa Neria alifanya kila kitu ambacho Yeremia nabii alimwamuru yeye kufanya. Alisoma kwa sauti maneno ya Yahwe ndani mwa nyumba ya Yahwe.
9 猶大王約西亞的兒子約雅敬第五年九月,耶路撒冷的眾民和那從猶大城邑來到耶路撒冷的眾民,在耶和華面前宣告禁食的日子,
Ilikuja tokea katika mwaka wa tano na mwezi wa tisa kwa Yehoyakimu mwana wa Yosia, mfalme wa Yuda, kwamba watu wote Yerusalemu na watu waliotoka Yerusalemu toka miji ya Yuda walitangaza kufunga kwa kumheshimu Yahwe.
10 巴錄就在耶和華殿的上院,耶和華殿的新門口,沙番的兒子文士基瑪利雅的屋內,念書上耶利米的話給眾民聽。
Baruku alisoma kwa sauti maneno ya Yeremia katika nyumba ya Yahwe, kutoka kwenye chumba cha Gamaria mwana wa Shafani mwandishi, katika ua wa juu, kwa mlango wa kuingilia wa nyumba ya Yahwe. Alifanya hivi kwa masikio ya watu wote.
11 沙番的孫子、基瑪利雅的兒子米該亞聽見書上耶和華的一切話,
Basi Mikaya mwana wa Gemaria alisikia maneno yote ya Yahwe kwenye kitabu.
12 他就下到王宮,進入文士的屋子。眾首領,就是文士以利沙瑪、示瑪雅的兒子第萊雅、亞革波的兒子以利拿單、沙番的兒子基瑪利雅、哈拿尼雅的兒子西底家,和其餘的首領都坐在那裏。
Alienda chini kwenye nyumba ya mfalme, kwenye chumba cha katibu. Tazama, maafisa wote walikuwa wamekaa hapo: Elishama mwandishi, Delaiah mwana wa Shemaiah, Elnathan mwana wa Achbor, Gemaria mwana wa Shefani, na Sedekia mwana wa Hananiah, na maafisa wote.
13 於是米該亞對他們述說他所聽見的一切話,就是巴錄向百姓念那書的時候所聽見的。
Kisha Mikaya alitoa taarifa ya maneno yote kwao ambayo alikuwa amesikia ambayo Baruku alisoma kwa sauti kwenye masikio ya watu.
14 眾首領就打發古示的曾孫、示利米雅的孫子、尼探雅的兒子猶底到巴錄那裏,對他說:「你將所念給百姓聽的書卷拿在手中到我們這裏來。」尼利亞的兒子巴錄就手拿書卷來到他們那裏。
Kwa hiyo maafisa wote walimtuma Jehudi mwana wa Nethania mwana wa Shelemiah mwana wa Kushi, kwa Baruku. Jehudi alisema kwa Baruku, “Chukua kitabu katika mkono wako, kitabu ambacho ulikuwa unakisoma kwa masikio ya watu and kuja.” Kwa hiyo Baruku mwana wa Neria alichukua kitabu katika mkono wake na alienda kwa maafisa.
15 他們對他說:「請你坐下,念給我們聽。」巴錄就念給他們聽。
Kisha walisema naye,”Kaa chini na usome haya katika masikio yetu.” Kwa hiyo Baruku akasoma kitabu.
16 他們聽見這一切話就害怕,面面相觀,對巴錄說:「我們必須將這一切話告訴王。」
Ilitokea wakati waliposikia haya maneno yote, kila mtu alipatwa na hofu kwa mtu aliye karibu naye na kusema kwa Baruku, “Kwa hakika tunapaswa kutoa taarifa ya maneno haya yote kwa mfalme.”
17 他們問巴錄說:「請你告訴我們,你怎樣從他口中寫這一切話呢?」
Kisha walimuuliza Baruku, “Tuambie, ulipataje kuandika maneno yote haya kwa imla ya Yeremia?”
18 巴錄回答說:「他用口向我說這一切話,我就用筆墨寫在書上。」
Baruku aliwaambia, “Alitoa imla ya maneno haya yote kwangu, na nikayaandika kwa wino kwenye kitabu hiki.”
19 眾首領對巴錄說:「你和耶利米要去藏起來,不可叫人知道你們在哪裏。」
Kisha maafisa walisema kwa Baruku, “Nenda, jifiche mwenyewe, na Yeremiah, pia. Usipatikane mtu yeyote kujua uko wapi.”
20 眾首領進院見王,卻先把書卷存在文士以利沙瑪的屋內,以後將這一切話說給王聽。
Kisha walienda kwa uwanja wa mfalme na wakatoa taarifa ya maneno haya kwake. Lakini kwanza walikihifadhi kitabu kwenye chumba cha katibu Elishama.
21 王就打發猶底去拿這書卷來,他便從文士以利沙瑪的屋內取來,念給王和王左右侍立的眾首領聽。
Basi mfalme alimtuma Yehudi kuchukua kitabu. Yehudi alikichukua toka chumba cha Elishama katibu. Kisha alikisoma kwa sauti kwa mfalme na wote maafisa walikuwa wamesimama karibu naye.
22 那時正是九月,王坐在過冬的房屋裏,王的前面火盆中有燒着的火。
Sasa mfalme alikuwa amesimama kwenye nyumba ya majira ya baridi katika mwezi wa tisa, na mkaa ulikuwa unawaka mbele yake.
23 猶底念了三四篇,王就用文士的刀將書卷割破,扔在火盆中,直到全卷在火中燒盡了。
Ilitokea wakati Yehudi aliposoma kurusa tatu au nne, mfalme angeweza kuikata kwa kisu na kuitupa kwenye moto katika mkaa mpaka kitabu chote kiliteketea.
24 王和聽見這一切話的臣僕都不懼怕,也不撕裂衣服。
Lakini wala mfalme wala yeyote wa mjakazi wake aliyesikia haya maneno yote aliogopa, wala hawakuchana nguo zao.
25 以利拿單和第萊雅,並基瑪利雅懇求王不要燒這書卷,他卻不聽。
Elnathani, Delaya, na Gemaria walikuwa wamemuomba mfalme asikichome kitabu, lakini hakuwasikiliza.
26 王就吩咐哈米勒的兒子耶拉篾和亞斯列的兒子西萊雅,並亞伯疊的兒子示利米雅,去捉拿文士巴錄和先知耶利米。耶和華卻將他們隱藏。
Basi mfalme alimwamuru Yerameeli, ndugu, Seraya mwana wa Azrieli, na Shelemia mwana wa Abdeeli kumfunga Baruku mwandishi na Yeremia nabii, lakini Yahwe alikuwa amewaficha.
27 王燒了書卷(其上有巴錄從耶利米口中所寫的話)以後,耶和華的話臨到耶利米說:
Kisha neno la Yahwe lilikuja kwa Yeremia baada ya mfalme kuwa amechoma kitabu na maneno ya Baruku yaliyokuwa yameandikwa kwa imla ya Yeremia, na alisema,
28 「你再取一卷,將猶大王約雅敬所燒第一卷上的一切話寫在其上。
“Rudi, chukua kitabu kingine kwa ajili yako, na uandike maneno haya yote ambayo yalikuwa kwenye kitabu cha kwanza, ambacho Yehoyakimu mfalme wa Yuda alikichoma.
29 論到猶大王約雅敬你要說,耶和華如此說:你燒了書卷,說:『你為甚麼在其上寫着,說巴比倫王必要來毀滅這地,使這地上絕了人民牲畜呢?』
Kisha unapaswa kusema hivi kwa mfalme Yehoyakimu mfalme wa Yuda: 'Ulichoma hicho kitabu! Na ulisema: Kwanini umeandika juu yake, “Mfalme wa Babeli hakika atakuja na kuharibu nchi hii, kwa kuwa atawaangamiza wanaume wote na wanyama ndani yake?”
30 所以耶和華論到猶大王約雅敬說:他後裔中必沒有人坐在大衛的寶座上;他的屍首必被拋棄,白日受炎熱,黑夜受寒霜。
Kwa hiyo Yahwe anasema hivi kuhusu wewe, Yehoyakimu mfalme wa Yuda: “Hakuna mzao wako atawahi kukaa kwenye kiti cha Daudi. Kama wewe, maiti yako itatupwa kwenye siku ya joto na usiku wa baridi.
31 我必因他和他後裔,並他臣僕的罪孽刑罰他們。我要使我所說的一切災禍臨到他們和耶路撒冷的居民,並猶大人;只是他們不聽。」
Kwa kuwa nitakuadhibu, wazao wako, na wajakazi wako kwa maovu yenu yote. Nitaleta kwenu, kwa wakazi wote wa Yerusalemu, na kwa kila mtu Yuda majanga ambayo nimewatishia ninyi, lakini kwa hamkuwa makini.”
32 於是,耶利米又取一書卷交給尼利亞的兒子文士巴錄,他就從耶利米的口中寫了猶大王約雅敬所燒前卷上的一切話,另外又添了許多相彷的話。
Kwa hiyo Yeremia alichukua kitabu kingine na akampa Baruku mwana wa Neria mwandishi. Baruku aliandika juu yake kwa imla ya Yeremia maneno yote ambayo yalikuwa katika kitabu kilichochomwa moto na mfalme Yehoyakimu mfalme wa Yuda. Zaidi, maneno mengi ya kufanana yaliongezwa kwenye kitabu hiki.