< 以賽亞書 60 >

1 興起,發光!因為你的光已經來到! 耶和華的榮耀發現照耀你。
Nyanyuka, uangaze; maana mwanga wako umekuja, na utukufu wa Yahwe umekuja kwako.
2 看哪,黑暗遮蓋大地, 幽暗遮蓋萬民, 耶和華卻要顯現照耀你; 他的榮耀要現在你身上。
Japokuwa giza litatanda katika nchi, na giza nene katika mataifa; Lakini Yahwe atakuja juu yenu, na utukufu wake utaonekana kwenu.
3 萬國要來就你的光; 君王要來就你發現的光輝。
Mataifa yatakuja kwenye mwanga wako, na wafalme katika mwanga wako mkali uliokuja
4 你舉目向四方觀看; 眾人都聚集來到你這裏。 你的眾子從遠方而來; 你的眾女也被懷抱而來。
Tazama na angalia pande zote. Wamekusanyika wao wenyewe kwa pamoja na wanakuja kwako. Watoto wako watatoka mbali, na binti zao watabebwa katika mikono yenu.
5 那時,你看見就有光榮; 你心又跳動又寬暢; 因為大海豐盛的貨物必轉來歸你; 列國的財寶也必來歸你。
Halafu wataangalia na kuwa furaha, na moyo wako utafurahia na kufurika, maana wingi wa maji utamwagwa juu yenu, utajiri wa mataifa utakuja kwenu.
6 成群的駱駝, 並米甸和以法的獨峰駝必遮滿你; 示巴的眾人都必來到; 要奉上黃金乳香, 又要傳說耶和華的讚美。
Msafara wa ngamia utawafunika ninyi, na ngamia wa Midiani na Efa; wote watakuja kutoka Sheba; wataleta dhahabu na ubani, wataimba sifa kwa Yahwe.
7 基達的羊群都必聚集到你這裏, 尼拜約的公羊要供你使用, 在我壇上必蒙悅納; 我必榮耀我榮耀的殿。
Makundi yote ya Kedari yatakusanika kwa pamoja kwako, kondoo wa Nebaioti watabeba mahitaji yako; watakubalika kutolewa sadaka katika madhebau yangu; na nitaitukuza nyumba yangu takatifu.
8 那些飛來如雲、 又如鴿子向窗戶飛回的是誰呢?
Ni nani hawa wanopaa wenyewe kama mawingu, na kama njiwa kwenye makazi yao?
9 眾海島必等候我, 首先是他施的船隻, 將你的眾子連他們的金銀從遠方一同帶來, 都為耶和華-你上帝的名, 又為以色列的聖者, 因為他已經榮耀了你。
Pwani itanitafuta mimi, na meli ya Tarshishi huwaongoza, huwaleta watoto wenu kutoka mbali, pamoja na fedha zao na dhahabu zao, maana jina la Yahwe Mungu wenu, na Mtakatifu wa Israeli, maana amekuheshimu wewe.
10 外邦人必建築你的城牆; 他們的王必服事你。 我曾發怒擊打你, 現今卻施恩憐恤你。
Watoto wa wageni watajenga tena kuta zenu, n awafalme wao watawatumikia ninyi; japo katika laana yangu nimewaadhibu ninyi, lakini kwa neema yangu nitawahurumia ninyi.
11 你的城門必時常開放, 晝夜不關; 使人把列國的財物帶來歸你, 並將他們的君王牽引而來。
Milango yenu itaendelea kuwa wazi; haitafungwa mchana au usiku, hivyo utajiri wa mataifa ili uweze kuletwa, pamoja na viongozi wanowaongoza.
12 哪一邦哪一國不事奉你,就必滅亡, 也必全然荒廢。
Kweli, mataifa na falme ambayo hayatakutumikia wewe yatatoweka; mataifa hayo yataangamizwa kabisa.
13 黎巴嫩的榮耀, 就是松樹、杉樹、黃楊樹, 都必一同歸你, 為要修飾我聖所之地; 我也要使我腳踏之處得榮耀。
Utukufu wa Lebanoni utakuja kwako, mti wa msonobari, mtidhari, pamoja na msonobari ili kupamba madhebau yangu; na Nitalitukuza eneo la miguu yangu.
14 素來苦待你的,他的子孫都必屈身來就你; 藐視你的,都要在你腳下跪拜。 他們要稱你為「耶和華的城」, 為「以色列聖者的錫安」。
Watakuja kwako kukusujudia wewe, watoto wa wale wanaokunyenyekea wewe; wataisujudia miguu yako; watakuita wewe mji wa Yahwe, sayani ya Mtakatifu wa Israeli.
15 你雖然被撇棄被厭惡, 甚至無人經過, 我卻使你變為永遠的榮華, 成為累代的喜樂。
Badala yake uwepo wenu umetelekezwa na kuchukiwa, kwa kuwa hakuna hata mmoja anayepita ndani yenu, nitawafanya kuwa kitu cha kiburi milele, furaha kutoka kizazi hata kizazi.
16 你也必吃萬國的奶, 又吃君王的奶。 你便知道我-耶和華是你的救主, 是你的救贖主,雅各的大能者。
Pia utakunywa maziwa ya mataifa, utatunzwa katika kifua cha wafalme; utajua kwamba Mimi Yahwe, Mimi ni mwokozi na mkombozi wenu, aliye Mkuu wa Israeli.
17 我要拿金子代替銅, 拿銀子代替鐵, 拿銅代替木頭, 拿鐵代替石頭; 並要以和平為你的官長, 以公義為你的監督。
Badala ya shaba Nitaleta dhahabu, badaia ya chuma nitaleta fedha; badala ya mbao, shabana badala ya jiwe, chuma. Nitachagua amani kwa kiongozi wenu, na haki kiongozi wenu.
18 你地上不再聽見強暴的事, 境內不再聽見荒涼毀滅的事。 你必稱你的牆為「拯救」, 稱你的門為「讚美」。
Vurugu hazitasikika katika aridhi yenu, uharibifu wala uvunjaji katika mipaka yenu; lakini mtaita kuta zenu wokovu, na malngo yenu mtayaita sifa.
19 日頭不再作你白晝的光; 月亮也不再發光照耀你。 耶和華卻要作你永遠的光; 你上帝要為你的榮耀。
Jua halitakuwa mwanga wenu wakati wa mchana, wala mwanga wa mwenzi wakati wa usiku hautawawakia ninyi; Lakini Yahwe atakuwa mwanga wenu wa milele, na Mungu wenu na utukufu wenu.
20 你的日頭不再下落; 你的月亮也不退縮; 因為耶和華必作你永遠的光。 你悲哀的日子也完畢了。
Jua lenu halitakuewepo wala mweni utaondoshwa na kutoweka; maana Yahwe atakuwa mwanga wenu daima, na siku za maombolezo zitakwisha.
21 你的居民都成為義人, 永遠得地為業; 是我種的栽子,我手的工作, 使我得榮耀。
Watu wako wote watakuwa wenye haki; watachukuwa urithi wa nchi kwa mda wote, tawi la mazao yangu, kazi ya mikono yangu, ili niweze kuitukuza.
22 至小的族要加增千倍; 微弱的國必成為強盛。 我-耶和華要按定期速成這事。
Mtoto atakuwa maelfu, na mdogo atakuwa taifa la wenye nguvu; Mimi Yahwe Nitayatimiza hayo mda utakapowadia.

< 以賽亞書 60 >