< 以賽亞書 35 >

1 曠野和乾旱之地必然歡喜; 沙漠也必快樂; 又像玫瑰開花,
Jangwa na Arabu watafurahia; na jangwa litafurahia na kuchanua. Kama waridi,
2 必開花繁盛, 樂上加樂,而且歡呼。 黎巴嫩的榮耀, 並迦密與沙崙的華美,必賜給它。 人必看見耶和華的榮耀, 我們上帝的華美。
Yatachanua kwa wingi na yatashangilia kwa furaha na nyimbo; litapewa utukufu wa Lebanoni, mapambo ya Karmeli na Sharoni; watauona utukufu wa Yahwe, mapambo ya Mungu wetu.
3 你們要使軟弱的手堅壯, 無力的膝穩固。
Itieni nguvu mikono iliyo dhaifu, na badala ya magoti yanayotingishika.
4 對膽怯的人說: 你們要剛強,不要懼怕。 看哪,你們的上帝必來報仇, 必來施行極大的報應; 他必來拯救你們。
Waambie wenye moyo wa uwoga, ''Wawe imara, wasiogope! Tazama, Mungu wako anakuja na kisasi, kwa ajili ya malipo ya Mungu. Atakuja na kutuokoa.''
5 那時,瞎子的眼必睜開; 聾子的耳必開通。
Halafu macho ya vipofu yataona, na masikio ya viziwi yatasikia.
6 那時,瘸子必跳躍像鹿; 啞巴的舌頭必能歌唱。 在曠野必有水發出; 在沙漠必有河湧流。
Halafu kilema atarukaruka kama kulungu, na ulimi wa bubu utaimba, maana maji yatabubujika Araba, na mifereji jangwani.
7 發光的沙要變為水池; 乾渴之地要變為泉源。 在野狗躺臥之處, 必有青草、蘆葦,和蒲草。
Mchanga ulioungua utakuwa kisima, na aridhi iliyo na kiu itakua chemchem; katika makazi mbweha, pale waliopokuwa wanaishi, kutakuwa na nyasi pamoja na mianzi.
8 在那裏必有一條大道, 稱為聖路。 污穢人不得經過, 必專為贖民行走; 行路的人雖愚昧, 也不致失迷。
Barabara kuu itaitwa Njia takatifu. Wasio safi hawatasifiri kwa kutumia njia hiyo. Lakini itakuwa kwa ajili ya mtu yeyote anayetembea juu yake. Hakuna mjinga atakayeipitia.
9 在那裏必沒有獅子, 猛獸也不登這路; 在那裏都遇不見, 只有贖民在那裏行走。
Hakuna simba pale, wala mnyama mkali katika barabara hiyo; hawatakuwepo kabisa pale, lakini waliokombolewa watapita pale.
10 並且耶和華救贖的民必歸回, 歌唱來到錫安; 永樂必歸到他們的頭上; 他們必得着歡喜快樂, 憂愁歎息盡都逃避。
Fidia ya Yahwe itarudi na itakuja kwa wimbo wa Sayuni, na furaha ya milele itakuwa katika vichwa vyao; furaha na shangwe vitawazidi wao; huzuni na magonjwa yataondoshwa mbali.

< 以賽亞書 35 >