< 何西阿書 14 >
1 以色列啊,你要歸向耶和華-你的上帝; 你是因自己的罪孽跌倒了。
Israeli, rudi kwa Bwana, Mungu wako, kwa kuwa umeanguka kwa sababu ya uovu wako.
2 當歸向耶和華, 用言語禱告他說: 求你除淨罪孽,悅納善行; 這樣,我們就把嘴唇的祭代替牛犢獻上。
Chukueni maneno pamoja nanyi na mrudieni Yahweh. Mwambieni, “Ondoa uovu wetu wote, uyakubali mema, ili tuweze kukupa matunda ya midomo yetu.
3 我們不向亞述求救, 不騎埃及的馬, 也不再對我們手所造的說: 你是我們的上帝。 因為孤兒在你-耶和華那裏得蒙憐憫。
Ashuru haitatuokoa; hatutapanda farasi kwenda vitani. Hatuwezi tena kuiambia kazi ya mikono yetu, 'ninyi ni miungu yetu,' kwa maana kwako mtu asiye na baba hupata huruma.”
4 我必醫治他們背道的病, 甘心愛他們; 因為我的怒氣向他們轉消。
'Nitawaponya kugeuka kwao; Nami nitawapenda kwa moyo, kwa maana hasira yangu itaondoka kwake.
5 我必向以色列如甘露; 他必如百合花開放, 如黎巴嫩的樹木扎根。
Nitakuwa kama umande kwa Israeli; atachanua kama maua na kuchukua mizizi kama mwerezi nchini Lebanoni.
6 他的枝條必延長; 他的榮華如橄欖樹; 他的香氣如黎巴嫩的香柏樹。
Matawi yake yataenea; Uzuri wake utakuwa kama mizeituni, na harufu yake kama mierezi ya Lebanoni.
7 曾住在他蔭下的必歸回, 發旺如五穀,開花如葡萄樹。 他的香氣如黎巴嫩的酒。
Watu wanaoishi katika kivuli chake watarejea; watafufuliwa kama nafaka na maua kama mizabibu. Utukufu wake utakuwa kama divai ya Lebanoni.
8 以法蓮必說: 我與偶像還有甚麼關涉呢? 我-耶和華回答他,也必顧念他。 我如青翠的松樹; 你的果子從我而得。
Efraimu, nifanye nini tena na sanamu? Mimi nitamjibu na kumtunza. Mimi ni kama mberoshi majani yake ni ya kijani daima; kutoka kwangu huja matunda yako.”
9 誰是智慧人?可以明白這些事; 誰是通達人?可以知道這一切。 因為,耶和華的道是正直的; 義人必在其中行走, 罪人卻在其上跌倒。
Nani mwenye busara ili aelewe mambo haya? Nani anaelewa mambo haya ili awatambue? Kwa kuwa njia za Bwana ni sawa, na wenye haki watatembea ndani yao, lakini waasi wataanguka ndani yake.