< 希伯來書 6 >

1 所以,我們應當離開基督道理的開端,竭力進到完全的地步,不必再立根基,就如那懊悔死行、信靠上帝、
Kwa hiyo, tukiacha tulichojifunza kwanza kuhusu ujumbe wa Kristo, twapaswa kuwa na juhudi kuelekea kwenye ukomavu, tusiweke tena misingi ya toba kutoka katika kazi zisizo na uhai na imani katika Mungu,
2 各樣洗禮、按手之禮、死人復活,以及永遠審判各等教訓。 (aiōnios g166)
wala misingi ya mafundisho ya ubatizo, na kuwawekea mikono, ufufuo wa wafu, na hukumu ya milele. (aiōnios g166)
3 上帝若許我們,我們必如此行。
Na tutafanya hivi ikiwa Mungu ataruhusu.
4 論到那些已經蒙了光照、嘗過天恩的滋味、又於聖靈有分,
Kwa kuwa haiwezekani kwa wale ambao waliipata nuru awali, ambao walionja kipawa cha mbinguni, na kufanywa kuwa washirika wa Roho Mtakatifu,
5 並嘗過上帝善道的滋味、覺悟來世權能的人, (aiōn g165)
na ambao walionja uzuri wa neno la Mungu na kwa nguvu za wakati ujao, (aiōn g165)
6 若是離棄道理,就不能叫他們重新懊悔了。因為他們把上帝的兒子重釘十字架,明明地羞辱他。
na kisha wakaanguka - haiwezekani kuwarejesha tena katika toba. Hii ni kwa sababu wamemsulubisha Mwana wa Mungu mara ya pili kwa nafsi zao, wakimfanya kuwa chombo cha dhihaka hadharani.
7 就如一塊田地,吃過屢次下的雨水,生長菜蔬,合乎耕種的人用,就從上帝得福;
Kwa kuwa ardhi iliyopokea mvua inyeshayo mara kwa mara juu yake, na ikatoa mazao muhimu kwa hao waliofanya kazi katika ardhi, hupokea baraka kutoka kwa Mungu.
8 若長荊棘和蒺藜,必被廢棄,近於咒詛,結局就是焚燒。
Lakini ikiwa huzaa miiba na magugu, haina tena thamani na ipo katika hatari ya kulaaniwa. Mwisho wake ni kuteketezwa.
9 親愛的弟兄們,我們雖是這樣說,卻深信你們的行為強過這些,而且近乎得救。
Ijapokuwa tunazungumza hivi, rafiki wapenzi, tunashawishiwa na mambo mazuri yawahusuyo ninyi na mambo yahusuyo wokovu.
10 因為上帝並非不公義,竟忘記你們所做的工和你們為他名所顯的愛心,就是先前伺候聖徒,如今還是伺候。
Kwa kuwa Mungu si dhalimu hata asahau kazi yenu na kwa upendo mliouonesha kwa ajili ya jina lake, katika hili mliwatumikia waamini na bado mngali mnawatumikia.
11 我們願你們各人都顯出這樣的殷勤,使你們有滿足的指望,一直到底。
Na tunatamani sana kwamba kila mmoja wenu aweze kuonesha bidii ile ile mpaka mwisho kwa uhakika wa ujasiri.
12 並且不懈怠,總要效法那些憑信心和忍耐承受應許的人。
Hatutaki muwe wavivu, lakini muwe wafuasi wa wale warithio ahadi kwa sababu ya imani na uvumilivu.
13 當初上帝應許亞伯拉罕的時候,因為沒有比自己更大可以指着起誓的,就指着自己起誓,說:
Kwa maana Mungu alipompa Abrahamu ahadi, aliapa kwa nafsi yake, kwa kuwa asingeliapa kwa mwingine yeyote aliye mkubwa kuliko yeye.
14 「論福,我必賜大福給你;論子孫,我必叫你的子孫多起來。」
Alisema, “Hakika nitakubariki, na nitauongeza uzao wako zaidi.”
15 這樣,亞伯拉罕既恆久忍耐,就得了所應許的。
Kwa njia hii, Abrahamu alipokea kile alichoahidiwa baada ya kusubiria kwa uvumilivu.
16 人都是指着比自己大的起誓,並且以起誓為實據,了結各樣的爭論。
Maana wanadamu huapa kwa yeye aliye mkuu kuliko wao, na kwao ukomo wa mashindano yote ni kiapo kwa kuyathibitisha.
17 照樣,上帝願意為那承受應許的人格外顯明他的旨意是不更改的,就起誓為證。
Wakati Mungu alipoamua kuonesha kwa uwazi zaidi kwa warithi wa ahadi kusudi lake zuri lisilobadilika, alilithibitisha kwa kiapo.
18 藉這兩件不更改的事,上帝決不能說謊,好叫我們這逃往避難所、持定擺在我們前頭指望的人可以大得勉勵。
Alifanya hivyo ili kwa vitu viwili visivyoweza kubadilika, ambavyo katika hivyo Mungu hawezi kusema uongo, sisi tulioikimbilia hifadhi tupate kutiwa moyo kushikilia kwa nguvu tumaini lililowekwa mbele yetu.
19 我們有這指望,如同靈魂的錨,又堅固又牢靠,且通入幔內。
Tunao ujasiri huu kama nanga imara na ya kutegemea ya roho zetu, ujasiri ambao unaingia sehemu ya ndani nyuma ya pazia.
20 作先鋒的耶穌,既照着麥基洗德的等次成了永遠的大祭司,就為我們進入幔內。 (aiōn g165)
Yesu aliingia sehemu ile kama mtangulizi wetu, akisha kufanyika kuhani mkuu hata milele baada ya utaratibu wa Melkizedeki. (aiōn g165)

< 希伯來書 6 >