< 創世記 5 >
1 亞當的後代記在下面。(當上帝造人的日子,是照着自己的樣式造的,
Hii ni orodha iliyoandikwa ya vizazi vya Adamu. Wakati Mungu alipomuumba Adamu, alimfanya kwa sura ya Mungu.
2 並且造男造女。在他們被造的日子,上帝賜福給他們,稱他們為「人」。)
Aliwaumba mwanaume na mwanamke, akawabariki. Walipokwisha kuumbwa, akawaita “mwanadamu.”
3 亞當活到一百三十歲,生了一個兒子,形像樣式和自己相似,就給他起名叫塞特。
Adamu alipokuwa ameishi miaka 130, alikuwa na mwana aliyekuwa na sura yake, mwenye kufanana naye. Akamwita Sethi.
Baada ya Sethi kuzaliwa, Adamu aliishi miaka 800, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Adamu aliishi jumla ya miaka 930, ndipo akafa.
Sethi alipokuwa ameishi miaka 105, akamzaa Enoshi.
7 塞特生以挪士之後,又活了八百零七年,並且生兒養女。
Baada ya kumzaa Enoshi, Sethi aliishi miaka 807, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Sethi aliishi jumla ya miaka 912, ndipo akafa.
Enoshi alipokuwa ameishi miaka tisini, akamzaa Kenani.
10 以挪士生該南之後,又活了八百一十五年,並且生兒養女。
Baada ya kumzaa Kenani, Enoshi aliishi miaka 815, naye alikuwa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Enoshi aliishi jumla ya miaka 905, ndipo akafa.
Kenani alipokuwa ameishi miaka sabini, akamzaa Mahalaleli.
13 該南生瑪勒列之後,又活了八百四十年,並且生兒養女。
Baada ya kumzaa Mahalaleli, Kenani aliishi miaka 840, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Kenani aliishi jumla ya miaka 910, ndipo akafa.
Mahalaleli alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Yaredi.
16 瑪勒列生雅列之後,又活了八百三十年,並且生兒養女。
Baada ya kumzaa Yaredi, Mahalaleli aliishi miaka 830, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Mahalaleli aliishi jumla ya miaka 895, ndipo akafa.
Yaredi alipokuwa ameishi miaka 162, akamzaa Enoki.
19 雅列生以諾之後,又活了八百年,並且生兒養女。
Baada ya kumzaa Enoki, Yaredi aliishi miaka 800, naye akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Yaredi aliishi jumla ya miaka 962, ndipo akafa.
Enoki alipokuwa ameishi miaka sitini na mitano, akamzaa Methusela.
22 以諾生瑪土撒拉之後,與上帝同行三百年,並且生兒養女。
Baada ya kumzaa Methusela, Enoki alitembea na Mungu miaka 300, na akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Enoki aliishi jumla ya miaka 365.
24 以諾與上帝同行,上帝將他取去,他就不在世了。
Enoki akatembea na Mungu, kisha akatoweka, kwa sababu Mungu alimchukua.
Methusela alipokuwa ameishi miaka 187, akamzaa Lameki.
26 瑪土撒拉生拉麥之後,又活了七百八十二年,並且生兒養女。
Baada ya kumzaa Lameki, Methusela aliishi miaka 782, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Methusela aliishi jumla ya miaka 969, ndipo akafa.
Lameki alipokuwa ameishi miaka 182, alimzaa mwana.
29 給他起名叫挪亞,說:「這個兒子必為我們的操作和手中的勞苦安慰我們;這操作勞苦是因為耶和華咒詛地。」
Akamwita jina lake Noa, akasema, “Yeye ndiye atakayetufariji katika kazi na maumivu makali ya mikono yetu yaliyosababishwa na ardhi iliyolaaniwa na Bwana.”
30 拉麥生挪亞之後,又活了五百九十五年,並且生兒養女。
Baada ya Noa kuzaliwa, Lameki aliishi miaka 595, akawa na watoto wengine wa kiume na wa kike.
Lameki aliishi jumla ya miaka 777, ndipo akafa.
Baada ya Noa kuishi miaka 500, aliwazaa Shemu, Hamu na Yafethi.