< 創世記 22 >

1 這些事以後,上帝要試驗亞伯拉罕,就呼叫他說:「亞伯拉罕!」他說:「我在這裏。」
Ikawa kwamba baada ya mambo hayo Mungu akampima Abraham. Akamwambia, “Abraham!” Abraham akasema, “Mimi hapa.”
2 上帝說:「你帶着你的兒子,就是你獨生的兒子,你所愛的以撒,往摩利亞地去,在我所要指示你的山上,把他獻為燔祭。」
Kisha Mungu akasema, “Mchukue mwanao, mwanao wa pekee, umpendaye, Isaka, na uende katika nchi ya Moria. Mtoe kama sadaka ya kuteketezwa mahali pale juu ya moja ya milima hiyo, ambayo nitakwambia.”
3 亞伯拉罕清早起來,備上驢,帶着兩個僕人和他兒子以撒,也劈好了燔祭的柴,就起身往上帝所指示他的地方去了。
Kwa hiyo Abraham akaamka asubuhi na mapema, akatandika punda wake, akawachukuwa vijana wake wawili, pamoja na Isaka mwanawe. Akakata kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, kisha akapanga safari kwenda mahali ambapo Mungu alimwambia.
4 到了第三日,亞伯拉罕舉目遠遠地看見那地方。
Siku ya tatu Abraham akatazama juu na akaona mahali pakiwa mbali.
5 亞伯拉罕對他的僕人說:「你們和驢在此等候,我與童子往那裏去拜一拜,就回到你們這裏來。」
Abraham akawambia vijana wake, “kaeni hapa pamoja na punda, mimi pamoja na Isaka tutakwenda pale. Tutaabudu na kisha tutarudi hapa penu.”
6 亞伯拉罕把燔祭的柴放在他兒子以撒身上,自己手裏拿着火與刀;於是二人同行。
Ndipo Abraham akachukua kuni kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa akaziweka juu ya Isaka mwanawe. Mkononi mwake akachukua moto na kisu; na wote wawili wakaondoka pamoja.
7 以撒對他父親亞伯拉罕說:「父親哪!」亞伯拉罕說:「我兒,我在這裏。」以撒說:「請看,火與柴都有了,但燔祭的羊羔在哪裏呢?」
Isaka akazungumza na Abraham baba yake akisema, “Baba yangu,” naye akasema, “Ndiyo mwanangu.” Akasema, “Tazama huu ni moto na kuni, lakini yuko wapi mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa?”
8 亞伯拉罕說:「我兒,上帝必自己預備作燔祭的羊羔。」於是二人同行。
Abraham akasema, “Mungu mwenyewe atatupatia mwanakondoo kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa, mwanangu.” Kwa hiyo wakaendelea, wote wawili pamoja.
9 他們到了上帝所指示的地方,亞伯拉罕在那裏築壇,把柴擺好,捆綁他的兒子以撒,放在壇的柴上。
Walipofika mahali ambapo Mungu alikuwa amemwambia, Abraham akajenga madhabahu pale na akaweka kuni juu yake. Kisha akamfunga Isaka mwanawe, na akamlaza juu ya madhabahu, juu ya zile kuni.
10 亞伯拉罕就伸手拿刀,要殺他的兒子。
Abraham akanyoosha mkono wake akachukua kisu ili kumuua mwanawe.
11 耶和華的使者從天上呼叫他說:「亞伯拉罕!亞伯拉罕!」他說:「我在這裏。」
Ndipo malaika wa Yahwe akamwita kutoka mbinguni na kusema, “Abraham, Abraham!” naye akasema, “Mimi hapa.”
12 天使說:「你不可在這童子身上下手。一點不可害他!現在我知道你是敬畏上帝的了;因為你沒有將你的兒子,就是你獨生的兒子,留下不給我。」
Akasema, “usinyooshe mkono wako juu ya kijana, wala usifanye jambo lolote kumdhuru, kwa kuwa sasa najua unamcha Mungu, kwa kuona kuwa hukumzuilia mwanao, mwanao wa pekee, kwa ajili yangu.”
13 亞伯拉罕舉目觀看,不料,有一隻公羊,兩角扣在稠密的小樹中。亞伯拉罕就取了那隻公羊來,獻為燔祭,代替他的兒子。
Abraham akatazama juu na tazama, nyuma yake kulikuwa na kondoo mume amenaswa pembe zake kichakani. Abraham akaenda akamchukua kondoo na akamtoa kama sadaka ya kuteketezwa badala ya mwanawe.
14 亞伯拉罕給那地方起名叫「耶和華以勒」,直到今日人還說:「在耶和華的山上必有預備。」
Kwa hiyo Abraham akapaita mahali pale, Yahwe atatoa,” na panaitwa hivyo hata leo. “Juu ya mlima wa Yahwe itatolewa.”
15 耶和華的使者第二次從天上呼叫亞伯拉罕說:
Malaika wa Yahwe akamwita Abraham kwa mara ya pili kutoka mbinguni
16 「耶和華說:『你既行了這事,不留下你的兒子,就是你獨生的兒子,我便指着自己起誓說:
na kusema - Hiki ni kiapo cha Yahwe, “Kwa ajili ya nafsi yangu nimeapa kwamba kwa kuwa umefanya jambo hili, na hukunizuilia mwanao, mwanao wa pekee,
17 論福,我必賜大福給你;論子孫,我必叫你的子孫多起來,如同天上的星,海邊的沙。你子孫必得着仇敵的城門,
hakika nitakubariki na nitakuzidishia uzao wako kama nyota za angani, na kama mchanga ulioko kwenye ufukwe wa bahari; na uzao wakowatamiliki lango la adui zao.
18 並且地上萬國都必因你的後裔得福,因為你聽從了我的話。』」
Kupitia uzao wako mataifa yote ya dunia watabarikiwa, kwa sababu umetii sauti yangu.”
19 於是亞伯拉罕回到他僕人那裏,他們一同起身往別是巴去,亞伯拉罕就住在別是巴。
Kwa hiyo Abraham akarejea kwa vijana wake, na wakaondoka wakaenda pamoja Beerisheba, hivyo akakaa Beerisheba.
20 這事以後,有人告訴亞伯拉罕說:「密迦給你兄弟拿鶴生了幾個兒子,
Ikawa kwamba baada ya mambo haya ambayo Abraham aliambiwa, “Milka amemzalia pia watoto, ndugu yako Nahori.”
21 長子是烏斯,他的兄弟是布斯和亞蘭的父親基母利,
Hawa walikuwa ni Usi mzaliwa wa kwanza, Busi ndugu yake, Kemueli aliye mzaa Aramu,
22 並基薛、哈瑣、必達、益拉、彼土利(彼土利生利百加)。」
Kesedi, Hazo, Pildashi, Yidlafu, na Bethueli.
23 這八個人都是密迦給亞伯拉罕的兄弟拿鶴生的。
Bethuel akamzaa Rebeka. Hawa walikuwa ni wale watoto wanane ambao Milka alizaa kwa Nahori, ndugu yake na Abraham.
24 拿鶴的妾名叫流瑪,生了提八、迦含、他轄,和瑪迦。
Suria wake, ambaye aliitwa Reuma, pia akamzaa Teba, Gahamu, Tahashi, na Maaka.

< 創世記 22 >