< 以西結書 48 >
1 眾支派按名所得之地記在下面:從北頭,由希特倫往哈馬口,到大馬士革地界上的哈薩‧以難。北邊靠着哈馬地(各支派的地都有東西的邊界),是但的一分。
Haya ndiyo majina ya makabila. Kabila la Dani litapokea sehemu moja ya nchi; mipaka yake itakuwa karibu na upande wa mashariki mpaka wa Israeli karibu na njia ya Hethloni na Lebo Hamathi. Mpaka wake utaenda hata karibu na Hazari Enani na karibu na mpaka wa Damaskasi hata upande wa kaskazini na kisha karibu na Hamathi. Mpaka wa Dani utaenda kutoka mashariki moja kwa moja hata Bahari Kubwa.
Kupakana na mpaka wa Dani, kutoka upande wa mashariki hata upande wa magharibi, Asheri itakuwa na fungu moja.
Kupakana na mpaka wa Asheri kutoka upande wa mashariki hata magharibi, Naftali atakuwa na fungu moja.
4 挨着拿弗他利的地界,從東到西,是瑪拿西的一分。
Kupakana na mpaka wa Naftali kutoka upande wa mashariki hata magharibi, Manase atakuwa na fungu moja.
Kupakana na mpaka wa Manase kutoka upande wa mashariki hata magharibi, Efraimu atakuwa na fungu moja.
Kupakana na mapaka wa Efraimu kutoka mashariki hata magharibi, Rubeni atakuwa na fungu moja.
Kupakana na mpaka wa Rubeni kutoka mashariki hata magharibi, Yuda atakuwa na fungu moja.
8 挨着猶大的地界,從東到西,必有你們所當獻的供地,寬二萬五千肘。從東界到西界,長短與各分之地相同,聖地當在其中。
Sadaka ya nchi ambayo mtaifanya itakuwa karibu na mpaka wa Yuda na hapohapo kutoka upande wa mashariki hata upande wa magharibi; itakuwa ridhaa elfu ishirini na tano upana. Urefu unakaribiana na fungu la kabila moja kutoka upande wa mashariki hata upande wa magharibi, na hekalu litakuwa katikati yake.
9 你們獻與耶和華的供地要長二萬五千肘,寬一萬肘。
Huu mji mtakao utoa sadaka kwa ajili ya Yahwe utakuwa na ridhaa elfu ishirini na tano urefu wake na ridhaa elfu kumi upana.
10 這聖供地要歸與祭司,北長二萬五千肘,西寬一萬肘,東寬一萬肘,南長二萬五千肘。耶和華的聖地當在其中。
Haya yatakuwa matoleo ya hili fungu takatifu la nchi: makuhani watakuwa na nchi watakayopewa kipimo chake ridhaa elfu ishirini na tano urefu kwa upande kaskazini; ridhaa elfu kumi upana upande wa magharibi; urefu wa ridhaa elfu kumi upande wa magharibi; na urefu rithaa elfu ishirini na tano upande wa kusini, pamoja na mahali patakatifu pa Yahwe katikati yake.
11 這地要歸與撒督的子孫中成為聖的祭司,就是那守我所吩咐的。當以色列人走迷的時候,他們不像那些利未人走迷了。
Hii itakuwa wakfu na makuhani wa safu ya Zadoki, aliyenitumikia kwa uaminifu na ambaye hakwenda nje ya mstari wakati watu wa Israeli walipoeenda nje ya mstari, kama Walawi walivyofanya.
12 這要歸與他們為供地,是全地中至聖的。供地挨着利未人的地界。
Sadaka yao itakuwa fungu la hiyo nchi takatifu sana, karibu na mpaka wa Walawi.
13 利未人所得的地要長二萬五千肘,寬一萬肘,與祭司的地界相等,都長二萬五千肘,寬一萬肘。
Nchi ya Walawi karibu na mpaka wa nchi ya makuhani itakuwa ridhaa elfu ishirini na tano urefu na ridhaa elfu kumi upana. Urefu wote wa eneo la nchi utakuwa ridhaa elfu ishirini na tano urefu na ridhaa elfu ishirini upana.
14 這地不可賣,不可換,初熟之物也不可歸與別人,因為是歸耶和華為聖的。
Hawataiuza au kuibadilisha; hakuna malimbuko ya hiyo nchi ya Israeli itakayogawanywa kutoka haya maeneo, kwa kuwa yote ni matakatifu kwa ajili ya Yahwe.
15 這二萬五千肘前面所剩下五千肘寬之地要作俗用,作為造城蓋房郊野之地。城要在當中。
Nchi iliyobaki, ridhaa elfu kumi na tano upana na ridhaa elfu ishirini na tano urefu, itakuwa kwa wote wanayoitumia hiyo nchi, nyumba, na sehemu ya malisho; huo mji utakuwa katikati yake.
16 城的尺寸乃是如此:北面四千五百肘,南面四千五百肘,東面四千五百肘,西面四千五百肘。
Hivi ndivyo vitakuwa vipimo vya mji: upande wa kaskazini utakuwa ridhaa 4, 500 urefu; upande wa kusini utakuwa ridhaa 4, 500 urefu; upande wa magharibi utakuwa ridhaa 4, 500 urefu; na magharibi itakuwa ridhaa 4, 500 urefu.
17 城必有郊野,向北二百五十肘,向南二百五十肘,向東二百五十肘,向西二百五十肘。
Kutakuwa na malisho ya mji kuelekea kaskazini, ridhaa 250 kwenda chini; hata kusini, ridhaa 250 kwenda chini; kuelekea mashariki, ridhaa 250 kwenda chini, na kuelekea magharibi ridhaa 250 kwenda chini.
18 靠着聖供地的餘地,東長一萬肘,西長一萬肘,要與聖供地相等;其中的土產要作城內工人的食物。
Eneo lililobaki la matoleo matakatifu litanyooshwa ridhaa elfu kumi hata mashariki na ridhaa elfu kumi kuelekea magharibi. Litanyooshwa karibu na mpaka wa matoleo matakatifu, na mazao yake yatakuwa chakula kwa ajili ya wale wanaofanya kazi katika nchi.
19 所有以色列支派中,在城內做工的,都要耕種這地。
Wale wafanyao kazi katika mji, watu wote wa kabila za Israeli, watailima hiyo nchi.
20 你們所獻的聖供地連歸城之地,是四方的:長二萬五千肘,寬二萬五千肘。
Matoleo yote ya nchi yatapimwa ridhaa elfu ishirini na moja kwa ridhaa elfu ishirini na tano. Kwa njia hii mtatengeneza matoleo matakatifu ya nchi, pamoja na nchi kwa ajili mji.
21 聖供地連歸城之地,兩邊的餘地要歸與王。供地東邊,南北二萬五千肘,東至東界,西邊南北二萬五千肘,西至西界,與各分之地相同,都要歸王。聖供地和殿的聖地要在其中,
Mabaki ya nchi mojawapo upande wa matoleo matakatifu na eneo la mji litakuwa kwa ajili ya mwana wa mfalme. Eneo la nchi ya mwana wa mfalme kuelekea mashariki litanyooshwa kwa ridhaa elfu ishirini na tano kutoka kwenye mpaka wa matoleo matakatifu hata mpaka wa mashariki-na eneo lake kuelekea mpaka wa magharibi. Katikati kutakuwa matolea matakatifu, na mahali patakatifu pa hekalu patakuwa katikati yake.
22 並且利未人之地,與歸城之地的東西兩邊延長之地(這兩地在王地中間),就是在猶大和便雅憫兩界中間,要歸與王。
Nchi imenyooka kutoka mali ya Walawi na eneo la mji katikati yake litakuwa kwa ajili ya mwana wa mfalme; itakuwa kati ya mpaka wa Yuda na mpaka wa Benjamini-hiyo nchi itakuwa kwa ajili ya mwana wa mfame.
Kwa kabila zitakazobaki, mafungu yao yataunganishwa kutoka upande wa mashariki. Benjamini atapokea fungu moja.
Kupakana na mpaka wa Benjamini kutoka upande wa mashariki hata magharibi, Simioni atakuwa na fungu moja.
Kupakana na mpaka wa Isakari kutakuwa na fungu moja.
26 挨着以薩迦的地界,從東到西,是西布倫的一分。
Kupakana na mpaka wa Isakari kutoka mashariki hata magharibi, Zebuloni atakuwa na fungu moja.
Hata kusini mwa mpaka wa Zebuloni, kutoka upande wa mashariki hata upande wa magahribi, kutakuwa na nchi ya Gadi-fungu moja.
28 迦得地的南界是從他瑪到米利巴‧加低斯的水,延到埃及小河,直到大海。
Mpaka wa kusini mwa Gadi kutanyooshwa kutoka Tamari hata kwenye maji ya Meriba Kadeshi, mbele hadi kijito cha Misri, na kisha hata Bahari kuu.
29 這就是你們要拈鬮分給以色列支派為業之地,乃是他們各支派所得之分。這是主耶和華說的。
Hii ndiyo nchi ambayo mtakazo gawana; kutakuwa na urithi wa makabila ya Israeli. Haya yatakuwa mafungu yao. Hivi ndivy Bwana Yahwe asemavyo.
Hawa ndio watakaoishi kutoka kwenye nchi: upande wa kaskazini, ambapo patapimwa ridhaa 4, 500 kwa urefu,
31 城的各門要按以色列支派的名字。北面有三門,一為呂便門,一為猶大門,一為利未門;
kutakuwa na malango matatu, yaitwayo kwa ajili ya Israeli: lango moja kwa ajili ya Rubeni, lango moja kwa ajili ya Yuda, na lango moja kwa ajili ya Walawi.
32 東面四千五百肘,有三門,一為約瑟門,一為便雅憫門,一為但門;
Kwa upande wa mashariki, ambapo patapimwa ridhaa 4, 500 kwa urefu, kutakuwa na malango matatu: lango moja kwa ajili ya Yusufu, lango moja kwa ajili ya Benjamini, na lango moja kwa ajili ya Dani.
33 南面四千五百肘,有三門,一為西緬門,一為以薩迦門,一為西布倫門;
Kwa upande wa mashariki, kutakuwa na kipimo cha ridhaa 4, 500 urefu, kutakuwa na malango matatu: lango moja kwa ajili ya Simioni, lango moja kwa ajili ya Isakari, na moja kwa ajili ya Zebuloni.
34 西面四千五百肘,有三門,一為迦得門,一為亞設門,一為拿弗他利門。
Kwa upande wa magharibi, ambao kipimo chake kitakuwa ridhaa 4, 500, kutakuwa ba malango matatu: lango moja kwa ajili ya Gadi, lango moja kwa ajili ya Asheri, na lango moja kwa ajili ya Naftali.
35 城四圍共一萬八千肘。從此以後,這城的名字必稱為「耶和華的所在」。
Umbali kuuzunguka mji utakuwa ridhaa elfu kumi na nane; kutoka hiyo siku, jina la huo mji litakuwa “Yahwe yupo hapo.”