< 以西結書 21 >
Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
2 「人子啊,你要面向耶路撒冷和聖所滴下預言,攻擊以色列地。
“Mwanadamu, weka uso wako kuelekea Yerusalemu, na neno juu ya patakatifu; tabiri juu ya nchi ya Israeli.
3 對以色列地說,耶和華如此說:我與你為敵,並要拔刀出鞘,從你中間將義人和惡人一併剪除。
Sema juu ya nchi ya Israeli, 'Yahwe asema hivi: Tazama! Ni juu yako! Nitautoa upanga wangu kutoka kwenye ala yake na kuwakatilia mbali wote yaani mtu mwenye haki na mtu mwovu kutoka kwako!
4 我既要從你中間剪除義人和惡人,所以我的刀要出鞘,自南至北攻擊一切有血氣的;
Ili niwakatilie mbali wote, mwenye haki na mwovu kutoka kwako, upanga wangu utatoka kwenye ala yake juu ya wote wenye mwili kutoka kusini hata kaskazini.
5 一切有血氣的就知道我-耶和華已經拔刀出鞘,必不再入鞘。
Kisha wote wenye mwili watajua yakwamba mimi, Yahwe, nimeutoa upanga wangu kutoka kwenye ala yake. Hautarudi tena!'
6 人子啊,你要歎息,在他們眼前彎着腰,苦苦地歎息。
Kwa hiyo, mwanadamu, gumia kama kuvunjika kwa viuno vyako! Katika uchungu gumia mbele ya macho yao!
7 他們問你說:『為何歎息呢?』你就說:『因為有風聲、災禍要來。人心都必消化,手都發軟,精神衰敗,膝弱如水。看哪,這災禍臨近,必然成就。這是主耶和華說的。』」
Kisha itatokea kwamba watakuuliza, 'Kwa sababu gani unalia?' Kisha utasema, 'Kwa sababu ya habari inayokuja, kwa kuwa kila moyo utakuwa dhaifu, na kila mkono utasita! Kila roho itazimia, na kila goti litatiririrka kama maji. Tazama! Inakuja na itakuwa kama hivi! -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.”'
Kisha neno la Yahwe likanijia, kusema,
9 「人子啊,你要預言。耶和華吩咐我如此說: 有刀、有刀, 是磨快擦亮的;
“Mwanadamu, tabiri na sema, 'Bwana asema hivi: sema: Upanga! Upanga! Utachongwa na kusuguliwa!
10 磨快為要行殺戮, 擦亮為要像閃電。 我們豈可快樂嗎?罰我子的杖藐視各樹。
Utanolewa ili kushiriki katika machinjio makubwa! Utasuguliwa ili uwe kama mng'ao wa radi! Je! Tufanye furaha katika fimbo ya mwana wa mfalme? Upanga ujao huchukia kila hiyo fimbo!
11 這刀已經交給人擦亮,為要應手使用。這刀已經磨快擦亮,好交在行殺戮的人手中。
Hivyo upanga utatolewa kwa ajili ya kusuguliwa, na kisha kushikika kwa mkono! Upanga umechongwa na umesuguliwa na utatolewa kwenye mkono wa yule auaye!'
12 人子啊,你要呼喊哀號,因為這刀臨到我的百姓和以色列一切的首領。他們和我的百姓都交在刀下,所以你要拍腿歎息。
Ita msaada na omboleza, mwanadamu! Kwa kuwa upanga umekuja juu ya watu wangu! Uko juu ya wakuu wote wa Israeli. Wametolewa dhidi ya upanga pamoja na watu wangu. Kwa hiyo, piga paja lako!
13 有試驗的事;若那藐視的杖歸於無有,怎麼樣呢?這是主耶和華說的。
Kwa kuwa kuna kujaribiwa, lakini itakuwaje kama fimbo ya kifalme haitakuwepo tena? -hivi ndivyo Bwana Yahwe asemavyo.
14 「人子啊,你要拍掌預言。我-耶和華要使這刀,就是致死傷的刀,一連三次加倍刺人,進入他們的內屋,使大人受死傷的就是這刀。
Basi wewe, mwanadamu, tabiri, na piga makofi, kwa kuwa upanga utakushambulia hata mara tatu! Upanga kwa wale watakaochinjwa! Utakuwa upanga kwa ajili ya kuchinjia, ukiwatoboa pande zote!
15 我設立這恐嚇人的刀,攻擊他們的一切城門,使他們的心消化,加增他們跌倒的事。哎!這刀造得像閃電,磨得尖利,要行殺戮。
Ili kuyeyusha mioyo yao na kuongeza kuanguka kwao, nimeweka machinjio ya upanga juu ya malango! Ole! Umeundwa kama mng'ao wa radi, umetengwa kwa ajili ya kuua!
16 刀啊,你歸在右邊,擺在左邊;你面向哪方,就向那方殺戮。
Wewe, upanga! Nyooka upande wa kuume! Nyooka upande wa kushoto! Nenda popote ulipoelekeza uso wako.
17 我也要拍掌,並要使我的忿怒止息。這是我-耶和華說的。」
Kwa kuwa pia nitapiga mikono yangu miwili kwa pamoja (makofi), na kisha nitaleta ghadhabu yangu kwa waliobakia! Mimi, Yahwe, nimesema hivi!”
Neno la Yahwe likanijia tena, kusema,
19 「人子啊,你要定出兩條路,好使巴比倫王的刀來。這兩條路必從一地分出來,又要在通城的路口上畫出一隻手來。
“Sasa wewe, mwanadamu, teua njia mbili kwa ajili ya upanga wa mfalme wa Babeli upate kuja. Njia hizo mbili zitaanza katika nchi moja, na kibao cha barabarani kitamwonyesha mmoja wao kama kuuelekea mji.
20 你要定出一條路,使刀來到亞捫人的拉巴;又要定出一條路,使刀來到猶大的堅固城耶路撒冷。
Onyesha njia moja kwa ajili ya jeshi la Wababeli kuja Raba, mji wa Waamoni. Onyesha nyingine kuelekea jeshi la Yuda na mji wa Yerusalemu, ambayo imeimarishwa.
21 因為巴比倫王站在岔路那裏,在兩條路口上要占卜。他搖籤求問神像,察看犧牲的肝;
Kwa kuwa mfalme wa Babeli atasimama kwenye makutano ya barabara, kwenye njia panda, ili kufanya uganga. Alitingisha mishale na kuuliza mwelekeo kutoka kwa sanamu na atalichunguza ini.
22 在右手中拿着為耶路撒冷占卜的籤,使他安設撞城錘,張口叫殺,揚聲吶喊,築壘造臺,以撞城錘,攻打城門。
Katika mkono wake wa kuume kutakuwa na dalili kuhusu Yerusalemu, kuweka mitambo ya kubomolea juu ya hiyo, kufungua kinywa chake kupanga kuchinja, kutoa sauti ya vita, kuweka mitambo ya kubomolea juu ya malango, kujenga ngazi, na kusimamisha wima minara ya boma.
23 據那些曾起誓的猶大人看來,這是虛假的占卜;但巴比倫王要使他們想起罪孽,以致將他們捉住。」
Itaonekana kuwa ishara isiyofaa katika macho ya wale walio katika Yerusalemu, wale walioapa kiapo kwa Wababeli! Lakini mfalme atawashtaki kwa kuvunja sheria ya mkataba ili kuwabariki!
24 主耶和華如此說:「因你們的過犯顯露,使你們的罪孽被記念,以致你們的罪惡在行為上都彰顯出來;又因你們被記念,就被捉住。
Kwa hiyo Bwana Yahwe asema hivi: Kwa sababu umeuleta uovu wako kwenye kumbukumbu zangu, makosa yenu yatafunuliwa! Dhambi zenu zitaonekana katika matendo yenu yote! Kwa sababu hii utamkumbusha kila mtu mtakamatwa kwa mkono wa adui yenu!
25 你這受死傷行惡的以色列王啊,罪孽的盡頭到了,受報的日子已到。
Kama wewe, mchafu na mtawala mwovu wa Israeli, ambaye siku ya hukumu imekuja, na ambaye mda wa kufanya uovu umekoma,
26 主耶和華如此說:當除掉冠,摘下冕,景況必不再像先前;要使卑者升為高,使高者降為卑。
Bwana Yahwe asema hivi kwako: Toa kilemba na vua taji! Mambo hayatakuwa tena kama yalivyokuwa! Kiinue kilicho chini na kiinue kilichoinuka!
27 我要將這國傾覆,傾覆,而又傾覆;這國也必不再有,直等到那應得的人來到,我就賜給他。」
Uharibifu! Uharibifu! Nitaiharibu! Haitakuwa tena hadi atakapokuja yeye ambaye ameteuliwa kutekeleza hukumu.
28 「人子啊,要發預言說:主耶和華論到亞捫人和他們的凌辱,吩咐我如此說:有刀,有拔出來的刀,已經擦亮,為行殺戮,使他像閃電以行吞滅。
Basi wewe, mwanadamu, tabiri na sema, 'Bwana Yahwe asema hivi hawa ni watu wa Amoni kuhusiana na ujio wa aibu yao: Upanga, upanga umechirwa! Umenolewa kwa ajili ya kuchinja, hivyo utakuwa kama kimuli muli cha radi!
29 人為你見虛假的異象,行謊詐的占卜,使你倒在受死傷之惡人的頸項上。他們罪孽到了盡頭,受報的日子已到。
Wakati manabii wameona maono ya uongo juu yako, wakati watakapofanya matambiko kuuijia kwa uongo juu yako, huu upanga utaanguka chini juu ya shingo za mwovu ambao wako karibu kuuawa, ambao siku ya ghadhabu imekuja na ambao mda wa uovu unakaribia kuisha.
30 你將刀收入鞘吧!在你受造之處、生長之地,我必刑罰你。
Rudisha upanga kwenye gala yake. Katika mahali ulipoumbwa, katika nchi ya chimbuko lako, nitakuhukumu!
31 我必將我的惱恨倒在你身上,將我烈怒的火噴在你身上;又將你交在善於殺滅的畜類人手中。
Nitamwaga hasira yangu juu yako! Nitapuliza upepo wa moto wa ghadhabu juu yako na kukuweka kwenye mkono wa watu wakatili, watu wajuao kuangamiza!
32 你必當柴被火焚燒;你的血必流在國中。你必不再被記念,因為這是我-耶和華說的。」
Utakuwa kuni kwa ajili ya moto! Damu yako itakuwa kati ya nchi. Hutakumbukwa tena, kwa kuwa mimi, Yahwe nimesema hivi!”'