< 出埃及記 40 >
Kisha Yahweh akasema na Musa na kumwambia,
“Siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza ya mwaka lazima wewe uandae hema la kukutania.
Utaweka sanduku la ushuhuda ndani yake, na utaziba sanduku kwa pazia.
4 把桌子搬進去,擺設上面的物。把燈臺搬進去,點其上的燈。
Utaleta ndani meza na kuandaa kwa mpangilio vitu vyake. Kisha utaleta kinara cha taa na kuandaa taa.
Nawe utaweka madhabahu ya dhahabu ya uvumba mbele ya sanduku la ushuhuda, na utaweka pazia katika mwingilio wa hema la kukutania.
Utaweka madhabahu kwa ajili ya sadaka ya kuteketezwa mbele ya mwingilio wa hema ya kukutania.
Utaweka ile saani kubwa katikati ya hema la kukutania na madhabahu na utaweka maji ndani yake.
Uandae nyuani inayoizunguka, na utundike pazia katika mwingilio wa nyuani.
9 用膏油把帳幕和其中所有的都抹上,使帳幕和一切器具成聖,就都成聖。
Lazima uchukuwe mafuta ya upako na upake hema la kukutania na kila kitu kilichopo ndani yake. Lazima uitenge na samani zake kwangu; kisha itakuwa takatifu.
10 又要抹燔祭壇和一切器具,使壇成聖,就都成為至聖。
Lazima upake mafuta madhabahu ya sadaka ya kuteketezwa na vyombo vyake. Lazima utenge madhabhu kwa ajili yangu na itakuwa takatifu kwangu.
Upake mafuta beseni la shaba na sakafu yake na uitenge kwa ajili yangu.
Umlete Aruni na wanae kwa mwingilio wa hema la kukutania na uwaoshe wote kwa maji.
13 要給亞倫穿上聖衣,又膏他,使他成聖,可以給我供祭司的職分;
Utamfunika Aruni kwa mavazi yaliyo tengwa kwa ajili yangu, mpake mafuta na umtenge ili anitumikie kama kuhani.
Utawaleta wana wake na kuwafunika kwa nguo nzito.
15 怎樣膏他們的父親,也要照樣膏他們,使他們給我供祭司的職分。他們世世代代凡受膏的,就永遠當祭司的職任。」
Utawapaka mafuta kama ulivyo mpaka baba yao ili wanitumikie kama makuhani. Upako wao utawafanya makuhani wa kudumu vizazi vyote vya watu wao.”
Hivi ndivyo Musa alivyo sema; alifuata yote Yahweh aliyo muamuru. Alifanya vitu vyote hivi.
Hivyo hema la kukutania liliandaliwa siku ya kwanza ya mwezi wa mwaka wa pili.
18 摩西立起帳幕,安上帶卯的座,立上板,穿上閂,立起柱子。
Musa alianda hema la kukutania, akaeka sakafu zake sehemu yake, akaanda fremu zake, akashikisha chuma zake, na akaanda minara na nguzo zake.
19 在帳幕以上搭罩棚,把罩棚的頂蓋蓋在其上,是照耶和華所吩咐他的。
Alitandaza mfuniko juu ya hema la kukutania na kuweka hema juu yake, kama Yahweh alivyo muamuru.
20 又把法版放在櫃裏,把槓穿在櫃的兩旁,把施恩座安在櫃上。
Alichukuwa amri za agano na kuweka kwenye sanduku. Pia aliweka nguzo kwenye sanduku na kuweka mfuniko wa kiti cha rehema.
21 把櫃抬進帳幕,掛上遮掩櫃的幔子,把法櫃遮掩了,是照耶和華所吩咐他的。
Aliichukuwa sanduku na kuweka ndani ya hema la kukutania. Aliandaa pazia ili lizibe sanduku la ushuhuda, kama Yahweh alivyo muamuru.
Alieka meza kwenye hema la kukutania, kwa upande wa kaskazini mwa hema la kukutania, nje ya pazia.
23 在桌子上將餅陳設在耶和華面前,是照耶和華所吩咐他的。
Alieka mkate kwa mpangilio katika meza ya Yahweh, kama Yahweh alivyo amuru.
24 又把燈臺安在會幕內,在帳幕南邊,與桌子相對,
Alieka kinara cha taa kwenye hema la kukutania, upande wa pili wa meza, kusini mwa hema la kukutani.
Aliwasha taa mbele za Yahweh, kama Yahweh alivyo muamuru.
Aliweka madhabahu ya dhahabu ya uvumba ndani ya hema la kukutania mbele ya pazia.
27 在壇上燒了馨香料做的香,是照耶和華所吩咐他的。
Alichoma uvumba wa manukato hapo, kama Yahweh alivyo muamuru.
Alitundika pazia katika hema ya kukutania.
29 在會幕的帳幕門前,安設燔祭壇,把燔祭和素祭獻在其上,是照耶和華所吩咐他的。
Aliweka madhabahu ya sadaka ya kuteketeza katika hema ya kukutania. Aliitolea sadaka ya kuteketeza na sadaka ya unga, kama Yahweh alivyo muamuru.
30 把洗濯盆安在會幕和壇的中間,盆中盛水,以便洗濯。
Aliweka beseni katikati ya hema ya kukutunia na madhabahu, na maji ya kuoshea.
Musa, Aruni, na wanae waliosha mikono yao na miguu kwenye beseni
32 他們進會幕或就近壇的時候,便都洗濯,是照耶和華所吩咐他的。
muda wowote walipoenda kwenye hema ya kukutania na muda wowote walipoenda kwenye madhabahu. Walijisafisha, kama Yahweh alivyo muamuru Musa.
33 在帳幕和壇的四圍立了院帷,把院子的門簾掛上。這樣,摩西就完了工。
Musa alianda nyuani nyuma ya hema ya kukutania na madhabahu. Alianda pazia katika mwingilio wa nyuani. Katika hili, Musa alimaliza kazi.
34 當時,雲彩遮蓋會幕,耶和華的榮光就充滿了帳幕。
Kisha wingu likafunika hema ya kukutania, na utukufu wa Yahweh ukafunika hema ya kukutania.
35 摩西不能進會幕;因為雲彩停在其上,並且耶和華的榮光充滿了帳幕。
Musa hakuweza kuingia hema ya kukutania kwasababu wingu lilikuwa juu yake, na kwasababu utukufu wa Yahweh ulijaza hema ya kukutania.
Muda wowote wingu lilipo chukuliwa juu kutoka hema ya kukutania, watu wa Israeli waliendelea na safari yao.
37 雲彩若不收上去,他們就不起程,直等到雲彩收上去。
Lakini kama wingu haliku nyanyuka juu kutoka hema ya kukutania, kisha basi watu hawaku safiri. Walibaki hadi siku lilipo nyanyuliwa juu.
38 日間,耶和華的雲彩是在帳幕以上;夜間,雲中有火,在以色列全家的眼前。在他們所行的路上都是這樣。
Kwa kuwa wingu la Yahweh lilikuwa juu ya hema ya kukutania mchana, na moto wake ulikuwa juu yake usiku, wazi kwa watu wote wa Israeli kipindi chote cha safari yao.