< 出埃及記 28 >

1 「你要從以色列人中,使你的哥哥亞倫和他的兒子拿答、亞比戶、以利亞撒、以他瑪一同就近你,給我供祭司的職分。
Umuite Aruni kaka yako na wana wake - Nadabu, na Abihu, na Eleazari, na Ithamari - miongoni mwa wana wa Israeli, ili anitumikie katika kazi ya ukuhani.
2 你要給你哥哥亞倫做聖衣為榮耀,為華美。
Nawe utamfanyia Aruni ndugu yako mavazi matakatifu, kwa utukufu na kwa uzuri.
3 又要吩咐一切心中有智慧的,就是我用智慧的靈所充滿的,給亞倫做衣服,使他分別為聖,可以給我供祭司的職分。
Nawe utawaambia watu wote wenye moyo wa hekima, niliowajaza na roho ya hekima wamfanyie Aruni mavazi ili kumtakasa anitumikie katika kazi ya ukuhani.
4 所要做的就是胸牌、以弗得、外袍、雜色的內袍、冠冕、腰帶,使你哥哥亞倫和他兒子穿這聖服,可以給我供祭司的職分。
Na mavazi watakayoyafanya ni kifuko cha kifuani, na naivera, na joho, na kanzu ya kazi ya urembo, na kilemba, na mshipi; nao watawafanyia Aruni nduguye, na wanawe, mavazi matakatifu ili anitumikie katika kazi ya ukuhani.
5 要用金線和藍色、紫色、朱紅色線,並細麻去做。
Nao wataitwaa dhahabu, na nguo ya rangi ya samawi, na ya rangi ya zambarau, na ya rangi nyekundu.
6 「他們要拿金線和藍色、紫色、朱紅色線,並撚的細麻,用巧匠的手工做以弗得。
Nao waifanye naivera kwa nyuzi za dhahabu, na za samawi, na za zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa kwa kazi ya mstadi.
7 以弗得當有兩條肩帶,接上兩頭,使它相連。
Lazima itakuwa na vipande viwili vya mabegani, vilivyoungana kwenye ncha zake mbili; ili ipate kuunganywa.
8 其上巧工織的帶子,要和以弗得一樣的做法,用以束上,與以弗得接連一塊,要用金線和藍色、紫色、朱紅色線,並撚的細麻做成。
Na mshipi wa kazi ya ustadi ulio juu yake, ili kuifunga mahali pake; utakuwa wa kazi kama ile ya naivera, ya vitu vile vile ya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na ya zambarau, na nyekundu, na kitani nzuri yenye kusokotwa.
9 要取兩塊紅瑪瑙,在上面刻以色列兒子的名字:
Nawe utatwaa vito viwili vya shohamu, ya rangi ya chani-kiwiti, nawe utachora juu yake majina ya wana wa Israeli;
10 六個名字在這塊寶石上,六個名字在那塊寶石上,都照他們生來的次序。
Majina yao sita katika kito kimoja, na majina sita yaliyosalia katika kile kito cha pili, kwa utaratibu wa kuzaliwa kwao.
11 要用刻寶石的手工,彷彿刻圖書,按着以色列兒子的名字,刻這兩塊寶石,要鑲在金槽上。
Kwa kazi mtu mwenye kuchora mawe kama vile muhuri ichorwavyo, utavichora hivi vito viwili, sawasawa na majina ya wana wa Israeli, nawe utavitia katika vijalizo vya dhahabu.
12 要將這兩塊寶石安在以弗得的兩條肩帶上,為以色列人做紀念石。亞倫要在兩肩上擔他們的名字,在耶和華面前作為紀念。
Nawe utavitia vile vito viwili juu ya vipande vya mabegani vya hiyo naivera, viwe vito vya ukumbusho kwa ajili ya wana wa Israeli. Naye Aruni atayachukua majina yao mbele za Yahweh juu ya mabega yake mawili ili kuwa ukumbusho.
13 要用金子做二槽,
Nawe fanya vijalizo viwili vya dhahabu
14 又拿精金,用擰工彷彿擰繩子,做兩條鍊子,把這擰成的鍊子搭在二槽上。」
na mikufu miwili ya dhahabu safi; utaifanya iwe mfano wa kamba, ya kazi ya kusokotwa; nawe uitie ile mikufu ya kazi ya kusokotwa katika vile vijalizo.
15 「你要用巧匠的手工做一個決斷的胸牌。要和以弗得一樣的做法:用金線和藍色、紫色、朱紅色線,並撚的細麻做成。
Nawe lazima utafanya kifuko cha kifuani cha hukumu, kazi ya fundi stadi; utakifanya kwa kuiandama ile kazi ya hiyo naivera. Fanya nyuzi za dhahabu, na za rangi ya samawi, na za rangi ya zambarau, na nyekundu, na kitani safi yenye kusokotwa, ndivyo utakavyokifanya.
16 這胸牌要四方的,疊為兩層,長一虎口,寬一虎口。
Kitakuwa mraba, tena cha kukunjwa; urefu wake utakuwa shibiri moja, na upana wake shibiri moja.
17 要在上面鑲寶石四行:第一行是紅寶石、紅璧璽、紅玉;
Nawe ukijaze viweko vya vito, safu nne za vito; safu moja itakuwa ni akiki, na yakuti ya rangi ya manjano, na baharamani, hivi vitakuwa safu ya kwanza.
18 第二行是綠寶石、藍寶石、金鋼石;
Na safu ya pili itakuwa zumaridi, na yakuti samawi, na almasi.
19 第三行是紫瑪瑙、白瑪瑙、紫晶;
Na safu ya tatu itakuwa hiakintho, na akiki nyekundu, na amethisto.
20 第四行是水蒼玉、紅瑪瑙、碧玉。這都要鑲在金槽中。
Na safu ya nne itakuwa ni zabarajadi, na shohamu, na yaspi. Vito hivyo vitakazwa ndani ya dhahabu kwa kujaa mahali pake.
21 這些寶石都要按着以色列十二個兒子的名字,彷彿刻圖書,刻十二個支派的名字。
Na vile vito vitakuwa sawasawa na majina ya wana wa Israeli, kumi na viwili, sawasawa na majina yao. Mfano wa kuchora kwa muhuri kila kimoja sawasawa na jina lake, vitakuwa vya hizo kabila kumi na mbili.
22 要在胸牌上用精金擰成如繩的鍊子。
Nawe lazima utie katika kile kifuko cha kifuani mikufu mfano wa kamba, ya kazi ya kusokotwa, ya dhahabu safi.
23 在胸牌上也要做兩個金環,安在胸牌的兩頭。
Nawe utie maduara mawili ya dhahabu katika kile kifuko cha kifuani, na kuzitia hizo pete mbili katika ncha mbili za kifuko cha kifuani.
24 要把那兩條擰成的金鍊子,穿過胸牌兩頭的環子。
Nawe utie hiyo mikufu miwili ya dhahabu iliyosokotwa katika zile pete mbili zilizo katika ncha za kifuko cha kifuani.
25 又要把鍊子的那兩頭接在兩槽上,安在以弗得前面肩帶上。
Na ncha zile nyingine za hiyo mikufu miwili ya kusokotwa utazitia katika vile vijalizo viwili, na kuvitia katika vile vipande vya mabegani vya naivera upande wa mbele.
26 要做兩個金環,安在胸牌的兩頭,在以弗得裏面的邊上。
Nawe utafanya viduara vili vya dhahabu, uzitie katika hizo ncha mbili za kifuko cha kifuani, katika ukingo wake.
27 又要做兩個金環,安在以弗得前面兩條肩帶的下邊,挨近相接之處,在以弗得巧工織的帶子以上。
Nawe lazima ufanye viduara vili vya dhahabu, na kuzitia katika vile vipande viwili vya mabegani vya ile naivera chini yake, upande wa mbele, karibu na kifungo chake, juu ya huo mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi.
28 要用藍細帶子把胸牌的環子與以弗得的環子繫住,使胸牌貼在以弗得巧工織的帶子上,不可與以弗得離縫。
Nao watakikaza kile kileso kwa vile viduara vyake kwenye viduara za naivera kwa ukanda wa rangi ya samawi, ili kwamba kikae pale juu ya ule mshipi wa naivera uliosukwa kwa ustadi, ili kwamba kifuko cha kifuani kisiachane na naivera.
29 亞倫進聖所的時候,要將決斷胸牌,就是刻着以色列兒子名字的,帶在胸前,在耶和華面前常作紀念。
Na Aruni atayachukua majina ya wana wa Israeli katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu juu ya moyo wake kwa kufanya maamuzi, hapo atakapoingia ndani ya mahali patakatifu, kuwa ukumbusho mbele yaYahweh daima.
30 又要將烏陵和土明放在決斷的胸牌裏;亞倫進到耶和華面前的時候,要帶在胸前,在耶和華面前常將以色列人的決斷牌帶在胸前。」
Nawe utie hizo Urimu na Thumimu katika kile kifuko cha kifuani cha hukumu; nazo zitakuwa juu ya moyo wa Aruni, hapo atakapoingia ndani mbele ya Yahweh na Aruni atachukua hukumu ya hao wana wa Israeli juu ya moyo wake mbele ya Yahweh daima.
31 「你要做以弗得的外袍,顏色全是藍的。
Nawe fanya hiyo joho ya naivera ya rangi ya samawi yote.
32 袍上要為頭留一領口,口的周圍織出領邊來,彷彿鎧甲的領口,免得破裂。
Nayo itakuwa na tundu katikati yake kwa kupitisha kichwa; itakuwa na utepe wa kazi ya kusokotwa kuzunguka hilo tundu lake, mfano wa tundu lililo katika kanzu ya chuma, ili lisipasuke.
33 袍子周圍底邊上要用藍色、紫色、朱紅色線做石榴。在袍子周圍的石榴中間要有金鈴鐺:
Nawe katika pindo zake utatia makomamanga ya rangi ya samawi, na ya rangi ya zambarau, na ya rangi nyekundu, kuzunguka pindo zake kotekote; na njuga za dhahabu kati ya hayo makomamanga pande zote.
34 一個金鈴鐺一個石榴,一個金鈴鐺一個石榴,在袍子周圍的底邊上。
Kengele ya dhahabu na komamanga, kengele ya dhahabu na komamanga, katika pindo za joho kuizunguka pande zote.
35 亞倫供職的時候要穿這袍子。他進聖所到耶和華面前,以及出來的時候,袍上的響聲必被聽見,使他不至於死亡。
Nayo itakuwa juu ya Aruni akitumika; na sauti ya hizo kengele itasikilikana hapo aingiapo ndani ya mahali patakatifu mbele ya Yahweh na hapo atokapo nje, ili kwamba asife.
36 「你要用精金做一面牌,在上面按刻圖書之法刻着『歸耶和華為聖』。
Nawe fanya bamba la dhahabu safi na kuchora juu yake, mfano wa machoro ya muhuri, “Mtakatifu kwa Yahweh.”
37 要用一條藍細帶子將牌繫在冠冕的前面。
Nawe ulitie hilo bamba katika ukanda wa rangi ya samawi, nalo litakuwa katika kile kilemba; litakuwa upande wa mbele wa kile kilemba.
38 這牌必在亞倫的額上,亞倫要擔當干犯聖物條例的罪孽;這聖物是以色列人在一切的聖禮物上所分別為聖的。這牌要常在他的額上,使他們可以在耶和華面前蒙悅納。
Nalo litakuwa katika kipaji cha uso cha Aruni, na Aruni atauchukua uovu wa vile vitu vitakatifu, watakavyovitakasa hao wana wa Israeli katika vipawa vyao vyote vitakatifu, nalo litakuwa katika kipaji chake cha uso sikuzote, ili kwamba vipate kukubaliwa mbele za Yahweh.
39 要用雜色細麻線織內袍,用細麻布做冠冕,又用繡花的手工做腰帶。
Na hiyo kanzu utaifuma ya kitani nzuri ya kazi ya urembo, ufanye na kilemba cha nguo ya kitani nzuri, nawe utafanya mshipi wa kazi ya mwenye kutia taraza.
40 「你要為亞倫的兒子做內袍、腰帶、裹頭巾,為榮耀,為華美。
Kisha utafany kanzu kwa ajili ya wana wa Aruni, nawe wafanyie mishipi, wafanyie na kofia kwa utukufu na uzuri.
41 要把這些給你的哥哥亞倫和他的兒子穿戴,又要膏他們,將他們分別為聖,好給我供祭司的職分。
Nawe mvike huyo nduguye Aruni na wanawe nao mavazi hayo; nawe watie mafuta, na kuwaweka kwa kazi takatifu, na kuwatakasa, ili wapate kunitumikia mimi katika kazi ya ukuhani.
42 要給他們做細麻布褲子,遮掩下體;褲子當從腰達到大腿。
Nawe wafanyie suruali za nguo ya kitani, ili kufunika tupu ya miili yao; suruali hizo zitafika tangu kiunoni hata mapajani.
43 亞倫和他兒子進入會幕,或就近壇,在聖所供職的時候必穿上,免得擔罪而死。這要為亞倫和他的後裔作永遠的定例。」
Aruni na wanawe watazivaa, hapo watakapoingia katika hema ya kukutania, au hapo watakapoikaribia madhabahu ili watumike katika mahali patakatifu; wasije wakachukua uovu, wakafa; hii itakuwa ni amri ya milele kwake yeye, na kwa wazao wake.

< 出埃及記 28 >