< 以斯帖記 2 >

1 這事以後,亞哈隨魯王的忿怒止息,就想念瓦實提和她所行的,並怎樣降旨辦她。
Baada ya mambo haya na baada ya hasira ya mfalme Ahusiero kutulia, alifikiri kuhusu Malkia Vashiti na alichokuwa amekifanya na tangazo alilokuwa ameamuru litolewe ya Vashiti kupoteza sifa za kuwa malkia.
2 於是王的侍臣對王說:「不如為王尋找美貌的處女。
Kisha vijana waliomtumikia mfalme wakasema, mfalme atafutiwemabikira warembo.
3 王可以派官在國中的各省招聚美貌的處女到書珊城的女院,交給掌管女子的太監希該,給她們當用的香品。
Mfalme na achague wasimamizi katika majimbo yote ya ufalme wake, ili wawakusanye mabikira warembo wote harem katika ikulu ya Susa. Mabikira hawa wawe chini ya usimamizi wa Hegai, msimamizi, ambaye ni mkuu wa wanawake, na wapewe vipodozi vyao vyote.
4 王所喜愛的女子可以立為王后,代替瓦實提。」王以這事為美,就如此行。
Na binti yule atakaye mfurahisha mfalme ndiye atakaye kuwa Malkia badala ya Vashiti.” Mfalme alupenda ushauri na akafanya kama alivoshauriwa,
5 書珊城有一個猶大人,名叫末底改,是便雅憫人基士的曾孫,示每的孫子,睚珥的兒子。
Katika mji wa Shushani alikuwepo Myahudi aliyeitwa Modekai mwana wa Jaira mwana wa Shimei mwana wa Kishi, aliye kuwa wa kabila la Benjamini.
6 從前巴比倫王尼布甲尼撒將猶大王耶哥尼雅和百姓從耶路撒冷擄去,末底改也在其內。
Yeye ni miongoni mwa Wayahudi waliochukuliwa pamoja na Yekonia, mfalme wa Yuda kutoka Yerusalemu na kupelekwa uhamishoni na mfalme Nebukadreza.
7 末底改撫養他叔叔的女兒哈大沙(後名以斯帖),因為她沒有父母。這女子又容貌俊美;她父母死了,末底改就收她為自己的女兒。
Modekai alikuwa akimlea, Hadasa, yaani Esta, binti wa mjomba wake kwa sababu hakuwa na wazaai wake wote wawili. Modekai alimchukuwa kama binti yake. Esta alikuwa na umbo zuri na uso wa kupendeza.
8 王的諭旨傳出,就招聚許多女子到書珊城,交給掌管女子的希該;以斯帖也送入王宮,交付希該。
Wasichana wengi waliletwa ikulu Shushani, baada ya tangazo na amri ya mfalme kutolewa. Waliwekwa chini ya usimamizi wa Hegai. Esta naye alikuwa ni miongoni mwa wasichana walioletwa na kuwekwa chini ya usimamizi wa Hegai, mwangalizi wa wanawake.
9 希該喜悅以斯帖,就恩待她,急忙給她需用的香品和她所當得的分,又派所當得的七個宮女服事她,使她和她的宮女搬入女院上好的房屋。
Esta alimfurahisha, na akapata kibali mbele ya Hegai. Akampa vipodozi na sehemu ya chakula. Akampa wahudumu wa kike saba kutoka katika ikulu ya mfalme, na akampeleka na wahudumu wa kike katika sehemu bora katika nyumba ya wanawake.
10 以斯帖未曾將籍貫宗族告訴人,因為末底改囑咐她不可叫人知道。
Esta hakuwa amemweleza mtu yeyote kuhusu jamaa zake kwa sababu Modekai alikuwa amemzuia.
11 末底改天天在女院前邊行走,要知道以斯帖平安不平安,並後事如何。
kila siku Modekai alienda na kurudi mbele nje ya ua wa nyumba ya wanawake, ili kwamba asikie kuhusu mambo ya Esta na atakachofanyiwa.
12 眾女子照例先潔淨身體十二個月:六個月用沒藥油,六個月用香料和潔身之物。滿了日期,然後挨次進去見亞哈隨魯王。
Zamu ilipofika ya kila msichana kwenda kwa mfalme Ahusero kwa kufuata maelekezo kwa wanawake, kila msichana alitakiwa kumaliza miezi kumi na miwili ya urembo, miezi sita ya mafuta ya manemane na miezi sita ya vipodozi.
13 女子進去見王是這樣:從女院到王宮的時候,凡她所要的都必給她。
wakati msichana alipoenda kwa mfalme, alipewa chochote alichotamani kutoka katika nyumba ya wanawake ili aende nacho katika nyuma ya mfalme.
14 晚上進去,次日回到女子第二院,交給掌管妃嬪的太監沙甲;除非王喜愛她,再提名召她,就不再進去見王。
Msichana alipaswa kwenda wakati wa usiku na kurudi katika nyumba ya wanawake, na kwa msimamizi Shaashigazi, msimamizi wa mfalme, ambaye alikuwa mwenye kuwalinda masulia. Msichana hakuruhusiwa kwenda tena kwa mfalme isipokuwa amemfurahiha mfalme na mfalme akaamuru arudi tena.
15 末底改叔叔亞比孩的女兒,就是末底改收為自己女兒的以斯帖,按次序當進去見王的時候,除了掌管女子的太監希該所派定給她的,她別無所求。凡看見以斯帖的都喜悅她。
Zamu ya Esta ilipotimia( mwana wa Abihaili, mjomba wa Modekai alikuw amemchukua kama kama binti yake) kwenda mbele ya mfalme, hakutaka kitu chochote isipokuwa vile ambavyo Hegai, msimamizi wa wanawake alimtaka avichukue.
16 亞哈隨魯王第七年十月,就是提別月,以斯帖被引入宮見王。
Esta akapata kibali mbele ya kila aliyemwona. Esta akapelekwa kwa Mfalme Ahusiero katika makazi ya kifalme mwezi wa kumi, ambao ni mwezi wa Tabeti, katika mwaka wa saba wa utawala wake.
17 王愛以斯帖過於愛眾女,她在王眼前蒙寵愛比眾處女更甚。王就把王后的冠冕戴在她頭上,立她為王后,代替瓦實提。
Mfalme alimpenda Esta zaidi kuliko wanawake wengine, na alipata kibali kuliko na wema mbele zake zaidi kuliko mabikira wengine na hivyo mfalme akamvika taji ya kimalkia badala ya Vashiti.
18 王因以斯帖的緣故給眾首領和臣僕設擺大筵席,又豁免各省的租稅,並照王的厚意大頒賞賜。
mfalme akawafanyia karamu kubwa wasimamizi na wahudumu wake wote, karamu ya Esta na akawapa unafuu wa kodi katika majimbo. Pia akawapa zawadi kwa ukarimu.
19 第二次招聚處女的時候,末底改坐在朝門。
Modekai alikuwa ameketi katika lango la mfalme wakati mabikira walipokuwa wamekusanyika kwa mara ya pili.
20 以斯帖照着末底改所囑咐的,還沒有將籍貫宗族告訴人;因為以斯帖遵末底改的命,如撫養她的時候一樣。
Esta alifuata ushauri Modekai ya kutomwambia mtu yeyote kuhusu jamaa zake. aliendelea kufuata ushauri wa Modekai kama alivyofanya alipokuwa mdogo.
21 當那時候,末底改坐在朝門,王的太監中有兩個守門的,辟探和提列,惱恨亞哈隨魯王,想要下手害他。
katika siku hizo ambazo Modekai alikuwa ameketi getini kwa mfalme, Bighani na Tereshi, wasimamizi wa mfalme walio linda lando, walikasirika na wakatafuta kumuua mfalme Ahusiero.
22 末底改知道了,就告訴王后以斯帖。以斯帖奉末底改的名,報告於王;
Jambo lilipowekwa wazi kwa Modekai, alimtaarifu Malkia Esta na Esta akamweleza kile achoelezwa na Modekai.
23 究察這事,果然是實,就把二人掛在木頭上,將這事在王面前寫於歷史上。
Habari hii ilipepelelezwa na kuonekana kuwa kweli na wanaume wawili walinyongwa juu ya mti. Na habari hii ikaandikwa katika kitabu cha taarifa mbele ya mfalme.

< 以斯帖記 2 >