< 申命記 19 >

1 「耶和華-你上帝將列國之民剪除的時候,耶和華-你上帝也將他們的地賜給你,你接着住他們的城邑並他們的房屋,
Wakati Yahwe Mungu wenu anayafutilia mbali mataifa, yale ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa nchi yao, na wakati mnakuja kwao na kuishi katika miji yao na nyumba,
2 就要在耶和華-你上帝所賜你為業的地上分定三座城。
mnapaswa kuchagua miji mitatu kwa ajili yenu katikati mwa nchi yenu ambayo Yahwe Mungu anawapa kuimiliki.
3 要將耶和華-你上帝使你承受為業的地分為三段;又要預備道路,使誤殺人的,都可以逃到那裏去。
Mnapaswa kujenga barabara na kugawa mipaka ya nchi yenu katika maeneo matatu, nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anafanya kuimiliki, ili kwamba kila mmoja anayeua mtu mwingine apate kukimbia hapo.
4 「誤殺人的逃到那裏可以存活,定例乃是這樣:凡素無仇恨,無心殺了人的,
Hii ni sheria kwa ajili ya mtu anayeua mwingine na anayekimbilia huko kuishi: yeyote auae jirani yake bila kujua, na hapo awali hakumchukia-
5 就如人與鄰舍同入樹林砍伐樹木,手拿斧子一砍,本想砍下樹木,不料,斧頭脫了把,飛落在鄰舍身上,以致於死,這人逃到那些城的一座城,就可以存活,
kama wakati mtu aingiapo katika msitu pamoja na jirani yake kukata kuni, na mkono wake ukata mti chini kwa shoka, na kichwa uteleza kutoka kwenye mpini na kumpiga jirani yake mpaka akafa- basi mtu huyu anapaswa kukimbilia katika moja ya miji hii na kuishi.
6 免得報血仇的,心中火熱追趕他,因路遠就追上,將他殺死;其實他不該死,因為他與被殺的素無仇恨。
Vinginevyo damu ya mlipiza kisasi atamfuata yeye aliyetoa uhai, na kwa hasira kali anampita kwa sababu ilikuwa safari ndefu. Na anampiga na kumuua, ijapokuwa mtu huyo akustahili kufa; na hata akustahili adhabu ya kifo kwa sababu hakumchukia jirani yake kabla hili halijatokea.
7 所以我吩咐你說,要分定三座城。
Basi sasa ninakuamuru kuchagua miji mitatu kwa ajili yako.
8 耶和華-你上帝若照他向你列祖所起的誓擴張你的境界,將所應許賜你列祖的地全然給你,
Kama Yahwe Mungu wenu apanua mipaka yenu, kama alivyoapa kwa mababu zenu kufanya, na kuwapa nchi yote ambayo amewaahadia kuwapa mababu zenu;
9 你若謹守遵行我今日所吩咐的這一切誡命,愛耶和華-你的上帝,常常遵行他的道,就要在這三座城之外,再添三座城,
kama mnazishika amri hizi zote kuzifanya, ambazo ninakuamuru leo- amri za kumpenda Yahwe Mungu wenu na daima kutembea katika njia zake, basi mnapaswa kuongeza miji mitatu zaidi kwa ajili yenu, isipokuwa ile mitatu.
10 免得無辜之人的血流在耶和華-你上帝所賜你為業的地上,流血的罪就歸於你。
Fanya hivi ili kwamba damu isiyo na hatia isimwangwe katikati ya nchi ambayo Yahwe Mungu wenu anawapa kwa ajili ya urithi, ili kwamba pasiwepo hatia ya damu kwenu.
11 「若有人恨他的鄰舍,埋伏着起來擊殺他,以致於死,便逃到這些城的一座城,
Lakini kama yeyote anamchukia jirani yake, uongo unamsubiri, uinuka dhidi yake, na majeraha ya kufa kwake ili kwamba anakufa, na kama basi anakimbia katika moja ya miji hii-
12 本城的長老就要打發人去,從那裏帶出他來,交在報血仇的手中,將他治死。
basi wazee wa mji wake wanapaswa kumtoa na kumrudisha toka huko, na kumkabizi katika mkono wa ndugu mhusika, ili kwamba amuue.
13 你眼不可顧惜他,卻要從以色列中除掉流無辜血的罪,使你可以得福。」
Jicho lako halipaswi kumuonea huruma; badala yake; unapaswa kuondoa hatia ya damu kutoka Israel, ili kwamba iwe vizuri kwako.
14 「在耶和華-你上帝所賜你承受為業之地,不可挪移你鄰舍的地界,那是先人所定的。」
Haupaswi kuondoa alama ya jirani yako ambayo wameweka katika eneo muda mrefu, katika urithi wako ambao utarithi, katika nchi ambayo Yahwe Mungu wako anakupa kumiliki.
15 「人無論犯甚麼罪,作甚麼惡,不可憑一個人的口作見證,總要憑兩三個人的口作見證才可定案。
Shahidi moja peke hapaswi kuinuka dhidi ya mtu kwa ajili ya uovu wowote, au kwa ajili ya dhambi yoyote, katika jambo lolote ambalo amefanya dhambi; kwa kinywa cha mashahidi wawili, au kwa kinywa cha mashahidi watatu, kunapaswa jambo lolote lilithibitishwe.
16 若有凶惡的見證人起來,見證某人作惡,
Kama ushuhuda wa mtu asiye na haki anainua dhidi ya mtu yeyote kushuhudia dhidi yake kwa mambo mabaya.
17 這兩個爭訟的人就要站在耶和華面前,和當時的祭司,並審判官面前,
Basi watu wote wawili, mmoja kati ya yule utata upo, anapaswa kusimama mbele ya Yahwe, mbele ya makuhani na waamuzi ambao wanatumika siku hizo.
18 審判官要細細地查究,若見證人果然是作假見證的,以假見證陷害弟兄,
Waamuzi wanapaswa kuchunguza kwa uangalifu; ona, kama ushahidi ni ushahidi wa uongo na umeshuhudiwa kwa uongo dhidi ya ndugu yake,
19 你們就要待他如同他想要待的弟兄。這樣,就把那惡從你們中間除掉。
basi unapaswa kufanya kwake, kama alivyokusudia kufanya kwa ndugu yake, na utaondoa uovu kutoka miongoni mwenu.
20 別人聽見都要害怕,就不敢在你們中間再行這樣的惡了。
Basi wale wanaobaki watasikia na kuogopa, na kuanzia hapo na kuendelea hawatafanya tena aina ya ouvu miongoni mwao.
21 你眼不可顧惜,要以命償命,以眼還眼,以牙還牙,以手還手,以腳還腳。」
Macho yako hapaswi kuona huruma; maisha yatalipa kwa maisha, jicho kwa jicho, jino kwa jino, mkono kwa mkono, mguu kwa mguu.

< 申命記 19 >