< 但以理書 4 >

1 尼布甲尼撒王曉諭住在全地各方、各國、各族的人說:「願你們大享平安!
Mfalme Nebukadneza aliituma amri hii kwa watu wote, mataifa, na lugha walioishi katika nchi: “Na amani yenu na iongezeke.
2 我樂意將至高的上帝向我所行的神蹟奇事宣揚出來。
Imeonekana vizuri kwangu kuwaambia juu ya ishara na maajabu ambayo Mungu Mkuu Aliye juu amenifanyia.
3 他的神蹟何其大! 他的奇事何其盛! 他的國是永遠的; 他的權柄存到萬代!
Ni kwa namna gani Ishara zake ni kubwa, na ni kwa namna gani maajabu yake yana nguvu! Ufalme wake ni ufalme unaodumu milele, na utawala wake hudumu kizazi hadi kizazi.”
4 「我-尼布甲尼撒安居在宮中,平順在殿內。
Mimi, Nebukadneza, nilikuwa ninaishi kwa furaha katika nyumba yangu, na nilikuwa nikifurahia mafanikio katika ikulu yangu.
5 我做了一夢,使我懼怕。我在床上的思念,並腦中的異象,使我驚惶。
Lakini ndoto niliyoiota ilifanya niogope. Nilipokuwa nimejilaza pale, taswira niliyoiona na maono katika akili yangu yalinitaabisha.
6 所以我降旨召巴比倫的一切哲士到我面前,叫他們把夢的講解告訴我。
Basi nilitoa agizo la kuwaleta mbele yangu watu wote wa Babeli waliokuwa na hekima ili kwamba waweze kunitafsiria ndoto.
7 於是那些術士、用法術的、迦勒底人、觀兆的都進來,我將那夢告訴了他們,他們卻不能把夢的講解告訴我。
Kisha walikuja wachawi, wale ambao hudai kuzungumza na wafu, watu wenye hekima, na wasoma nyota. Niliwaambia juu ya ndoto, lakini hawakuweza kunitafsiria.
8 末後那照我神的名,稱為伯提沙撒的但以理來到我面前,他裏頭有聖神的靈,我將夢告訴他說:
Bali mwishoni Danieli aliingia ndani - yeye ambaye huitwa Belteshaza jina la mungu wangu, na ambaye ndani yake kuna roho ya miungu mitakatifu - na nilimwambia juu ya ndoto.
9 『術士的領袖伯提沙撒啊,因我知道你裏頭有聖神的靈,甚麼奧祕的事都不能使你為難。現在要把我夢中所見的異象和夢的講解告訴我。』
“Belteshaza, mkuu wa wachawi, ninajua kuwa roho ya miungu watakatifu iko ndani yako na ya kwamba hakuna siri iliyo ngumu kwako. Niambie kile nilichokiona katika ndoto yangu na nini maana yake.
10 「我在床上腦中的異象是這樣:我看見地當中有一棵樹,極其高大。
Haya ndiyo niliyoyaona katika akili zangu nilipokuwa nimejilaza katika kitanda changu: Nilitazama, na kulikuwa na mti katikati ya dunia, na urefu wake ulikuwa ni mkubwa sana.
11 那樹漸長,而且堅固,高得頂天,從地極都能看見,
Mti ulikua na ukawa wenye nguvu. Na sehemu ya juu yake ilifika mbinguni, uliweza kuonekana kutoka miisho ya dunia yote.
12 葉子華美,果子甚多,可作眾生的食物;田野的走獸臥在蔭下,天空的飛鳥宿在枝上;凡有血氣的都從這樹得食。
Majani yake yalikuwa mazuri, matunda yake yalikuwa ni mengi, na juu yake kulikuwa na chakula kwa ajili ya wote. Wanyama wa mwituni walipata kivuli chini yake, na ndege wa angani waliisha katika matawi yake. Viumbe vyote hai vililishwa katika mti huo.
13 「我在床上腦中的異象,見有一位守望的聖者從天而降。
Nilipokuwa nimelala kitandani kwangu, niliona katika akili zangu, mjumbe mtakatifu alishuka kutoka mbinguni.
14 大聲呼叫說:『伐倒這樹!砍下枝子!搖掉葉子!拋散果子!使走獸離開樹下,飛鳥躲開樹枝。
Alipiga kelele na kusema, 'Ukateni mti na yafyekeni matawi yake, yapukutisheni majani yake, na kuyasambaza matunda yake. Wanyama na wakimbie kutoka chini yake na ndege wapae mbali kutoka katika matawi yake.
15 樹墩卻要留在地內,用鐵圈和銅圈箍住,在田野的青草中讓天露滴濕,使他與地上的獸一同吃草,
Mkiache kisiki cha mizizi yake katika nchi, mkifunge na fungu la chuma na shaba, katikati ya mche mororo wa shambani. Na kilowanishwe na umande wa kutoka mbinguni. Kiacheni kiishi na wanyama kati ya mimea ya ardhini.
16 使他的心改變,不如人心,給他一個獸心,使他經過七期。
Akili yake na ibadilishwe kutoka akili ya kibinadamu, na apewe akili ya mnyama mpaka ipite miaka saba.
17 這是守望者所發的命,聖者所出的令,好叫世人知道至高者在人的國中掌權,要將國賜與誰就賜與誰,或立極卑微的人執掌國權。』
Uamuzi huu ni kutokana na amri iliyotolewa na mjumbe. Ni uamuzi uliofanya na yeye aliye mtakatifu ili kwamba hao walio hai wajue kwamba Mungu aliye juu sana anatawala juu ya falme za watu na huwapa kwa kila mmoja apendaye kumweka juu yao, hata kwa watu wale wanyenyekevu sana.'
18 「這是我-尼布甲尼撒王所做的夢。伯提沙撒啊,你要說明這夢的講解;因為我國中的一切哲士都不能將夢的講解告訴我,惟獨你能,因你裏頭有聖神的靈。」
Mimi, Mfalme Nebukadneza nilipata ndoto hii. Sasa, wewe Belteshaza, niambie tafsiri yake, kwasababu hakuna mtu mwenye hekima katika ufalme wangu anayeweza kunitafsiria. Lakini wewe unaweza kufanya hivyo, kwa kuwa roho ya miungu watakatifu iko ndani yako.”
19 於是稱為伯提沙撒的但以理驚訝片時,心意驚惶。王說:「伯提沙撒啊,不要因夢和夢的講解驚惶。」伯提沙撒回答說:「我主啊,願這夢歸與恨惡你的人,講解歸與你的敵人。
Ndipo Danieli aliyeitwa pia Belteshaza, alihuzunishwa kwa muda, na mawazo yake yalimshitua. Mfalme akasema, “Belteshaza, usifadhaishwe na ndoto au tafsiri yake.” Belteshaza akajibu, “Bwana wangu, ndoto hii na iwe kwa ajili ya watu wanaokuchukia, na tafsiri yake na iwe kwa ajili ya adui zako.
20 你所見的樹漸長,而且堅固,高得頂天,從地極都能看見;
Mti ule uliouona - uliokua na ukawa na wenye nguvu, na ambao sehemu yake ya juu ilifika hata mbinguni, na ambao waweza kuonekana kutoka miisho ya dunia yote -
21 葉子華美,果子甚多,可作眾生的食物;田野的走獸住在其下;天空的飛鳥宿在枝上。
ambao majani yake ni mazuri, na matunda yake yalikuwa ni mengi, ili kwamba ndani yake kulikuwa na chakula cha wote, na chini yake wanyama wa mwituni walipata kivuli, na ndani yake ndege wa angani waliishi -
22 「王啊,這漸長又堅固的樹就是你。你的威勢漸長及天,你的權柄管到地極。
huu mti ni wewe, mfalme, wewe uliyekua na kuwa na nguvu. Ukuu wako umeongezeka na kufika mbinguni, na mamlaka yako yamefika hata miisho ya dunia.
23 王既看見一位守望的聖者從天而降,說:『將這樹砍伐毀壞,樹墩卻要留在地內,用鐵圈和銅圈箍住;在田野的青草中,讓天露滴濕,使他與地上的獸一同吃草,直到經過七期。』
Ewe mfalme, ulimwona mjumbe akishuka kutoka mbinguni na akisema, “Ukateni mti na uteketezeni, lakni kiacheni kisiki cha mizizi yake katika nchi, kifungeni kwa ukanda wa chuma na shaba, katikati ya mche mororo katika shamba. Na kilowanishwe na umande kutoka mbinguni. Kiache kiishi katika wanyama wa mwituni katika mashamba mpaka ipite miaka saba.'
24 「王啊,講解就是這樣:臨到我主我王的事是出於至高者的命。
Mfalme, hii ni tafsiri yake. Ni agizo la Yeye Aliye Juu ambalo limekufikia, bwana wangu mfalme.
25 你必被趕出離開世人,與野地的獸同居,吃草如牛,被天露滴濕,且要經過七期。等你知道至高者在人的國中掌權,要將國賜與誰就賜與誰。
Utafukuzwa utoke miongoni mwa watu, na utaishi pamoja na wanyama wa mwituni huko mashambani. Utafanywa uwe unakula majani kama ng'ombe, na utalowanishwa na umande wa kutoka mbinguni, miaka saba itapita mpaka pale utakapokiri kwamba Mungu Aliye Juu anatawala juu ya falme zote za watu na ya kwamba yeye humpa falme hizo mtu yeyote amtakaye.
26 守望者既吩咐存留樹墩,等你知道諸天掌權,以後你的國必定歸你。
Kama ilivyoamriwa kwamba kukiacha kisiki cha mizizi ya mti, kwa njia hii ufalme wako utarudishiwa katika kipindi ambacho utajifunza kwamba mbingu inatawala.
27 王啊,求你悅納我的諫言,以施行公義斷絕罪過,以憐憫窮人除掉罪孽,或者你的平安可以延長。」
Hivyo basi, mfalme, ushauri wangu na ukubalike kwako. Acha kutenda dhambi na utende haki. Geuka uache uovu wako wa kuonesha huruma kwa walionewa, na itakuwa kwamba mafanikio yako yataongezwa.”
28 這事都臨到尼布甲尼撒王。
Vitu hivi vyote vilitokea kwa mfalme Nebukadneza.
29 過了十二個月,他遊行在巴比倫王宮裏。
Baada ya miezi wa kumi na miwili alipokuwa akitembea juu ya dari la ikulu ya kifalme katika Babeli,
30 他說:「這大巴比倫不是我用大能大力建為京都,要顯我威嚴的榮耀嗎?」
na alisema, “Je hii si Babeli kuu, ambayo nimeijenga kwa ajili ya makao yangu ya kifalme, kwa ajili ya utukufu wa enzi yangu?”
31 這話在王口中尚未說完,有聲音從天降下,說:「尼布甲尼撒王啊,有話對你說,你的國位離開你了。
Wakati maneno yakali katika midomo ya mfalme, sauti ilisikika kutoka mbinguni: “Mfalme Nebukadneza, imetangazwa kwako kwamba ufalme huu umeondolewa kutoka kwako.
32 你必被趕出離開世人,與野地的獸同居,吃草如牛,且要經過七期。等你知道至高者在人的國中掌權,要將國賜與誰就賜與誰。」
Utafukuziwa mbali kutoka miongoni mwa watu, na makao yao yatakuwa pamoja na wanyama wa mwitu katika mashamba. Utafanywa kulamajani kama ng'ombe. Miaka saba itapita mpaka pale utakapokiri kwamba Mungu Aliye Juu anatawala juu ya falme za watu na humpa falme mtu yeyote amtakaye.”
33 當時這話就應驗在尼布甲尼撒的身上,他被趕出離開世人,吃草如牛,身被天露滴濕,頭髮長長,好像鷹毛;指甲長長,如同鳥爪。
Agizo hili kinyume na Nebukadneza lilitekelezwa ghafla. Aliondolewa miongoni mwa watu. Alikula majani kama ng'ombe, na mwili wake ulilowa kwa umande wa kutoka mbinguni. Nywele zake zilirefuka kama manyoa ya tai, na makucha yake yalikuwa kama makucha ya ndege.
34 日子滿足,我-尼布甲尼撒舉目望天,我的聰明復歸於我,我便稱頌至高者,讚美尊敬活到永遠的上帝。 他的權柄是永有的; 他的國存到萬代。
Na katika mwisho wa siku, mimi, Nebukadneza niliinua macho yangu kuelekea mbinguni, utimamu wa akili nilirudishiwa. “Nilimsifu Mungu Aliye Juu sana, na nilimheshimu na kumtukuza yeye aishiye milele. Kwa kuwa utawala wake ni wa milele, na ufalme wake unadumu katoka katika vizazi vyote hadi vizazi vyote.
35 世上所有的居民都算為虛無; 在天上的萬軍和世上的居民中, 他都憑自己的意旨行事。 無人能攔住他手, 或問他說,你做甚麼呢?
Wenyeji wote wa duniani huhesabiwa na yeye kuwa bure; hufanya lolote limpendezalo miongoni mwa jeshi la mbinguni na wakazi wa dunia. Hakuna hata mmoja awezaye kumzuia au kumpa changamoto. Hakuna hata mmoja awezaye kumwambia, “Mbona umefanya hivi?”
36 那時,我的聰明復歸於我,為我國的榮耀、威嚴,和光耀也都復歸於我;並且我的謀士和大臣也來朝見我。我又得堅立在國位上,至大的權柄加增於我。
Kwa wakati ule ule utimamu wa akili zangu uliponirudia, utukufu wangu na fahari yangu ilinirudia kwa ajili ya utukufu wa ufalme wangu. Washauri wangu na watu wenye heshima walitafuta msaada wangu. Nilirudishwa kwenye kiti changu cha enzi, na nilipewa ukuu zaidi.
37 現在我-尼布甲尼撒讚美、尊崇、恭敬天上的王;因為他所做的全都誠實,他所行的也都公平。那行動驕傲的,他能降為卑。
Sasa basi, mimi Nebukadneza, ninamsifu, ninamtukuza na kumheshimu mfalme wa mbinguni, kwa kuwa matendo yake yote ni ya haki, na njia zake ni za adili. Anaweza kuwashusha wale wanaotembea katika kiburi chao wenyewe.

< 但以理書 4 >